Mbugi
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,488
- 257
Mzee wa Juu kwa Juu,
Unabwaga bonge la point halafu unakimbia. Kaa humu humu usaidie kujibu. Ndiyo maana mimi nimeng'ang'ana na kuwauliza kuhusu Shyrose Bhanji ambaye ni muwakilishi kwenye Bunge la Afrika Mashariki.
Kama ulivyosema uwakilishi si ajira. Uwakilishi ni kutuwakilisha kwenye vikao amvayo hatuwezi kwenda nchi nzima au kata nzima au kijiji kizima. Vikao vikiisha wewe muwakilishi kama ni mbunge njoo utuambie majibu uliyopewa tulipokutuma utuwakilishe. Basi.
Uwakilishi si ajira, iwe ni udiwani, ubunge, au hata uwakilishi wa mkutano wa kijiji, mkutano wa mtaa, mkutano wa chama cha siasa.
Ninakubaliana na dhana ya kuwa wote wawili yaani diwani na mbunge ni wawakilishi wa umma lakini si watumishi wa umma kwa maana ya sheria ya utumishi wa umma ya mwaka 2002 na kanuni zake za 2003 na pia ninakubaliana kuwa Udiwani si ajira kwa kuzingatia ibara YA 24 Inayotamka juu ya haki ya mtu kulipwa kutokana na kazi anayofanya, kwa maana ya kulipwa stahili inayofanana na kazi kinyume chake diwani pia sheria ama kanuni na maadili ya diwani yanabainisha kuwa diwani ni mtu anayechaguliwa na wananchi ktk eneo lake kwa namna tu ya umaarufu wake na kwa imani kuwa ana uwezo fulani.