Diwani amcharukia Magufuli: Hakuna Mwananchi atakayefyeka bangi kwenye kata yangu

Akimpinga diwani kwa hoja na vifungu vya sheria bila blah blah na mahaba yake kwa rais nitag mkuu
 
Kwa kuwa una_element za kikabila je wewe ni kabila gan??

Pia wewe unaamini mzazi ndo hutenda mema tu (hakosei) kuliko mtoto/watoto wake??
 
JPM nae amezidi kukurupuka na kujitamkia lolote. PhD holders hawabehave namna hiyo.
 
Nilichoelewa mimi ni kwamba kuna mijitu humu jf inawaigi seat tu, comments zao hazina mashiko....kijiji kina watoto,wazee, wanawake wajawazito , vilema na wachungaji so unaposema wote wakamatwe inamanisha hajaangalia mazingira ya watu hawa. Diwani yupo sawa na mheshimiwa kateleza angei elaborate kauli yake ili raia waielewe vizuri
 
Angeagiza serikali ya kijiji kuchukua wajibu huo wakisaidiana na vyombo vya ulinzi .na maana angetoa agizo kukumbushia jukumu hilo kutekelezwa na serikali za vijiji .na sio kuagiza Polisi kuamrisha serikali ya kijiji .kisheria serikali ya kijiji ina mamlaka kamili.ndio maana polisi wakitaka kukagua nyumba ya mwanakijiji au kata lazima awepo mwakilishi wa serikali kijiji au kata
 
Amezungumza mambo ya msingi sana kiasi kwamba ameonesha ni kiasi gani phd zingine ni za hovyo. Unamkamata mtu na kumpa adhabu kwa kosa la mtu mwingine kivipi? Na gongo ikikamatwa watawalazimisha wanakijiji wote wainywe? Hiyo mihadarati mingine kama cokein na heroin wanapoikamata kwanini wasikamate na wananchi wote kwenda kuiteketeza badala yake wanabeba na kuipeleka kusikojulikana
 
Hujitambui rais ni taasisi hakuna ruksa kuvunja sheria kisa rais. Ataambiwa tu. Huyo si john magufuri wa chato au akiwa rais anakuwa mungu acheni ujuha
 
Mkuu kwa ushahidi,Mkuu amekuwa akitoa maagizo yanayokinzana na sheria na yakatekelezwa,mfano.mahakama ilitoa zuio la watu wa kimara kuvunjiwa nyumba zao zikavunjwa!!
Aliagiza machinga wauze barabarani pasipo kubugudhiwa,japo kuna sheria zinazoongoza mambo hayo,mwisho wa siku machinga wakajaa mpaka ikawa kero!(rejea Mwanza,Morogoro na kariakoo)
Na hii unaitetea kwamba ni jambo la kisiasa haliwezi kutekelezeka,tusubiri!!!
 
Hahahaha absolutely
 
Akili za CCM ni za kupengea kamasi tu,hivi umeelewa hoja ya diwani?
Hata hivyo CHADEMA mmelalamikiwa muda mrefu hadi yakatolewa maoni mmpimwe maana mnatumia. Rais ana maana nzuri. Haiwezekani mtu alime bangi wananchi au wakazi wa eneo husika wasichujue. Kumbuka huyo mkulima wa Bangi ana majirani, Mwenyekiti wa Kitongoji na Mwenyekiti wa kijiji. Ifikie hatua tusitete maovu. Kila mwanamchi awe Mlinzi wa mwenzake. Pia unakushauri usifikiri kama taahira.
 
kama wamemtuma ataenda kuwasimulia vzr wenzake ...tamko la rais ni sheria haiwezekani watu walime bangi halafu jirani zake msijue ile ni bangi ya nani ndicho alichomaanisha mh rais vinginevyo mkimlinda mtuhumiwa ndipo hapo mkaifyeke hiyo bangi
Kwa sheria mmea hauwezi kuthibitika kuwa ni bangi mpaka athibitishe mkemia
 
Wapenda umaarufu kwenye utawala huu wataumia sana eti diwani na yeye anasema "mark my words" kupinga amri ya magufuri atapoteza kila kitu

Someni alama za nyakati umaarufu wa kisiasa kwenye huu utawala utawapoteza sasa jiandae kuulizwa uraia
Uelewa wenu ni mdogo sana kama huyo rais wenu, diwani kapinga kwa vifungi vya sheria vilivyo chini ya sheria mama ya nchi (Katiba) ambayo rais aliapa kuilinda na kuitetea kwa nguvu zote, sasa ninyi badala ya kuja na vifungu vya sheria kumpinga Mh diwani mnakuja na mihemko na mahaba yenu kwa rais....hovyo sana ninyi mbumbumbu
 
Inaonyesha dogo ni very smart upstairs...
Hofu yangu ni reaction ya mpokeaji wa huu ujumbe.
 
Mimi sipingi lakini approach aliyotumia sio sahihi na itamugharimu
 
Wapenda umaarufu kwenye utawala huu wataumia sana eti diwani na yeye anasema "mark my words" kupinga amri ya magufuri atapoteza kila kitu

Someni alama za nyakati umaarufu wa kisiasa kwenye huu utawala utawapoteza sasa jiandae kuulizwa uraia
Huwezi kuacha dhuluma itawala kwa kisingio cha kusoma alama za nyakati huo utakuwa uzuzu
 
Kwani cocaine huwa mnawapa mliowakamata nayo waiteketeze!? Maagizo ya kiendewazimu hayo.
 
Yeye ana backing ya sheria na ameziquote sheria hizo.
Agizo la JPM lina backing ya sheria?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…