“Divorce is more Painful than Death

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,139
Unaweza ukapaka lipstick ya nguvu na bado kinywa kikatoa maneno yasiyo ya baraka! Usitumie neno talaka
Naomba jiulize kidogo hivi ni mara ngapi kunapotokea mgogoro katika ndoa yako umekuwa unawaza au kutishia kwamba utaachana (talaka) na huyo mume wako au mke wako?

Inawezekana unaishi katika wakati mgumu sana katika ndoa yako umeumizwa sana, umekatishwa tamaa sana, hupendwi, hakujali tena, umejawa na stress kiasi kwamba hata unapotamka kwamba afadhari kupata talaka na kujianzia maisha mapya kivyako huoni uzito wa neno talaka unavyolitamka.
Ukweli ni kwamba kwa maneno yetu tunayotamka tunaweza kuweka mustakabali wa maisha yetu ya baadae.
Maneno hushibisha nafsi sawa na chakula
(Mithali 18:20)

Maneno tunayoongea yana uwezo wa ajabu ndani yake; yana uwezo kuponya au kuua au kuumiza, yana uwezo wa kutia moyo au kukatisha tamaa kabisa, yana uwezo wa kusema ukweli au kudanganya kwa uwongo wa ajabu, yanauwezo kutoa sifa au kulaumu, yana uwezo wa kubariki au kulaani nk.

Neno talaka ni neno lenye sumu na neno baya sana kulitumia katika ndoa yako na zaidi ya yote huweza kuumba kwenye akili na mawazo yako zaidi ya wewe unavyofikiria na kutoa matokeo sawa na mbegu iliyopandwa.

Unapotamka maneno mabaya kwa ndoa yako au katika maisha yako ya kila siku unamwaga sumu na ipo siku itakuwa kweli kwani kila unachopanda lazima utavuna.

Kawaida maneno tunayoongea kwenye ndoa wetu ni kama kioo kwa mwingine (mwanandoa mwenzako).
Ukisema nakupenda, mwenzako anajisikia vizuri na kujihisi kweli anapendwa;
Ukisema umependeza, atajisikia vizuri na kujiona amependeza;
Ukisema ndoa chungu, na mwenzako atajisikia ndoa chungu,
Ukisema nitakufa ni kweli utakufa kabla ya muda wako.

Hivyo ni vizuri kila mmoja kuongea maneno yanayojenga ambayo ni positive ili ndoa zetu zidumu.
Ukizoea kutamka neno talaka ni kweli usishangae siku ndoa inaishia kule unaitamkia hata kama ulikuwa unatania.
Ndoa haitaniwi!
Neno talaka inabidi lifutwe kwenye misamiati yako hasa baada ya kuoa au kuolewa

Duniani tuna watu wa aina tatu tu:
Kwanza wale wanafikiri chakuongea kabla ya kuongea
Pili wale wanafikiri cha kuongea huku wanaongea
Tatu wale wanaongea kwanza ndo wanafikiria nini wameongea

Wewe upo kundi gani na unatumia vipi uwezo wako wa maneno?
Unajua wewe.................................

“Divorce is more Painful than Death
 
  • Thanks
Reactions: EWM
Back
Top Bottom