kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 277
Diwani wa Kata ya Endasaki, wilayani Hanang, Mkoa wa Manyara kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hashimu Muna Kamunga, ametangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa maelezo kuwa amekuwa akiandamwa kushirikiana na upinzani.
Diwani huyo alitangaza uamuzi wa kuihama CCM juzi mchana katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Endasaki.
Kamunga alisema kuwa kabla ya kuchukua hatua hiyo, viongozi kadhaa wa CCM walikuwa wakimshutumu na kumshinikiza kuwa anashilikiana na vyama vya upinzani.
Alisema kuwa amechukua uamuzi huo kutokana na chama chake kutokuwa na imani naye na kuonekana kama msaliti, wakati madai dhidi yake hayakuwa na ukweli wowote.
Kamunga alisema kuwa CCM ni chama cha ajabu na kwamba kuna wanachama na viongozi wachache wenye chuki, fitina na ubinafsi.
Alisema: Mimi nilikuwa na msimamo wangu wa kutetea wananchi na kuwa mkweli wa kila jambo la maendeleo, katika kata yangu tulikuwa mbele.
Kutokana na uamuzi wake wa kujiondoa CCM, Kata ya Endasaki imebaki bila diwani hadi hapo uchaguzi mpya utakapoitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).
Kata ya Endasaki iko wazi, umma wa Tanzania wajue hilo na tunasubiri tu uchanguzi mdogo ili tuone ukweli uko wapi kati yangu na wana-CCM na wananchi kwa ujmla, alisema.
Katika mkutano huu, Kamunga alirundisha vifaa mbalimbali vya CCM ikiwemo kadi, ilani na sare za chama hicho.
Zaidi ya wanachama 30 wa CCM walihamasika na kuamua kujiunga na Chadema hapo uwanjani na kukabidhi kadi kwa Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila.
Naye Mbuge wa Viti Maalum (Chadema), Rose Kamili, alisema kuwa CCM ina wakati mgumu sana.
Huyu jamaa (Kamunga) anakubalika kwa watu Sasa Endasaki ipo wazi, tusubiri uchanguzi mdogo ufanyike ili tushinde kwa sababu huyu anakumbalika, alisema Kamili.
Kamili alisema: Tutaendelea kuibomoa CCM mpaka kieleweke, waache ufisadi wanaonaendelea nao wa kutesa wananchi. Kwa sasa umefika wakati wa kuacha malumbano na kuleta maendeleo kwa wananchi wetu, sio wa Chadema wala kwa CCM pekee.
Kamili alisema kuwa kwa sasa ni wakati wa kuwaelenza wananchi umuhimu wa kukiunga mkono Chadema kwa sababu ndicho chama mbadala ambacho kinawenza kuboresha maisha ya Watanzania walio wengi.
CHANZO: NIPASHE