Diwani CCM akimbilia Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diwani CCM akimbilia Chadema

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 22, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Diwani wa Kata ya Endasaki, wilayani Hanang, Mkoa wa Manyara kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hashimu Muna Kamunga, ametangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa maelezo kuwa amekuwa akiandamwa kushirikiana na upinzani.
  Diwani huyo alitangaza uamuzi wa kuihama CCM juzi mchana katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Endasaki.
  Kamunga alisema kuwa kabla ya kuchukua hatua hiyo, viongozi kadhaa wa CCM walikuwa wakimshutumu na kumshinikiza kuwa anashilikiana na vyama vya upinzani.
  Alisema kuwa amechukua uamuzi huo kutokana na chama chake kutokuwa na imani naye na kuonekana kama msaliti, wakati madai dhidi yake hayakuwa na ukweli wowote.
  Kamunga alisema kuwa CCM ni chama cha ajabu na kwamba kuna wanachama na viongozi wachache wenye chuki, fitina na ubinafsi.
  Alisema: “Mimi nilikuwa na msimamo wangu wa kutetea wananchi na kuwa mkweli wa kila jambo la maendeleo, katika kata yangu tulikuwa mbele.”
  Kutokana na uamuzi wake wa kujiondoa CCM, Kata ya Endasaki imebaki bila diwani hadi hapo uchaguzi mpya utakapoitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).

  “Kata ya Endasaki iko wazi, umma wa Tanzania wajue hilo na tunasubiri tu uchanguzi mdogo ili tuone ukweli uko wapi kati yangu na wana-CCM na wananchi kwa ujmla,” alisema.

  Katika mkutano huu, Kamunga alirundisha vifaa mbalimbali vya CCM ikiwemo kadi, ilani na sare za chama hicho.
  Zaidi ya wanachama 30 wa CCM walihamasika na kuamua kujiunga na Chadema hapo uwanjani na kukabidhi kadi kwa Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila.

  Naye Mbuge wa Viti Maalum (Chadema), Rose Kamili, alisema kuwa CCM ina wakati mgumu sana.
  “Huyu jamaa (Kamunga) anakubalika kwa watu…Sasa Endasaki ipo wazi, tusubiri uchanguzi mdogo ufanyike ili tushinde kwa sababu huyu anakumbalika,” alisema Kamili.

  Kamili alisema: Tutaendelea kuibomoa CCM mpaka kieleweke, waache ufisadi wanaonaendelea nao wa kutesa wananchi. Kwa sasa umefika wakati wa kuacha malumbano na kuleta maendeleo kwa wananchi wetu, sio wa Chadema wala kwa CCM pekee.”
  Kamili alisema kuwa kwa sasa ni wakati wa kuwaelenza wananchi umuhimu wa kukiunga mkono Chadema kwa sababu ndicho chama mbadala ambacho kinawenza kuboresha maisha ya Watanzania walio wengi.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hivi huwa inakuweje diwani agombee kwa chama tawala then hata muda haupiti baada ya kuchaguliwa anahama hii ni kwamba alikua mamluki ama??
   
 3. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Chama kimekosa kujiamini, na hizo ni dalili za kuelekea kufa!!:kev:
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Sijaona sababu ya msingi aliyoitoa... hana msimamo na ni myu asiyeweza kutetea msimamo wake. Ina maana hata akiwa aupinzani akianza kuandamwa kuisaidia CCM atarudi hukohuko
   
 5. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  matatizo kama haya huwa yanacost vyama vingi sana watu huwa wanashindwa kuwa na msimamo mmoja kama viongozi na usishangae mwakani tena akarudi ccm
   
 6. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #6
  Jan 22, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  amechagua fung lililo jema
   
 7. Wakumwitu

  Wakumwitu JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Huyu bwana ana haki ya kujitoa CCM wanapenda mtu ambaye hawasumbui kimtizamo. mfano; ukijidai unajua kutetea sana masilahi ya wananchi wanaanza kukupiga vita kuwa siyo mwenzao kwa sababu fedha zinazotolewa kwa ajili ya maendeleo haziwezi kutafunwa hovyo kama ww una msimamo. Kwa hiyo watafanya kila mbinu uondoke ili watafune vizuri. Nina mpongeza kama kweli alikuwa anatetea wananchi wa kata yake. Ila ajue pia Chadema hakuna longolongo.
   
 8. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  so hapo patahiotajika uchaguzi tena?
   
 9. Taluma

  Taluma Senior Member

  #9
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wote wanaochukizwa na uovu wa CCM inabidi wampongeze huyu mheshimiwa diwani......! ameshinda uchaguzi kwa tiketi ya CCM halafu anawapiga chini kabla hata mwaka haujaisha!
   
 10. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #10
  Jan 22, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  And the music plays...
   
 11. z

  zherc Member

  #11
  Jan 22, 2011
  Joined: Jul 28, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :kev:
   
 12. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #12
  Jan 22, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  sisiemu sasa hv hakuna maslahi watu wanakosa mishahara
   
 13. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #13
  Jan 22, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Tuseme ukweli aliye au anayeshabikia CCM ujue kuna kimkate cha leo anapata anasema kesho potelea mbali!maana utawala mbovu wa ccm unamgusa kila mtu!soma mwananchi ya jana:WENYE VIWANDA KUVIFUNGA WAKATI WOWOTE ni hasara wanayopata kutokana na tanzania kutokua na umeme wa uhakika!hapo ajira kiasi gani kupotea? DRC wana mradi INGA POWER PLANTs wanataka uzalize 100 000MW kutoka 3500MW za sasa!chini ya ccm hata 600mw hatuwezi
   
 14. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #14
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Na bado,
  si mnajua mdhamini wao mkuu RA ndiye anayeteka bakuli alipwe mkwa mgongo wa dowans? Ngoja ikwame au itokee jamaa akamatwe, hapo chama kitatangazwa 'kilikuwepo enzi hizo' maana kitakuwa mfu milele.
  wee acha bana...ipo pabaya ccm sana chalii!
   
 15. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #15
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hapana mkuu CCM ukiwaeleza ukweli unaonekana wewe ni adui,kama kina Sitta na Mwakyembe,sasa ili uendelee na msimamo wako ni bora uwashambulie ukiwa nje,ukiendelea kuwashambulia ukiwa ndani huwa hawachelewi kuku-kolimba.

   
 16. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #16
  Jan 22, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  huyu mdhamini pesa anapata wapi mbona tuna wafanyabiashara wakubwa kuliko yeye hapa bongo lakini hawazungumzwi kama anavyosemwa yeye na itafika kipindi fedha yote itakua mikononi mwa huyu jamaa matokeo yake serikali itaishiwa fedha!tutaindia upya kwenye azimio kama la arusha!kuwanyanganya mabepari!
   
 17. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #17
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Na akirudi huko wanampa kitengo cha uropokaji (propaganda) ili ajimalize kabisa machoni mwa Wadanganyika.

   
 18. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #18
  Jan 22, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hahaaaa kama tambwe
   
 19. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #19
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kama vile ulikuwa akilini mwangu,huyu jamaa wanammaliza.

   
 20. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #20
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Je ni Madiwani wangapi waliokwisha jiuzulu tangu uchaguzi mkuu?
  Kwa wale nilionataarifa nao mpaka sasa ni 5 je kuna wengine unaowafahamu?
  Rolya---------------------- 3
  Arusha-------------------- 1
  Na huyu wa Manyara---- 1
   
Loading...