Diwani aliyechomwa Kisu afariki dunia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diwani aliyechomwa Kisu afariki dunia

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Jan 3, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Diwani wa Chama cha Kata ya Mtibwa, wilayani Mvomero, mkoa wa Morogoro Chadema, Tusekile Mwakyoma(28), amefariki dunia, baada ya kuchomwa kwa kisu na mchumba wake.
  Diwani huyo alifariki jana majira ya saa 6:00 mchana katika Hospitali ya misheni ya Bwagala alikokuwa amelazwa, baada ya kuchomwa na kisu na mchumba wake kwa kile kinachoelezwa kuwa wivu wa mapenzi.

  Marehemu Tusikile anadaiwa kuchomwa na kisu Desemba 26, mwaka jana katika ziwa la kushoto na mchumba wake ambaye ni Mkurugenzi wa Mafunzo na Uenezi wa Chama cha Chadema katika wilaya ya Mvomero, Songa Mgweno.

  Mtuhumiwa ambaye ni mkazi wa kijiji cha Kilimanjaro, inadaiwa kuwa baada ya kufanya kitendo hicho alitoweka.
  Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCI) Mkoa wa Morogoro, Hamis Selemani,alithibitisha kutokea kwa kifo cha diwani huyo na kueleza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa huyo ili afikishwe mahakamani.

  Kwa mujibu wa ofisa huyo, kabla ya kufikwa na mauti hayo, marehemu alieleza kuwa siku ya tukio, mchumba wake Mgweno alimpigia simu saa mbili usiku aende nyumbani kwake katika kijiji cha Kilimanjaro ili akachukue fedha alizokuwa akimdai Shilingi 200,000.


  Akisema kuwa marehemu likwenda huko na kuamua kulala na ilipofika alfajiri alimuamsha na kumuuliza amefanya juhudi gani kuhakikisha wazazi wake wanakubali amuoe ambapo marehemu alimwambia kuwa hana jibu.


  “Tuliendelea kulala lakini baada ya muda aliendelea kunipapasa nikasikia maumivu makali chini ya ziwa la kushoto baada ya kujichunguza nikaona kisu kikininginia,“ alisema marehemu wakati alipokuwa amelazwa.


  Marehemu alieleza kuwa Mgweno aliendelea kumkaba koo na kuchomoa kisu hicho na kutaka kumpiga kingine, lakini alijitahidi kumdhibiti huku akipiga kelele kuomba msaada ambapo ndugu wa mwanaume waliamka na kwenda chumbani kwao kutoa msaada.


  Alieleza kuwa ndugu wa Mgweno waliamua kumchukua na kumpeleka marehemu katika hospitali ya misheni ya Bwagala ambapo alipatiwa matibabu, lakini hali yake iliendelea kuwa mbaya mpaka alipofariki dunia.


  Akizungumza kwa simu na gazeti hili, Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Jonas Zeland, alithibitisha kifo cha diwani huyo na kueleza kuwa alipata taarifa hizo kupitia kwa wazazi wa marehemu.


  Zeland alisema kuwa anawasiliana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Sara Linoma, kwa ajili ya kusafirisha mwili wa marehemu leo kuelekea mkoani Mbeya kwa ajili ya mazishi.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Mapenzi yanarun dunia...feel free to love.. RIP diwani "unachokipenda ndo kitakachokuua"
   
 3. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana!
   
 4. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nimepotea jukwaa ama!!
   
Loading...