Disappointment in love issues

real thinker

Senior Member
Jun 24, 2012
118
195
Habari wanajukwaa,

Naombeni msaada wa mawazo kutoka kwenu maana nimekuwa mtu ambae sina imani tena na mahusiano ya mapenzi kutokana na wakati mgumu niliopitia, mimi ni kijana mwenye miaka 23 ni mfanya kazi wa serikali pia ni mwanafunzi wa chuo cha taifa cha usafishaji (NIT) nasomea masuala ya logistics and transport management katika ngazi ya degree mikezi kadhaa nyuma nilikuwa na mahusiano na mfanya kazi mwenzangu ambae nimedu mu nae kwa zaidi ya miezi nane lakini katika mahusiano yetu tumeweza kupitia mengi ikiwemo kupishana kauli pamoja na usaliti wa wazi wazi ambapo nimewahi kumfuma lakini nikaweza kusamehe ambapo nilikuwa nikitegemea atabadilika na tukafanya maisha.

Changamoto nyingine ni kwamba kanizidi umri kama miaka minne hivi ingawa sikuona kama ni tatizo kwa upande wangu ingawa ndugu jamaa na rafiki walikuwa wakidai hanifai ni mkubwa kwangu, katika kipindi chote hicho alikuwa ni mtu wa kutofautiana na rafiki zangu pia alikuwa hapendi niwe na mawasiliano na msichana yeyote ambae yeye hamfahamu hata kama anamjua lakini kwa mapenzi yake hampendi alikuwa hataki niwasiliane nae all in all nilivumilia pia simu yangu alitaka mda wote awe nayo ila yake ni yake tu.

Kikubwa kilichonikatisha tamaa ni kwamba juzi kati alienda kulewa alinikuta na wanafunzi wa CBE wawili wasichana na mmoja mvulana tunasoma kozi moja tulikuwa tunafanya discussion maana wanakaa pale nilipopanga mm akaja akaanzisha fujo ikiwemo tupasua chupa za bia kubwa nililolifanya nikufanikiwa kuwaondoa wale wanafunzi eneo lile na kubakia na yule mtu wangu ambapo aliweza kuchukua chupa na kutaka kunichoma nayo ambapo alikuja rafiki yangu na kujaribu kumshika yule msichana ambapo ilipelekea huyo rafiki yangu kuumia mkononi na msichana pia pia cha kushangaza akaenda polisi na kudai kuwa mimi na rafiki yangu tulimvamia na kumpiga ambapo ikapelekea kupelekwa lockup kwa mda mda wa masaa 24 lakini kibaya zaidi wakati narudi nyumbani baada ya kutoka polisi nikamkuta na mwanaume mwingine yupo nae ndani kwake nikajiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu ambapo nikaamua kuacha kama ilivo maana ndo ustaarabu aliochagua.

Kutokana na hali hiyo imenipelekea kukosa imani na wasichana pia mda mwingi kuwa na msongo wa mawazo pale ninapokuwa peke yangu ambayo wakati mwingine yanapelekea kukosa usingizi na kukosa hamu ya kula.

Naombeni mchango wenu ili niweze kuondokana na msongo huu wa mawazo wana jamvi.
 

lup

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
2,297
2,000
Na kwa taarifa yako..hata pale alipowakuta alikuwa katoka kwa mwanaume na huenda ni mme wa mtu na kamgegenda ndio akaja kwako...
 

Mhandisi Mzalendo

JF-Expert Member
Aug 23, 2010
4,285
2,000
Songa mbele acha kulialia...
Kuwa busy na mambo mengine wanawake wapo kibao, we saka hela na concetrate na masomo yako...
Achana na huyo mwanamke amini utaweza na utaweza...
 

Tater

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
4,620
2,000
Baada ya kuona NIT nikaacha kusoma post yako.... Wewe bado mwanafunzi komaa na kitabu, mapenzi hayazeeki wala hayachuji utayakuta mbeleni...
 

Survival

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
219
225
Mkuu unatia hasira kwa huo ujinga,sasa hapo unataka ushauriwe nini?Me nakushauri tafuta G.P.A kwanza hayo mambo mengine baadae
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom