Disemba 9 kila mwaka: Tunasherehekea uhuru wa nchi ipi?

-kwa nini nisherehekee miaka 50 ya nchi ambayo haipo? Hii inamaanusha kuwa upstairs hakupo sawa tunabebwa bebwa tu.
-nchi inarudi nyuma badala ya kwenda mbele,Mungu alitupa rasilimali zote..hii ni nchi ya asali na maziwa ..kwa nini wananchi wake wote wana suffer?(except wakubwa na ndugu zao)
-miaka 50 tumeshindwa kujipanga kuanzia umeme wa uhakika barabara na maji safi na salama.wazungu wameshatengeneza technology zote ..wamefikiria kila kitu na kuumiza vichwa vyao sisi kazi yetu ni ku import kile kitu ambacho kipo ready for use ..lakini hadi hili tumeshinda.
-ajira nyingi wanapewa wageni eti wazawa ni wezi wanaiba(jk alishasema hili kama hamjui) tatizo ni nini? Kama ni elimu duni nani anahusika kuimarisha hio elimu ili tutoe changamoto kwenye ajira mabli mbali chini?
Sioni mantiki ya kushangilia uhuru hewa..wala sitaki kusikia au kuona hio sherehe yenu..mmenikera kweli leo na mafataki yenu .
Hakuna mantiki ya kusherehekea uhuru hewa:
kwa mtindo huu huwezi kuiona mkuu .....cha msingi ponda mali kufa kwaja meeeeeeeeeeeen
pesa makaratasi hasara roho babuuuuuuuuuu
 
Tanganyika sio huru bado ni koloni la Zanzibar, kuna kazi kubwa ya kuipatia Tanganyika kutoka katika ukoloni wa pili baada ya ule wa Muingereza!!
 
Ninavyo jua Tanzania tangu izaliwe haijatiza miaka 50 haya ni madhamisho ya Tanganyika kwa mlango wa nyuma 2014 tutakuwa na maadhimisho ya Tanzania mkuu
 
My take:
Muungano ni muungano jina tu.haupo wala haujawahi kuwepo
Uhuru unaosherehekewa ni wa Tanganyika, nchi ambayo kwa sababu ambazo hazieleweki vema, takriban miaka miwili baada ya uhuru wake ilibadilishwa jina na kuitwa Tanzania
 
Ni ubakaji wa kihistoria kutangaza ati twasherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania,hakuna kitu cha namna hiyo,Tanzania haijafikisha miaka 50 wala hakuna nchi Inaitwa Tanzania ilipata duniani,Bali Tanganyika ndio iliyopata Uhuru na Zanzibar ndio iliyopata uhuru Kisha Zikaungana zikazaa dude Tanzania,so kama tunataka kusherehekea Muungano inatakiwa tuseme kuadhimisha sherehe za Muungano wa Tanzania nakama tunakata kusherehekea uhuru inatakiwa tuseme sherehe za kuadhimisha Uhuru wa Tanaganyika,coz Tanganyika ndio iliyopata Uhuru na sio Tanzania.Tanzania wakati tunapata Uhuru haikuwepo duniani hata mimba yake haikuwepo.

Kwanini tuendelee kuibaka historia na kusema ati tunasherehekea 50 years of Tanzanian independence?!,eeeeeeeee,nyerere kaondoka bilka kujibu swali hili lakini kwani wanaoshikilia mikoba yake wamekufa?kwanini wasijibu na kurekebisha tizo hili.?
 
Uwongo na Unafiki ni mambo mabaya sana ambayo hata vitabu vya Mwenyezi Mungu vinakataza! Msema kweli siku zote ndiye mpenzi wa Mungu.
SASA MIMI NINA SWALI LINANITATIZA! JE TAREHE 12 DESEMBA NI SIKU YA UHURU WA TANZANIA BARA AU UHURU WA TANGANYIKA?
 
Tunaona mambo mapya yanatendeka kimyakimya, Serikali kwanini haiwalezi wananchi kuhusu mabadiliko haya ya jina la sherehe za uhuru wa TANGANYIKA na badala yake imekua TANZANIA.
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    31.9 KB · Views: 159
Kaka hawataki kuelewa watanganyika mana kitu si kitu wanasema tanzania mana hawajui kutofautisha kati ya tanganyika na tanzania...ila nahisi ukiwaita watanganyika kma wanatukanwa ndio mana wanaita tanzania ila ipo siku watalikubali neno tanganyika
 
Hayo ni Majina ambayo hayana chochote bali ni busara kwa vizazi kusimamia vile mabvyo wamerithishan kwa wema.Mwalimu anasema alituma watu wamtafutie jina Tanganyika lilitoka wapi lakini mpaka anaondoka sikupata kumsikia kusema alipata maana ya Tanganyika na hao waliobuni jina la Tanganyika.

