Enzi za zamani nzuri jamani!!! Nakumbuka Moshi technical walikuja kwenye shughukli za ' Red Cross' mh walikuja wamevaa ' Raba Mtoni' na Jeans, jamani enzi zile kupata Jeans mpaka uletewe na ndugu yako kutoka nje ya nchi. Mh Wasichana wa Korogwe viroho juujuu! ( mh kumbe kuja kwenye Red Cross kulikuwa kuna lengo lingine tena) Vijana wakajieleza mpaka walimu wakakubali kuvuka mipaka nje ya Moka wa Tanga. Haooo na mabasi mpaka Moshi na walimu wetu watatu.. Sharti ilikuwa lazima kurudi shule mara baada ya mziki usiku uleule. Mh wanafunzi wamepania muziki mpaka asubuhi, Madereva wa mabasi sijui wamepelekwa wapi nia tu lazima muziki mpaka asubuhi! Walimu wakang'ang'ania mara madereva wakaibuliwa saa 2 baadae muda uliopangwa kuondoka. Hao safari kurudi Korogwe Girls Secondary school.Mhh ile miziki ilikuwa mizuri saaana, those good days!
Ha ha ha,kumbe vituko viliendelea,katikati blues kali,form one wa Mazengo na form four wa Msalato,kumbe form one alimdanganya patna wake kuwa naye ni form four,umeme na mziki ulikatika ghafla,binti toka Msalato akahamaki kwa sauti "Whats the matter?",kwa haraka Mazengo boy akajibu "Matter is anything which occupies space and has got weight"!

Mzukila