Sijui diku hiyo itakuwaje
Mama kaweka wazi kuwa huwa anapitia huku JF na kuperuzi majukwaa mbalimbali, am sure huwa kuna baadhi ya ID, post, replies huwa vinamchekesha sana
Yanayodhaniwa hayawezekani kuna siku yanaweza kuwezekana! Chakula cha usiku /get together wana JF na mama rais kwa mwaliko maalum!
Siku hiyo hao watakaobahatika kualikwa am sure watavunja makabati kwa kutafuta kiwalo kikali cha kuonekana kwenye video na rais
Sasa kichekesho kitakuja hapo ukumbini... Mama akiwa kakaa meza kuu anawaangalia waalikwa wake walivyo wapole na watakatifu... Kwakuwa kutakuwa hakuna kutambulishana ID za JF.. Basi mama atakuwa tu anafanya guess work kichwani mwake [emoji23]
Yule kwa kumtazama tuu ni
rickboy Mzee wa kula tunda kimasihara
Yule kwa pozi lile ni
Asprin mchaga kikongwe asiyependa kuzeeka(siku hiyo atakuwa kaenda saluni kuupiga uso deck na kuweka wave na super black[emoji23]
Mama akiendelea kuangaza kwa taratibu sana atamuona kwenye kona mtu mmoja katulia sana atajisemea huyu hakosi kuwa
Bujibuji Simba Nyamaume
Kwa vyovyote
Maxence Melo atakuwepo akiwa kapendeza sana! Huyu anawatambua baadhi ya members kwa sura.. Kuna kipindi atamuinamia mama na watateta jambo kisha watatabasamu, ujue hapo atakuwa kamuonyesha mama kuwa yule mzee mwenye suti pale ndio
johnthebaptist na pale tayari keshaandika mada tatu za mistari 6
Kuna wanyange pia watakuwepo wamependeza mno kina
Dr. Mariposa na wengine wengi
Hakika itakuwa siku ya furaha kuu.. Ila Team SELFIKA watakosa cha kutupia maana simu zote camera zake zitakuwa hazifanyi kazi kwa muda [emoji23]
Mimi kama nitaalikwa sasa...!
View attachment 2542490