Ramea
JF-Expert Member
- Mar 19, 2015
- 2,146
- 4,090
Nitangulie kwa kusema Utamaduni ni neno pana linalojumuisha mfumo mzima wa Maisha, lengo la Uzi huu ni kuonesha ni jinsi gani tulivyoubeba utamaduni wa kigeni na kuufanya dini zetu na pengine tumenufaika nao ama kuumizwa nao pasipo kujua.
Nitawapitisha kwenye vipengele vya utamaduni 'Culture'. Hapa Ukristo nitauita 'Jewish Culture', Uislam kama 'Arabic Culture' na dini ya mwafrika ambayo ni 'African Traditional Religion' nitaiita African Culture. Kwahiyo nitazungumzia utamaduni wa kiyahudi, kiarabu na kiafrika. Sitarajii kupata maswali ya NINI MAANA YA DINI. Hapa hiyo dini yako naijadili Kama tamaduni tu wa watu fulani.
1. Uongozi na siasa. Waafrika walikuwa na tamaduni zao za kupata kiongozi, pia sheria na kanuni zao kabla ya kuletewa tamaduni mpya za kiarabu zilizoletwa na wa Asia hasa waarabu na kiyahudi zilizoletwa na wazungu. Kwenye makabila mengi, kiongozi wa kijadi alivaa kofia mbili, ya kisiasa na kidini kwenye matambiko. Ukristo ukaleta taratibu zake, siasa na dini zilitenganishwa. Huu ni utamaduni wa kiyahudi ambao haukuwa na uhusiano kati ya makuhani na magavana wa kirumi.
Uislam Kama ilivyo utamaduni wa kiarabu. Siasa na dini hufungamana. Ndiyo maana kuna nchi zinazofuata 'Sharia' za kiislam/kiarabu katika kuamua na kuongoza. Hizo zote ni tamaduni tu za watu, siyo maagizo ya Mungu.
2. Music. Waafrika wana vyombo vyao vya muziki 'music instruments' na styles zao za uimbaji 'musical notations'. Zeze, filimbi, ngoma, pembe za wanyama nk... Wakristo wakachukua muziki wa kiyahudi na kirumi uliotajwa kwenye Biblia. Baragumu, tarumbeta, zeze, vinanda...kuwa muziki safi wa kumwimbia Mungu. Kwa wakatoliki Papa Gregory akapendekeza Tuni fulani itumike duniani kote 'Gregorian music'. Hali kadhalika Waislam na kaswida, dufu ambazo ni musical notation za kiarabu wakazifanya nyimbo za kumsifu Mungu. Ni utamaduni tu, Mungu hana aina fulani ya kuimbiwa.
3. Language. Lugha zetu za kibantu zilitumika kuomba na maombi yakapokelewa. Viongozi wa kimila walitambika kwa Lugha zao kwa Miungu yao. Wazungu wakatuletea ukristo katika lugha ya kilatini. Ibada na misa zilifanyika kwa Lugha hii kwa karne kadhaa. Warumi ndiyo walikifanya kilatini kiwe lugha ya Mungu ingawa Mambo yalibadilika badae. Uislam kwakuwa ni utamaduni wa kiarabu, wao Hadi leo huamini Mungu anajua kiarabu tu. Hakijabadilika chochote. Ni utamaduni tu, hata kichina na kijapani Mungu anakisikia.
4. Food. Chakula katika utamaduni wa kiafrika una makatazo na kanuni za kula chakula. Kulikuwa na hadithi zenye kukataza au kuruhusu chakula/mnyama fulani. Utamaduni wa kiyahudi hali kadhalika, Kuna chakula haram na kisicho haramu, ingawa warumi wamefanya yao kugeuza masndiko. Kuna wakristo wanaokula kila kitu na wale wanaochagua kulingana na mapokeo ya agano la kale la kiyahudi. Waislam pia, utamaduni wa kiarabu katika chakula umebebwa kama ulivyo. Haram na Halal ni kadiri ya utamaduni wa kiarabu ambao walifungamana sana na wayahudi. Ndiyo maana, haram zilizopo katika Agano la kale utazikuta kwenye Qur'an.
