Diss Tracks: 5 Kali kuliko zote.

Diss Tracks: 5 Kali kuliko zote.

The August

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2018
Posts
1,079
Reaction score
2,027
Katika muziki wa Hip Hop, Beef huwa haipukiki.. Kutoka na utamaduni wa majigambo juu ya maisha mazuri, gari nzuri, dem mkali, hela za kutosha bank basi conflicts huibukia hapo..

Tunakumbuka 2pac v BIG, Jay Z v Nas, Nelly v KRS One, Lil Kim v Fox Brown, na way back pia Ice Cube dhidi ya Clique yake ya Zamani N.W.A.

Beefs hizi zilizalisha nyimbo kali ambazo zilikua ni beef tracks..

Chini hapa ni beef track 10 kali kwangu, unaweza kosoa na kueleza zako pia..


1. ETHER Ya Nas

Nas ni fav rapper wangu.. Ana mashairi mazito.... Ni mwanafalsafa sana. Nyimbo ya I Can ni Elimu ya dunia... Hakuna aliyepinga hilo... Baada ya Big kufa, swali lilikuwa ni nani ni Mfalme wa New York... Ni Jay Z ama Nas? Mwaka 2001 Nas alitoa nyimbo hii ambayo ililenga kujibu Takeover ya Jay Z. Kwanini hii ni districk bora kabisa kwangu.. Moja, upande wa Jay Z ulikiri kuwa hii nyimbo iliwasumbua sana.. Memphis Bleek, crew ya jay z alikiri hili... Pili ilikuwa direct.... Aliibua tuhuma za Ushoga za Jay Z, Ukandamizaji wa rappers wengine wa Jay Z, Ubunifu mdogo wa Jay Z kimuziki kwa kuchukua kazi za watu wengine..



2. NO VASELINE ya Ice Cube

Miaka ya 1980 mwishoni, Niggers with attitude, clique iliyokuwa ikitokea Compton Calfonia, ilikua katika zama za mwisho wa uhai wake.. ice Cube alizinguana na kina Eazy E, Dr Dre katika masuala mbalimbali. Hela kama ilivyo chanzo cha makundi mengi kuvunjika, ilikua sababu, NWA walimuita jamaa msaliti kiasi cha kimfananisha na Askari msaliti wa kikosi cha Marekani katika Civil war, Benedict Anorld aliyejiunga na kambi ya Uingereza.

Alipojitoa, Alitoa kombora hili.. Kwanini ni best dist track kwangu... Kwanza jina... No Vaseline (nadhani nimeeleweka), Pili ilijibu tuhuma nyingi zake, pia iliwachana sana NWA kwa issues kama za kumsupport G. Bush ambaye hakuwa akipendwa na Blacks..




3. HIT EM UP Ya 2 Pac

2pac na Big walikuwa ni washkaji sana kabla ya kuja kutibuana na kuwa mahasimu wakubwa sana. Beef yao inaelezwa kuchangiwa na mambo mengi, biashara ya muziki ikiwa ni jambo kubwa zaidi.. Katika track hii Makaveli amemchana sana Big kiasi cha kuweka hadharani kuwa alimla mke wa Big mwanamama Faith Evans..



4. 300 Bar and Running ya The Game.

Kutoka Compton huyu ni rapper bora miaka ya 2000 hadi 2010.. Alipewa shavu na Dr Dre na kuunganishwa G Unit ya 50. By character ikawafanya watu hawa kuwa haaelewani kabisa... Nadhani ndio beef iliyodumu muda mrefu kuliko zote katika Ulimwengu wa Hip Hop.. Kwa ujumla jamaa wemetoa distrack kati yao zaidi 50.. Kali kuliko zote ni hii ya The Game..



5. SHETHER Ya Remmy Ma.

Hii ni latest distrack ya rapper Remmy Ma mwenye 'line' ya Terror squad yake Fat Joe... Amechukua jina la Ether ya Nas ambaye pia ameshiriki kuiandika hii nyimbo... Ni distrack kwa Nicki Minaj




Hizi beefs jamaa zinawalipa sana kwa mauzo ya nyimbo kupush album pamoja na concerts...







Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sijaiona kama hit em up,naamini ndio diss track Kali ya hip-hop duniani

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna diss track kama Hit em up" ...Miaka nenda rudi

Sent using Jamii Forums mobile app
Hadi adui akikiri, basi ujue 'bomu' limelenga katikati ya kambi!
Screenshot_20190224-221309.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Motherfucking Real GS...ya Eazy E, hii nidistrack Kwa Dr.Dre
 
Back
Top Bottom