Hivyo kwa sie tuliozaliwa miaka ya 70s na kushuka chini mpaka 2012 hatujui hicho mnachokiita Tanganyika.Tumejifunza na kuona Tanganyika kwenye makaratasi kama historia.Mimi ni mfano halisi wa Mtanzania, Baba yangu kazaliwa Tanganyika, mama yangu kazaliwa Tanzania hivyo jina Tanganyika kwangu ni historia njema kuwa Taifa langu hapo zamani lilipata kuwa Tanganyika.

Urithi uwa haubadiliki,hivyo ikitokea Wazanzibar wakafikia sehemu wanajitoa kwenye Muungano basi ni kitendo cha wao kuwa wanajitoa na hawatatumia jina Tanzania kama sehumu yao ya ardhi,basi mwisho sie tulioko Tanzania tunaendeleza Tanzania yetu.
 
Nyerere ni mtu mwenye akili sana anapotaka jambo lake lifanikiwe mbona akumuuliza baba yake kwanini aliitwa kambarage nyerere? kwa kuwa akuanzisha yeye au kusimamia neno Tanganyika so halina maana Tanzania kalisimamia yeye so wote tufuate ni ujinga sana,

England ipo pale milele haitofutika pamoja wanayo Great Britain and Northern Iraland hivyo hivyo, New york itabaki pale pamoja na USA ipo, siku USA ikivunjika Yankee anaendelea na New York yao still inatangazika hawatopata shida kuitambulisha duniani same na Zanzibar hawotopata shida kuitambulisha Kivumbi kwa Tanganyika Tunaaanza Moja from 1961............................... Poleni Msioipenda Tanganyikaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Hayo ni Majina ambayo hayana chochote bali ni busara kwa vizazi kusimamia vile mabvyo wamerithishan kwa wema.Mwalimu anasema alituma watu wamtafutie jina Tanganyika lilitoka wapi lakini mpaka anaondoka sikupata kumsikia kusema alipata maana ya Tanganyika na hao waliobuni jina la Tanganyika.

Hivyo kwa sie tuliozaliwa miaka ya 70s na kushuka chini mpaka 2012 hatujui hicho mnachokiita Tanganyika.Tumejifunza na kuona Tanganyika kwenye makaratasi kama historia.Mimi ni mfano halisi wa Mtanzania, Baba yangu kazaliwa Tanganyika, mama yangu kazaliwa Tanzania hivyo jina Tanganyika kwangu ni historia njema kuwa Taifa langu hapo zamani lilipata kuwa Tanganyika.

Urithi uwa haubadiliki,hivyo ikitokea Wazanzibar wakafikia sehemu wanajitoa kwenye Muungano basi ni kitendo cha wao kuwa wanajitoa na hawatatumia jina Tanzania kama sehumu yao ya ardhi,basi mwisho sie tulioko Tanzania tunaendeleza Tanzania yetu.
Nakereka mno na watu WAVIVU WA KUFIRIKI. Hivi jina Tanzania hujui limetokana na nini? Mdosi aliyebuni jina hilo kasema waziwazi chanzo chake sasa wewe unasema Zanzibar ikitoka kwenye muungano bado ubaki na Tanzania? Hata ukimuuliza mtoto wa darasa la kwanza 2 - 1 atakujibu inabaki 1 na sio 2!
 
Nyerere ni mtu mwenye akili sana anapotaka jambo lake lifanikiwe mbona akumuuliza baba yake kwanini aliitwa kambarage nyerere? kwa kuwa akuanzisha yeye au kusimamia neno Tanganyika so halina maana Tanzania kalisimamia yeye so wote tufuate ni ujinga sana,

England ipo pale milele haitofutika pamoja wanayo Great Britain and Northern Iraland hivyo hivyo, New york itabaki pale pamoja na USA ipo, siku USA ikivunjika Yankee anaendelea na New York yao still inatangazika hawatopata shida kuitambulisha duniani same na Zanzibar hawotopata shida kuitambulisha Kivumbi kwa Tanganyika Tunaaanza Moja from 1961............................... Poleni Msioipenda Tanganyikaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Wanaokataa TANGANYIKA hawana tofauti na wanaokataa wazazi wao.
 
