Kinachotokea kwa Disasta na Rapcha, ni marudio ya Eminem na MGK.
MGK alionywa mapema kabisa. 50 cents akamwambia "nice song, but you're messing with the wrong guy". Ndicho kilichotokea. Eminem hakujali beats zenye mvuto, wala flow ya kuremba, he just destroyed MGK Lyrically!
Naona pia ndicho alichokifanya Disasta kwenye best friend. Yeye amejikita kwenye mashairi na content, habari ya beats na flow kamuachia dogo ahangaike nazo mwenyewe.
Sidhani kama Disasta atajibu hii diss ya pili. Sioni kama ni battle ya level yake. Itakua kama Tyson Furry kuvimbiana na Mandonga, it's a waste of time!
Fair battle kwa Disasta ni atakapopambana na na MC's design ya One the incredible au P Mawenge. Hapo lolote laweza kumkuta. Rapcha ni level za akina Lunya na Motra.
Simshauri Disasta kujibu tena diss za huyo dogo!