Diwani wa CCM kata ya Kijichi kizimbani kwa kupokea rushwa ya Tsh. Milioni 1

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
IMG-20200521-WA0189-574x1024.jpg


DIWANI wa Kata ya Kijichi halmashauri ya Manispaa wa Temeke kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), Elias Mtarawanje (29), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke akikabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kupokea rushwa ya Sh. Milioni moja kutoka kwa Yusuf Omary.

Diwani huyo amefikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashtaka yake na mwendesha mashtaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mwanakombo Rajabu mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Catherine Madili.

Akisoma hati ya mashtaka, Rajabu alidai kuwa Februari 6, mwaka huu katika eneo la Mtoni Kijichi lililopo Temeke jijini Dar es Salaam mshtakiwa huyo akiwa kama Diwani wa Kijichi aliomba rushwa ya Sh. Milioni moja kutoka kwa Yusuf Omary kama kishawishi kwake ili hasiweze kuzuia malipo ya fidia la eneo jambo ambalo amelifanya tofauti na mahusiano ya shughuli za mwajiri wake.

Katika shtaka la pili, inadaiwa kuwa Februari 6, mwaka huu, eneo hilo hilo la Mtoni Kijichi mshtakiwa huyo akiwa diwani kwa njia za rushwa alijipatia Sh. Milioni moja kama kishawishi kwake ili hasiweze kuzuia malipo ya fidia la eneo jambo ambalo amelifanya tofauti na mahusiano ya shughuli za mwajiri wake.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo mshtakiwa alikana kutenda makosa hayo, upande wa Takukuru ulidai kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika hivyo wanaomba tarehe kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Akitoa masharti ya dhamana, Hakimu Madili alimtaka mshtakiwa huyo kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bodi ya sh. 500,000 kila mmoja.

Hata hivyo mshtakiwa huyo ameachiwa kwa dhamana, na kesi inayomkabili imeharishwa hadi Juni 3, 2020.
 
...Au sioni vizuri? Hiyo Diwani ana miaka 29 tu kweli?
Mbona kama ni MTU mzima Fulani hivi ?...
 
Back
Top Bottom