Diwani anaruhusiwa kuendelea na ajira ya serikali? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diwani anaruhusiwa kuendelea na ajira ya serikali?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MchunguZI, Sep 1, 2012.

 1. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Wataalamu wa siasa na sheria nisaidieani.
  Nina hakina kwamba kuna watu wanaendelea na utumishi wa serikali wakati wao ni madiwani. Wengi wao ni chama tawala. Hii inaruhusiwa?
   
 2. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 6,027
  Trophy Points: 280
  Hairuhusiwi hata chembe! Tunaomba mifano ku-support madai haya mazito.
   
 3. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kwa mujibu wa katiba mtu anapopata majukumu ya kisiasa anatakiwa aache utumishi wa uma mara moja.leta majina
   
 4. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kwani madiwani wanalipwa mshahara? asipofanya kazi hiyo posho isiyozidi laki tano itamtosha? Navyofahamu madiwani wengi wanatokea vijiweni (Jobless) na baadhi yao wana biashara binafsi ambao huendea nazo hata baada ya kuchagulia
   
 5. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kwa ujumla hata ubunge si ajira hivyo unaweza kuendelea na ajira kama ajira hiyo haiathiriki na vikao vya bunge. Mbunge hana tofauti na diwani, kwani wote ni wawakilishi na si watumishi.

  Labda niulize, Je, Shyrose Bhanji ameacha kazi NMB? Jibu lisibadili mwelekeo wa thread lakini kama hajaacha basi nadhani nitaeleweka zaidi.
   
 6. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  mbona madiwani wengi tu wanapiga kazi kama kawaida. mfano ni wale wafanyakazi wa SUA ambao ni madiwani kwenye sehemu mablimbali za manispaa ya Morogoro. Huenda iko hivyo kwa sababu, madiwani tofauti na wabunge, siyo kazi inayohitaji wawepo kazini (kwenye udiwani) muda wote.
   
 7. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Mbunge ni mtumishi ndio maana wanapewa barua za ajira zao na ofisi ya Bunge
   
 8. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Barua hata diwani angeweza kupewa.
   
 9. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #9
  Sep 1, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kama angeweza kupewa. Je wanapewa?
  Wabunge wanalipwa mishahara lakini madiwani hawalipwi. Je ni haki kuwalinganisha.
   
 10. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #10
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hivi kinachomuweka mtu katika kundi fulani ni concept au treatment. Kwa sababu kitendo cha mbunge kupewa barua ni treatment. Kitendo cha diwani kutopewa barua nacho ni treatment.

  Concept ni kwamba wote ni representatives kama alivyo Shyrose Bhanji.
   
 11. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #11
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 6,027
  Trophy Points: 280
  Huu mfano wa Shyrose Bhanji unaweza usiwe relevant sana. Hoja hapa ni uwakilishi wa umma vs utumishi wa umma. Kwanza naomba kujua, Mbunge wa Afrika Mashariki anawakilisha jimbo gani? Tanzania labda. Pili, hivi NMB ni taasisi ya umma?
   
 12. M

  Maseto JF-Expert Member

  #12
  Sep 1, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 721
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Diwani anaruhusiwa kuendelea na kazi ya umma kama si mwajiriwa wa halmashauri ambayo yeye ni mjumbe.mbunge ni mtumishi wa kitaifa,kwa hiyo haruhusiwi kuendelea na utumishi wa umma.
   
 13. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #13
  Sep 1, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Wote ni wawakilishi wa wananchi lakini mmoja analipwa mshahara na mwinginehalipwi. Kwahiyo huyu asiyelipwa mshahara analazimika kutafuta kazi ili kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao.
  Mbunge wa JMT pamoja na kuwa ni muwakilishi wa wananchi lakini pia ni mtumishi (mwajiriwa) wa umma.
   
 14. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #14
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mwita,

  Naona unababaika au unababaisha bila kujua mantiki iliyopo. Ukweli ni kwamba wote ni wawakilishi. Full stop.

  Nilitegemea kama unatumia akili yako vizuri kufikiri basi ungejiuliza kwa nini huyu alipwe mshahara na kwa nini mwenzake asilipwe wakati wote wanafanya jambo lilelile yaani uwakilishi.

