Mkuu Ngongo,
Wewe unajulikana hapa JF kua hua unapinga kila jambo hata liwe jema linalofanywa na Mh Lema na CDM kwa ujumla.Kwa sababu hiyo huwezi hata siku moja ku judge jambo linalofanywa na CDM katika fair ground.Ngongo,huyu diwani alichaguliwa na watu (majority) kwenye kata yake,hivyo wewe peke yako huwezi kusema ati sio mpiganaji na hajui analopigania,ati hana msimamo.Wananchi walimwamini wakampa nafasi hiyo akiwa CCM. Wewe umemwona hivyo kwa sababu tu kahamia CDM.
Vyama vya CCM na CDM vimekuwa vikichukuliana wanachama pale mikutano yao inapofanyika,Majuzi tumesikia ngeleja amewachukua viongozi kadhaa wa CDM. Hatukuona comment yako kwamba CCM imefanya jambo la kipumbavu kuchukua hao wana CDM.Je iweje leo useme kuwa CDM imefanya jambo la kipumbavu.All in all hata wewe tunakukaribisha CDM pale utakapokuwa umeuelewa ukweli.Najua saivi ni hasira tu.