Nakereka mno na watu WAVIVU WA KUFIRIKI. Hivi jina Tanzania hujui limetokana na nini? Mdosi aliyebuni jina hilo kasema waziwazi chanzo chake sasa wewe unasema Zanzibar ikitoka kwenye muungano bado ubaki na Tanzania? Hata ukimuuliza mtoto wa darasa la kwanza 2 - 1 atakujibu inabaki 1 na sio 2!
Usisumbuliwe na itikadi ya chuki eti kwakuwa lilibuniwa na mdosi, nembo nyingi sana za Nchi na majina ya vitu muhimu vya zamani na vya sasa vilibuniwa na watu kama wewe!!!

Hata Fedha unayotumia wewe ni ubunifu wa watu usitishwe na hayo msemo maalufu dunia wa Diamonds are forever ulitolewa na mswahili mwenzio mwenyeji wa Tanga!!Walikuwa wanabishana na wakurugenzi wa De-Beers kwenye kikao cha board, wakurugenzi wakijinadi kwa utafiti wao kuwa soon mgodi wa Williamson Diamonds LTD utafungwa kwa kuwa ALMAS zitakuwa zimeisha yeye akawambia jibu moja tu '' Diamond are Forever" toka amewaambia hivyo Mkurugenzi Mkuu wa DE-Beers akaondoka na useme ule kuunadi kwenye shughuri zake matokeo yake leo ni msemo wa dunia.

Jina Tanganyika kwa historia ya google laoenekana Tulipewa na Wajerumani kwa hivyo Jacobus wajerumani ni wazazi wako?.Manako Baba wa TAIFA lako alitoa TENDA kwa Wasanii Artist wa Tanzania wakati huo watafute jina zuri kwa ajili ya kuunda jina Nchi yakaletwa mengi kisha watu wazima wakakaa chini wakafanya uchaguzi ikaonekana linafaa nami kijana wa leo, baba wa leo, babu wa kesho naona sahihi kumrithisha jina la Tanzania mjukuu wangu,jina lililoasisiwa na Watanzania wenyewe kwa ridhaa yao wenyewe na MUNGU alikuwa nyuma yao basi walilibariki na ndio maana tunaishi kwa AMANI.

Unapokuwa kwenye muungano wa kibiashara wakati mwingine unapojitoa binafsi basi walioko kwwenye biashara wanachofanya ni wewe kulipwa chako wauisha share zako na unawaacha wenzio waendelee na maisha ya biashara husika.

Hii si biashara ya tarakimu hii ni realiaty, Watanzania wa digital wengi kayumba wanaoibukia kizazi cha facebook, google, IPad na Galaxy leo uwaletee habari za mwaka Alobaini na saba eti TANGANYIKA!!!! not necessary name but what has it done to be so special to change back to something which we haven't seen or feel it yet!!!!daaaaaaammmmm man its ridiculous, and for we current new generations TANGANYIKA is so dame, and we respect it. We will always appreciate our beloved ancestors who happen to survival under the colonial rule with that name, they played their part now and we are playing our party accordingly to the world we are living currently made everything possible for the coming future generation.

Kama ni Museeeeeeeeeeee ya miaka iyo tafakari Museeeeeee!!! lete hoja why we should bring Tanganyika? ukiachana na historia ya muungano!!!Tunataka benefit zitakazo tushibisha tufike uamuzi wa kuungana na wewe kuitetea Tanganyika jina unalolilia ka Mtoto mchanga!!!
 
Nasikia matangazo leo kila mahala kwamba eti kesho kuna maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania Bara.Nimesoma historia, sikumbuki kama katika ramani ya dunia kuliwahi kuwa nan chi iliyoitwa Tanzania Bara na ambayo ilipata Uhuru tarehe 9 Desemba 1961. Kumbukumbu zinanitanabaisha kuwa ilipata kuwapo nchi kwa jina la Tanganyika katika Afrika ya Mashariki na ambayo ilipata Uhuru wake tarehe 9 Desemba 1961.Ni nchi ambayo Babu yangu mzee Emil Lusambo Sr. alipata kuwa raia wake.

Kesho ni miaka 51 tangu ulipozaliwa mama yetu Tanganyika.Hivi kwa nini watoto wako hawapendi kukutaja Eee mama Tanganyika?? Uliwakosea nini watoto hawa mapaka waoni kinyaa kukukumbuka angalau kwa historia tu??

