mkuu kosa la kwanza kabisa ni kuwa na mahusiano na mwanamke aliyekuzidi miaka minne! hiyo miaka 4 ni mingi mno, walau ingekuwa miwili...
1. madhara yake ndo hayo amekuwa akifanya mahusiano na wanaume ambapo wengi wao itakuwa ndo wa makamu yake na hata kumzidi umri.
2. kutokubalika kea ndugu na rafiki zako kulipelekea yeye kutokuwa na imani ya kuolewa nawe hivyo kulazimika kuwa na mahusiano na wanaume ambao wamemzidi umri ili in case humuoi basi wale awagande mmoja wao angemuoa.
3. kutokana na kukuacha sana kiumri anakuwa anakudharau, ndoa za wazee wetu zilidumu kutokana na mzee kuwa mkubwa hata kwa miaka 10 dhidi ya mkewe, je wewe mdogo wake atakuheshimu vipi.
4. kiukweli ulikosea mkuu, jitoe katika mahusiano hayo, ikiwezekana hama hapo kaa mbali na jitahidi asipajue kwako, hayo mahusino si kitu ndo maana ameweza kuwashtaki police, je ukifungwa jela ina maana kwake si kitu. vitu vingine ni akili yako tu kuamua wala haihitaji kufikiri sana kwa hili, upofu wa mapenzi usiwazidi nguvu amua maamuzi magumu, mwache aondoke