Dini imetekwa na miujiza

Dini imetekwa na miujiza

Mbona misikitini na kwenye makanisa ya wasabato ijumaa na jmosi hakuna ndinga nyingi kuliko hayo makanisa unayosema? Am just curious!!
misikitini ndio hakunaga ndinga nyingi, hiyo inajulikana hao ni wavivu wa kufanya kazi, nenda kkkt utakuta ndinga nyingi utadhani ni yard kumbe ni magari ya waumini na hakuna kuombewa miujiza huko
 
Kwahiyo mkiwa nazo nyinyi ni sawa ila wakiwa nazo wa kwa mwamposa ni utapeli sio juhudi na kazi wala miujiza, nauliza tu lkn
 
Hili ni somo lingine tofauti kuhusu kutoa .. Kumbuka ni kwa kutoa ndio tunapokea.. Na hii ni universal law!

Wakati watu wa imani moja wakihimizwa wamtolee Mungu kilicho bora! (Refer sadaka za Abel na Habil) hivyo kuiikuta wanapambana kufanya kazi kwa bidii ili wajenge jengo zuri la ibada na kuwahudumia watumishi( hii automatically ni baraka) kuna imani nyingine inaamini nyumba ya ibada inajengwa na wenye nacho tuuu.. No sharing! Baraka itatoka wapi hapo
Lakini pia kuna standards za maisha zinazotautiana
 
Wanazo sana tuu ila pengine hawapendi kwenda nazo kuepuka kuonekana mambo safi
 
Kumekuwa na nyomi kubwa sana kwa hawa wahubiri wa miujiza. Hizi nyomi ukizichunguza utagundua zinatoka kwenye ile dini, dini ya mnyaazi mungu, a.k.a dini ya haki. Kule wamechoshwa na mafundisho yaleyale karne na karne, wamekosa matumaini, bahati mbaya wanakimbilia kwenye miujiza pasipokuwepo na mafundisho thabiti ya neno la Mungu
 
Kwahiyo mkiwa nazo nyinyi ni sawa ila wakiwa nazo wa kwa mwamposa ni utapeli sio juhudi na kazi wala miujiza, nauliza tu lkn
Unasali kwa Mwamposa? At per hakosi watu elfu 10 kwa ibada moja.. Je wenye 'ndinga kali' ni wangapi? Hawafiki 10% I can assure you!
 
Hili ni somo lingine tofauti kuhusu kutoa .. Kumbuka ni kwa kutoa ndio tunapokea.. Na hii ni universal law!

Wakati watu wa imani moja wakihimizwa wamtolee Mungu kilicho bora! (Refer sadaka za Abel na Habil) hivyo kuiikuta wanapambana kufanya kazi kwa bidii ili wajenge jengo zuri la ibada na kuwahudumia watumishi( hii automatically ni baraka) kuna imani nyingine inaamini nyumba ya ibada inajengwa na wenye nacho tuuu.. No sharing! Baraka itatoka wapi hapo
Lakini pia kuna standards za maisha zinazotautiana
Sawa mkuu umeeleweka
 
Kwahiyo mkiwa nazo nyinyi ni sawa ila wakiwa nazo wa kwa mwamposa ni utapeli sio juhudi na kazi wala miujiza, nauliza tu lkn
hao wa kwa mwamposa wamepata hizo ndinga kwa juhudi zao wenyewe kufanya kazi na sio miujiza. Unataka muujiza wa kuombewa nguvu za kiume? Uharibu nguvu za kiume mwenyewe kwa kutokuzingatia afya ya kula halafu utake muujiza?
 
Unasali kwa Mwamposa? At per hakosi watu elfu 10 kwa ibada moja.. Je wenye 'ndinga kali' ni wangapi? Hawafiki 10% I can assure you!
Hapana sisali kwa mwamposa mm ni muislam

Sipingani na hoja yako ila najiulizaga tu kwanini hawa watu wanaosali kwa mitume feki somehow wanakuwa na life standard nzuri haliyakuwa tunaona wazi kuwa wanatapeliwa! Na ukienda kwenye mihadhara yao hukosi kukuta ndinga za maana

Kingine makanisa mengi siku hizi hasa haya ya kiprotestant yanahubiri profitism ya miujiza na sadaka lakini pia ndinga nje hazikosi tena nyingi na kali tu why?
 