Wala hatutawasahau wazalendo walioyatoa maisha yao kwa ajili yako Tanganyika...oohh,.walotoa jasho lao, waliomwaga damu yao,.waliojitolea kila namna ya tunu walizojaaliwa na mwenyezi Mungu kuhakikisha mama Tanganyika unasitawi, tutawakumbuka. Waliokatisha mahusiano ya ndoa zao katika kipindi cha ujana wao na kubaki wajane,.

Hakika historia ya kweli yako mama Tanganyika itawakumbuka daima.Ingawa sisi tunaokukumbuka tunaonekana wabinafsi na wanaopenda kujitenga,.hatutaacha kukumbuka. Mimi ninakukumbuka. Mohamed Mikidadi anakukumbuka.George Bosco anakukumbuka.Sophia Shayo anakukumbuka. Athumani Bushiri na wengine wengi wanakukumbuka.Sisi sote tunasikitishwa na upotoshwaji wa Historia unaofanywa na hawa ndugu zetu wa damu.Wanafanya unafiki lakini daima ukweli husimama.

Hakuna taifa linaloweza kuendelea duniani likiwa na msingi katika unafiki.Unafiki ni kielelezo cha woga na kutojiamini.Hatuwezi kujenga amani ya kweli na mshikamano pamoja na maridhiano ya kitaifa juu ya msingi wa Unafiki.Tukijenga juu ya msingi wa unafiki tutavuna woga,kutojiamini na kupungukiwa na uzalendo.Leo hulka ya wanaoitwa waTanzania imekuwa ni woga.Leo dada yangu anatembea barabarani bila kujiamini.Leo kila mtu fisadi kwa kuwa hakuna Uzalendo kwa taifa.

Haya ni matunda machache ya kujenga taifa juu ya msingi wa Unafiki.Muulize Mwanaisha mwanafunzi wa darasa la tatu B shule ya msingi Muungano akuelezee historia ya nchi yake.Utashangaa kusikia mambo ambayo hayaeleweki mwanzo wala wapi yalipo.Historia yetu haieleweki vizuri na wala haifundishwi sawasawa kwa vizazi vyetu.

Wenzetu Marekani kwa mfano wana umri wa zaidi ya miaka 200 lakini nchi ni moja yenye mshikamano na amani ya kweli kwa kuwa walijengajuu ya msingi wa ukweli.Kama leo motto wa darasa la tatu hajui historia yake vizuri itakuwaje kwa vitukuu vyetu miaka 250 ijayo?

Tanganyika Heri wanaokutaja na kukumbuka.Heri wanaokulilia leo.Kwa kuwa ukweli hushinda naamini si muda mrefu utaturudia mama yetu.Tunajivunia wewe kuwa mama yetu.Tunajivunia utajiri wa rasilimali ulizanazo ambazo sisi ni waeithi ee mama yetu.Wanaoona aibu kukutaja wasamehe mama,.ila sisi tutakutaja kwa gharama yoyote.

Mungu akujalia uzima na afya tele katika kipindi hiki kigumu.Ni mapito tu,tunajua kama sio kesho basi keshokutwa utaturudia tena na tutaishi pamoja nawe mama yetu.Tunakupenda mama yetu.

NI UHURU WA NCHI GANI??
 
Ukiwa roho mbaya ndio unakuwa kama hivyo hulitaki hata taifa lako,nyumbani ni nyumbani.

Zanzibar ni taifa, limeungana na taifa hewa ambalo halitajwi sasa ila kulamisha kuwa kuna Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Hatujaoneshwa mkataba wa muungano unasemaje maana lazima humo ndani itajwe Tanganyika huru. Na waliounganisha ni akina nani maana sisi wengine tulizaliwa Tanganyika na 1964 tulikuwa na haki ya kupiga kura lakini halikutokea hilo. Unafiki kuukataa ukweli kwa kukataa uwepo wa Tanganyika. Ni nchi iliyopo ila inafutwa kijanja sijui kwa maslahi ya nani. Yote tisa huu muungano halali wa Tanzania ni wa wachache kulingana na mchakato uliotumika; kumi haya malalamiko na mchakato wa kuupigia kura muungano ili kuupa uhalali wa uwakilishi na uundwaji wa sisi sote mbona unachakachuliwa?
 
Ina maana hata uhuru wa bendera Tanganyika imepoteza sasa ni digital name TANZANIA BARA.
 
Back
Top Bottom