  Ukisema mbunge ni mtumishi na diwani si mtumishi basi inaelekea hujui ni nini maana ya utumishi wa umma. Mbunge anawakilisha binadamu wenzake. Diwani anawakilisha binadamu wenzake. Umma ni kundi la binadamu kuanzia wawili na zaidi. Kama kuwakilisha kwa mbunge kunaitwa kutumikia umma kana kwamba kuwakilisha kwa diwani ni kuwakilisha tumbili au ngedere basi ningesema kuna tofauti.

  Lakini wote wanawakilisha binadamu katika maeneo yao. Wote wanaenda kuwakilisha vikaoni ambavyo hufanyika kwa muda fulani tu wa mwaka. Wote hawana likizo. Wote hawana maternity leave kwa wanawake. Sasa utasemaje lugha kama uliyosema hapo juu. Na zaidi unashindwa kujibu kuhusu Shyrose Bhanji.
   
 15. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #15
  Sep 1, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kanuni za utumishi wa umma zinamkataza kufanya kazi ya utumishi wa umma katika halmashauri ilipo kata yake. kwa mfano Diwani wa Kibamba anaweza kufanya kazi ya utumishi wa umma Kibaha. Kazi za mashirika binafsi hazina pingamizi.
   
 16. j

  juu kwa juu JF-Expert Member

  #16
  Sep 1, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Diwani ataendelea n utumishi wa umma, lakini si katika halimashaurinnayofania kazi. Mfano Yule wa cdm kule mwnz ni mwalim lakini diwani. Yule anayegombana n wenje.,, udiwani si ajira. Kwa heri
   
 17. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #17
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mzee wa Juu kwa Juu,

  Unabwaga bonge la point halafu unakimbia. Kaa humu humu usaidie kujibu. Ndiyo maana mimi nimeng'ang'ana na kuwauliza kuhusu Shyrose Bhanji ambaye ni muwakilishi kwenye Bunge la Afrika Mashariki.

  Kama ulivyosema uwakilishi si ajira. Uwakilishi ni kutuwakilisha kwenye vikao amvayo hatuwezi kwenda nchi nzima au kata nzima au kijiji kizima. Vikao vikiisha wewe muwakilishi kama ni mbunge njoo utuambie majibu uliyopewa tulipokutuma utuwakilishe. Basi.

  Uwakilishi si ajira, iwe ni udiwani, ubunge, au hata uwakilishi wa mkutano wa kijiji, mkutano wa mtaa, mkutano wa chama cha siasa.
   
 18. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #18
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Kwa maelezo haya yote bado ni tatizo. Je kuna anayeweza kuleta maandiko yanayoelekeza nini kinatakiwa kufanyika?

  Kwa ubunge, ukisha teuliwa tu na chama chako, unatakiwa kuacha kazi ya ajira serikalini. Diwani sifahamu. Isije kuwa sheria pia inambana ila watu wanafumba macho kwa kujua ni chama tawala maana siamini kama kuna diwani toka upinzani anayeendelea na utumishi serikalini.

  Pale SUA umekuwa ni mchezo wa kudumu. Meya wa jiji kwa kipindi kilichopita alikuwa akiendelea na utumishi wake SUA kwa miaka 5 aliyokuwa Diwani na meya, ingawa naambiwa hakufundisha kabisa pamoja na kwamba alikuwa akilipwa mshahara.

  Sasa hivi kuna watu watatu pale ni madiwani na bado wanalipwa mishahara ya chuo.

  Hebu tupate hizo sheria za utumishi wa umma zinasemaje, labda tutawadai mishahara yetu.

   
 19. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #19
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,621
  Likes Received: 2,042
  Trophy Points: 280
  Mleta uzi ameulizia kwa wale waliokuwa watumishi wa serikali wakaingia katika siasa je wanaruhusiwa kurudi tena katika ajira zao? ndio akaomba mwongozo kwa wanaJF kama wanaelewa kuhisiana na hili hajagusa wale ambao walio katika shughuli binafsi kama biashara na hao jobless (nadhani hawa waliomchagua watakuwa ni wavivu wa kutupwa hivyo wakachagua mtu ambae hawezi himiza maendeleo ikiwepo issue ya kuchangia)
   
 20. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #20
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,621
  Likes Received: 2,042
  Trophy Points: 280
  Yes nime-observe hii kitu somewhere nadhani lengo ni kuepuka bias in case kama atafanya kazi katika halmashauri hiyo hiyo
   
Loading...