WAKUONDOKA
Member
- Oct 8, 2014
- 46
- 24
Niliwahi kuwaza na kujiuliza hivi wakati mababu zetu wanapokea ustaarabu mpya/dini walikuwa na taratibu zao za kuishi na kila taratibu zilikuwa na mazingira ambayo watu wanaishi chini ya kivuli cha Utamaduni.Ujio wa dini ulikuta watu na mazingira yao na tamaduni zao.
Ila dini zikaingilia tamaduni na mazingira ya watu(ama kwa uzuri/kwa ubaya) zikaja na taratibu mpya za kuishi kwa watu, kwa mf:dini ya kiislam ktk mazingira ilipokuta watu iliingiza utamaduni wa kiarabu(uislam ni imani
haina utamaduni)
1.Iliwavika kofia na kanzu (ikaondoa asili ya Uvaaji)
2.Ikawabatiza majina mapya (ikaondoa asili ya watu) kutoka ktk mazingira yao
Kwa mf: Leo ukimuuliza mtu Maana ya jina Juma au Seif hajui maana yake.
Angalizo: majina ya kibantu yalikuwa yakitolewa kuendana na mazingira/asili yake.
Ilihali hata ukristo unabeba mazila yaleyale ya uislam yani leo ukimuuliza mtu akupe maana ya jina Robert au Daud hajui.
Tafakari yangu...
1.Ivi haikuwa busara kwa mtu akaachwa na mazingira/tamaduni yake apokee imani tu.
Faida yake:
Ingesaidia kuacha watu wakaishi bila hila kwa sababu wako tofauti kiimani ila tamaduni wanashare pamoja.
2.Ingekuwa busara pia watu wakabaki na majina ya asili ikabaki imani tu
Faida yake:
Hii pia ingeacha watu wawe wamoja bila kubaguana kwa majina kwamba uyu ni muislam uyu ni mkristo.
3.Ingesaidia pia imani za watu kubaki moyoni na ingeimarisha zaidi hali ya kuvumiliana kidini(Religious tolerance)
Majumuisho ya yote hapo juu yangesaidia pia kuondoa ubinafsi ktk imani kwa sasa kila mmoja anaona mungu wake ndo sahihi ila si mungu wa mwenzake.
Nawasilisha,nakaribisha michango,mawazo mapya,kukosolewa.