Hairuhusiwi hata chembe! Tunaomba mifano ku-support madai haya mazito.
Kwa mujibu wa katiba mtu anapopata majukumu ya kisiasa anatakiwa aache utumishi wa uma mara moja.leta majina
Kwa ujumla hata ubunge si ajira hivyo unaweza kuendelea na ajira kama ajira hiyo haiathiriki na vikao vya bunge. Mbunge hana tofauti na diwani, kwani wote ni wawakilishi na si watumishi.
Labda niulize, Je, Shyrose Bhanji ameacha kazi NMB? Jibu lisibadili mwelekeo wa thread lakini kama hajaacha basi nadhani nitaeleweka zaidi.
Mbunge ni mtumishi ndio maana wanapewa barua za ajira zao na ofisi ya Bunge
Barua hata diwani angeweza kupewa.
Kama angeweza kupewa. Je wanapewa?
Wabunge wanalipwa mishahara lakini madiwani hawalipwi. Je ni haki kuwalinganisha.
Hivi kinachomuweka mtu katika kundi fulani ni concept au treatment. Kwa sababu kitendo cha mbunge kupewa barua ni treatment. Kitendo cha diwani kutopewa barua nacho ni treatment.
Concept ni kwamba wote ni representatives kama alivyo Shyrose Bhanji.
Wote ni wawakilishi wa wananchi lakini mmoja analipwa mshahara na mwinginehalipwi. Kwahiyo huyu asiyelipwa mshahara analazimika kutafuta kazi ili kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao.
Mbunge wa JMT pamoja na kuwa ni muwakilishi wa wananchi lakini pia ni mtumishi (mwajiriwa) wa umma.
Diwani ataendelea n utumishi wa umma, lakini si katika halimashaurinnayofania kazi. Mfano Yule wa cdm kule mwnz ni mwalim lakini diwani. Yule anayegombana n wenje.,, udiwani si ajira. Kwa heri
mbona madiwani wengi tu wanapiga kazi kama kawaida. mfano ni wale wafanyakazi wa SUA ambao ni madiwani kwenye sehemu mablimbali za manispaa ya Morogoro. Huenda iko hivyo kwa sababu, madiwani tofauti na wabunge, siyo kazi inayohitaji wawepo kazini (kwenye udiwani) muda wote.
Kwani madiwani wanalipwa mshahara? asipofanya kazi hiyo posho isiyozidi laki tano itamtosha? Navyofahamu madiwani wengi wanatokea vijiweni (Jobless) na baadhi yao wana biashara binafsi ambao huendea nazo hata baada ya kuchagulia
Kanuni za utumishi wa umma zinamkataza kufanya kazi ya utumishi wa umma katika halmashauri ilipo kata yake. kwa mfano Diwani wa Kibamba anaweza kufanya kazi ya utumishi wa umma Kibaha. Kazi za mashirika binafsi hazina pingamizi.