Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 (Tanzania Development Vision 2025)...

hiyo namba sita tamu...ngoja tuone kama yatatekelezwa...
 
Kwa matanuzi yenu ya Serikali yalivyo makubwa yaliyojaa anasa, kwa ukubwa huu wa Wizara na Idara, Kwa ufisadi huu - aisee hiyo ni ndoto ya mchana; wadanganyeni watu wa Iramba!!
 
2025 mbona mbali? Lakni uzembe kazini au kufanya kazi kwa kiundugu undugu hatufiki popote watakao pata maendeleo ni watu wachache na sio taifa zima.
"Miaka 100 ijayo Tanzania itakua nchi iliyoendelea zaid ya zile zilizoendelea".Shemeji akiwahutubia vijana pale 7/7 mwaka huu,sasa unashangaa hapo 2025 si ndo dira ya taifa inavyosema?tujiulize huo mpango wa taifa wa miaka mitano unatekelezwa?wananchi wanaujua?wameupitia?,kwanza zipo doc 2 sijui ipi inatekelezwa
 

Ayaaa shemeji noma anaongelea maendeleo ya kitukuu atakapo kuwa mkubwa. Sasa hapo kila awamu ya uongozi, kiongozi ahakikishe anakuwa tajiri kuliko matajiri wote waliotangulia hadi miaka mia ipite ndo tulifikilie taifa.
 

why mambo yote ya ahadi as if na yeye ni chama pinzani akiomba kura?
Atahakikisha lini and not now?
Apiga kampeni ya uchaguz sahivi nini!
 
why mambo yote ya ahadi as if na yeye ni chama pinzani akiomba kura?
Atahakikisha lini and not now?
Apiga kampeni ya uchaguz sahivi nini!

Tumechoka na maneno tumewapa kura miaka 50 bado ndio tunaendea nyuma kutoka na jinsi rasilimali zinavyovunwa sasa hivi
 
Ayaaa shemeji noma anaongelea maendeleo ya kitukuu atakapo kuwa mkubwa. Sasa hapo kila awamu ya uongozi, kiongozi ahakikishe anakuwa tajiri kuliko matajiri wote waliotangulia hadi miaka mia ipite ndo tulifikilie taifa.
Kwanza wanaoutaka uongoz hasa urais wanapaswa kuhakikisha kwamba wanaitekeleza hii mipango ya maendeleo,nna shaka kuna docs zitatupwa,mfano BRN kuna watu wakija wanakuja na zao,ila kulikua na MTWARA CORRIDOR leo haitajw tena,watu wamekuja na SAGCOT si mbaya ila where is MTWARA CORRIDOR?.Utajiri ni kweli,watawala wetu wanaingia maskin ila wanatoka matajiri sana,hili wala halifichiki,iko wapi sheria ya kutenganisha biashara na siasa?hata wapinzani hawaiulizii kwakua nao ni wafanya biashara
 

Nchi hii inasheria lakni inaongozwa kisiasa siasa, mfano fundi ujenzi umpe tenda ya kukujengea nyumba vifaa vyote umpe halafu mwisho wa siku fundi auze simenti yote, na wewe umwambie fundi nimekusamehe endelea na ujenzi unadhani atajenga vipi bila simenti.

"Tumewasamehe misamaha ya kodi" kesho utasikia taifa linadaiwa mabilioni, sasa mnataka azilipe nani?.
 




Kwanza huyo mjinga kwani habari ya babayake ya maisha bora kila mtanzania yameishia wapi?
 
Hii nchi ina utajir gan mpaka ianze kuwasamehe matajiri kulipa kodi?
 
Kwanza huyo mjinga kwani habari ya babayake ya maisha bora kila mtanzania yameishia wapi?
"Tuliposema Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania,hatukumaanisha Kuwajaza mapesa mfukoni,bali kuwajengea miradi ya kimaendeleo kama vile barabara,umeme,maji ili vikuwezeshe kujiletea maendeleo".SHEMEJI Mbinga ALIPOKUA AKIZINDUA BARABARA YA LAMI YA MBINGA-SONGEA.
Baada ya takriban miaka 9 ndo anaifafanua kauli mbiu yake,pole kwa waliokua wakitafsiri tofaut,hao ndo wanasiasa
 
Last edited by a moderator:
Kwanza huyo mjinga kwani habari ya babayake ya maisha bora kila mtanzania yameishia wapi?


Maisha bora kwa kila mtanzania huku mtaani mahitaji mhimu yamepanda bei sababu ya kodi, hospitalini dawa hakuna, harafu bei ya mazao ya biashara yameshuka bei. aseme maisha bora kwa kila alienacho.

Kilimo kwanza huku unamnyonya mkulima kwa kushusha bei ya mazao na kupandisha bei ya bidhaa unategemea maisha bora yatatoka wapi? Tushukuru kuwepo nguo za mitumba la sivyo wa kutembea uchi tungekuwa wengi na ukilinganisha bei ya pamba mwaka huu ilikuwa kati ya 800 hadi 1000.
 

Barabara, maji, umeme na vinginevyo ni kodi za wananchi sio hela ya mtu mmoja au chama. Kinachofanya watu waongee ni usimamizi na matumizi ya kodi zetu, unatoa kwa masikini unapeleka kwa matajili. Wamepandisha bei ya umeme ikawa haitoshi wakaongeza service charge ya umeme na maji. Hapo naona hajatatua tatizo bali ameongeza.
 
Last edited by a moderator:
Umeme bado ni anasa,maji bado ni anasa kwa mijini na vijijini,licha ya kwamba ni ghali bado hayapatikan,huwa natembelea vijijin watu wana shida sana ya maji,kwa mfano makao makuu ya wilaya ya Kilombero,Ifakara,mji umezungukwa na mito mikubwa ila dumu la maji ni 500-1000/=,kuna mto Lumemo na mto KILOMBERO,sasa nashangaa mji wenye mito una shida ya maji?.Nimegundua kuwa wanasiasa wanategea kutatua matataizo wapate nafas ya kupatia Kura
 

Sisi watanzania tuna elimu ya viwango tofauti lakni kuwepo kwa elimu hiyo hatuna elimu ya utawala bora. Leo hii ukiwaambia wananchi wenye shida ya maji, umeme na miundo mbinu wamuulize kiongozi wao maswali, hakika wengi watatoa pongezi.

Mgombea akisimama jukwaani anajinadi nitawajengea barabara, maji nitawaletea na umeme mtapata. Hakuna wa kumuuliza utafanya hayo yote kwa pesa yako au ya wananchi? Hakuna wa kumuuliza kuwa atatumia mbinu gani kupunguza ukali wa maisha japo kidogo, tunatoa kodi kubwa je, inamalengo yapi kwa taifa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…