I once said that it will not be too easy for CDM. Kasi na mtindo wa utendaji wa CDM utawashinda wengi waliojiunga wakifikiri ni CCM mbadala. Wasioweza wajiondoe lakini hawatazuia mabadiliko ambayo hii nchi inahitaji. CCM hawabembelezwi kwa sababu hawabembelezeki. Lugha wanayoielewa ni ya jino kwa jino. Huwezi kumuokoa ndugu yako kutoka makucha ya simba kwa kumchekea, na wewe utakuwa mlo.
Wapo wengi sana wataondoka kwa namna hii. Cha muhimu ni uongozi wa CDM kuandaa makada wengi wanaoelewa itikadi ya chama ili kuweza kupata viongozi wazuri baada ya hawa mamluki kujiengua. Yaliyotokea Mbeya kwa Shitambala yaendelee kutoka ngazi za vijiji, kata, tarafa, wilaya, mikoa na taifa. Wasioweza, wakifikiri siasa ni kazi ya kuwapatia kipato waondoke.