Anaruhusiwa kufanyakaz kama Mhandisi, lakini chini ya prof engineer hasa inapokuja jambo linalohitaji maamuz, kisheria graduate engineer haruhusiw kufanya maamuz, hasa ukizingatia bado serikali haijakuamini na kupewa mihuri na leseni(Practising Licence). Kwa hiyo watu nawashangaa kwa ushabiki wa kitoto eti chuo fulani ni bora na kwa mfano mtu unaposema chuo fulani kinatoa short term na kingine long term engineers au sijui wengine engineer bora kwa kupitia diploma mara form6 ukijumlisha na miaka4 pale CoET ndo ubora. Hayo yote hayana msingi wowote.ERB hupima Wahandisi wake na kuwapa leseni na mihuri kwa kuangalia muda aliokaa kwenye field, miradi aliyoshiriki na ushahidi wa wahandisi waliomsimamia. Mara nyingi wahandisi washauri(consulting Engineers) lazima wathibitishe kwa kugonga mihuri yao. Ikumbukwe moja ya watu ambao wako strict ni Consulting Engineers, kamwe huwezi kuandika ripoti ya uongo ukadanganya kwa mfano ulishiriki ujenzi wa mliman city na BICO, Millenium towers mpya chini ya UNDI Consult, au mradi wa NORPLAN, COWI,NIMETA Consult au TanConsult,InterConsult na nyingine wakati hukushiriki, never huwezi kugongewa. Ni kwa umakini huu wa consulting firms ERB kamwe hawawezi kukusajili kama hujafanya kazi na hawa wahandisi washauri. Hakuna narudia hakuna chuo chochote ambacho kinatoa mhandisi bora eti kwa zile lecture notes na madesa, lazima uje mtaani upikwe upya. Kwa kumalizia, Engineer ni trainable person ambae anakua fit akipigwa msasa, ila huwezi leo kumaliza chuo fulani halafu ukapewa mradi udesign retaining wall, daraja au ghorofa 20 ikiwa na basementl,kamwe hutaweza,ila ukikaa kwenye game ukapikwa utaweza tu bila kujali umetoka chuo gani, na ndo maana ERB wanatoa practising Licence na siyo theoretical licence kama mdau mmoja aliposema UDSM ni bora theoretically than DIT. Engineering hasa ni Practical aporoach ili kitu kitokee kwa maana ni uumbaji ambao ni tofauti na ule wa Mungu muweza ambae yeye alitamka tu KUWA na kitu kikatokea. Engineering lazima ufanye ili kitu kitokee na siyo siasa.