5. Art, craft and Architecture. Sanaa na ubunifu. Waafrika tulikuwa na styles zetu za ujenzi wa nyumba za kuishi na ibada michoro na mapambo. Lakini leo hii nyumba za ibada zetu ni sawa na mahekalu ya kiyahudi na kirumi kwa wakristo, kukiwa na nakshi za misalaba. Kwa waislamu nako ni ramani za nyumba za kiarabu, michoro ya kiarabu na alama za 'Mwezi' ambao ni Mungu wa kiarabu aliyeabudiwa hata kabla ya Uislam. Ni tamaduni za watu tumejitwika.
6. Social interaction. Jamii za kiafrika zilikuwa na namna yake ya kuingiliana na kuhusiana kulingana na umri na jinsia. Ukristo wa kale ulibagua sana wanawake Kama ilivyo tamaduni za kiyahudi. Mwanamke alikuwa ni mtu wa 'kusitiriwa' lakini mambo yakabadilika badae, leo hii anasimama Hadi madhabahuni.
Waislam wao wameichukua tamaduni ya kiarabu Kama ilivyo ya kumsitiri mwanamke na kumfanya kiumbe dhaifu. Hachangamani na mwanaume iwe kwenye ibada hadi matukio ya kifo. Hii ni tamaduni ya kiarabu hadi leo, si maagizo ya Mungu, Ni utamaduni tu.
7. Tradition. Hii dhana ni pana.
~Dressing style, waafrika tulikuwa na namna yetu ya uvaaji, Kama ya masai na wengine, lakini ukristu ukatuletea kanzu na majoho. Hayo ni mavazi ya makuhani wa kiyahudi, si kwamba ukivaa shuka la kimasai Mungu hakusikii. Waislam nao kanzu, juba, hijab ambayo ni mavaz ya kiarabu yakafanywa kuwa mavazi rasmi. Ni utamaduni tu, Mungu hakuagiza uvae hayo ili uwe wake.
~Eating style. Namna ya kula kwa waafrika wa zamani ni tofauti na jamii za leo zilizoathiriwa na tamaduni za kiyahudi na kiarabu. Wapo wanaoamini kuwa na namna fulani ya ukaaji,(mezani au mkeka) Mungu hapendi, kisa tu myahudi au Mwarabu alifanya hivyo. Ni tamaduni zao tumezigeuza kuwa dini.
~Festivals. Sherehe na kumbukizi za kiafrika wa kale ni tofauti na za leo. Mtoto wa kiafrika akizaliwa kulikuwa na taratibu zake hadi anaingia utu uzima. Kuanguka kitovu, siku 40... Kwa wakristo utasikia kuna ubatizo, kipaimara (kipaimara ni hatua ambayo ipo hadi leo kwa wayahudi ambao siyo wakristu).... Pasaka pia ilikuwepo kabla ya ukristo. Na Waislam wana yao kama 'Hakika'..... Ambayo hufanyiwa watoto wa kiarabu kadiri ya tamaduni zao, si maagizo ya Mungu.
~Mazishi. Waafrika tukizika kwa namna tofauti tofauti kulingana na tamaduni ya kabila husika. Kuuacha mwili kwenye mapango na kuhama makazi, kufukia chini.... Ukristu umeleta style yake na Uislam hali kadhalika. Matumizi ya sanda, jeneza, kukafini, kuosha maiti ni tamaduni tu za kiarabu na kiyahudi, siyo maagizo ya Mungu.
~Tohara. Kwa waafrika hili jambo lilikuwepo kwa baadhi ya makabila. Wengine hadi Leo hawatahiriwi. Ni utamaduni wao. Kwa wayahudi ni utamaduni wao tangu kale, hali kadhalika waarabu. Kutahiri kumefanywa Jambo la kidini ingawa Ni utamaduni tu. Si agizo la Mungu kwamba hapokei kiumbe chenye 'govi' kwenye makao yake ya milele. Wapo wazungu na waafrika ambao hadi leo hawatahiriwi.
Karibuni kwa mjadala, kusiwe na malumbano ya kupigania Utamaduni wa kiyahudi Wala kiarabu hapa. Tujadili kwa hoja. Huu ni mtazamo wangu tu, unaweza kuwaza tofauti.