Kumekuwa na nyomi kubwa sana kwa hawa wahubiri wa miujiza. Hizi nyomi ukizichunguza utagundua zinatoka kwenye ile dini, dini ya mnyaazi mungu, a.k.a dini ya haki. Kule wamechoshwa na mafundisho yaleyale karne na karne, wamekosa matumaini, bahati mbaya wanakimbilia kwenye miujiza pasipokuwepo na mafundisho thabiti ya neno la Mungu
Ni kweli, msukumo wa kutafuta miujiza na ufumbuzi wa matatizo magumu ya kimaisha umekuwa kichocheo kikuu kwa watu wengi kukimbilia makanisa yanayoongozwa na manabii na mitume.
Hali hii inachangiwa na mambo kadhaa ya kijamii, kiuchumi, na kisaikolojia:

Changamoto za Kiuchumi na Umaskini: Watu wengi hukimbilia kwa manabii wakitafuta miujiza ya kifedha, ajira, au mafanikio katika biashara kutokana na ukosefu wa fursa za kiuchumi.

Gharama na Uduni wa Huduma za Afya: Katika maeneo ambapo huduma za afya ni ghali au hazipatikani kwa urahisi, makanisa haya yanachukuliwa kama mbadala wa hospitali kwa ajili ya kuponya magonjwa sugu.
Kutafuta Matumaini

(Psychological Hope):
Matatizo ya kimaisha yanapozidi, binadamu huwa na tabia ya kutafuta faraja na matumaini ya haraka kupitia nguvu za kiungu au miujiza.
Imani ya Nguvu za Giza: Katika jamii nyingi, matatizo kama kutokupata watoto au mikosi huchukuliwa kuwa ni matokeo ya ushirikina, hivyo watu huenda kwa manabii kutafuta "ukombozi".

Ushawishi wa Shuhuda:
Shuhuda za watu wanaodai kupata mafanikio au kuponywa zinazosambazwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii huvuta waumini wapya wenye matatizo yanayofanana.

Ni muhimu kuwa na umakini na utambuzi, kwani maandiko pia yanatahadharisha juu ya kuwepo kwa manabii wa uongo wanaotumia miujiza kama njia ya kupotosha au kujipatia manufaa.
 
hao wa kwa mwamposa wamepata hizo ndinga kwa juhudi zao wenyewe kufanya kazi na sio miujiza. Unataka muujiza wa kuombewa nguvu za kiume? Uharibu nguvu za kiume mwenyewe kwa kutokuzingatia afya ya kula halafu utake muujiza?
Sasa utapeli upo wapi hapo na hilo ndio swali langu

Yani mtu atafanywaje masikini kwa kutapeliwa na utapeli wa miujiza na maji ya upako halafu amiliki ndinga inakuwaje!
 
Kinachonishangaza ukienda makanisani siku ya jpili unakuta ndinga za maana zimepaki au wanakodi?
Kwa wale wanaojua ulokole wa zamani, enzi Moses Kulola (RIP) akiwa kijana. Kipindi hicho ungemjua mlokole kwa mavazi yake. Shati unakuta ukosi umechakaa vibaya na nguo zao ni za kishamba kishamba, hata hawana za kubadilisha. Mchungaji anakuja kuhubiri kwenye mkutano kwa daladala. Halafu uende kanisa la kilokole umkute msichana mrembo amevaa na kujipodoa ki-sexy sexy kama sasa? Thubutu! Kweli mambo yamebadilika.
 
Hapana sisali kwa mwamposa mm ni muislam

Sipingani na hoja yako ila najiulizaga tu kwanini hawa watu wanaosali kwa mitume feki somehow wanakuwa na life standard nzuri haliyakuwa tunaona wazi kuwa wanatapeliwa! Na ukienda kwenye mihadhara yao hukosi kukuta ndinga za maana

Kingine makanisa mengi siku hizi hasa haya ya kiprotestant yanahubiri profitism ya miujiza na sadaka lakini pia ndinga nje hazikosi tena nyingi na kali tu why?
OK sawa iko hivi hayo makanisa ya manabii na mitume yako machache sana.. Wana matawi pembezoni mwa miji lakini lile kubwa ndio wakubwa wengi huenda kumfuata mtume/nabii kwakuwa ni zaidi ya ibada
Pale ni makutano ya dili na connection mbali mbali
 
Sasa utapeli upo wapi hapo na hilo ndio swali langu

Yani mtu atafanywaje masikini kwa kutapeliwa na utapeli wa miujiza na maji ya upako halafu amiliki ndinga inakuwaje!
Hao wenye ndinga ni bango la kuwavuta wengine! Kuna watu wanaenda kwenye hayo makanisa kwa malipo sio bure
 
Back
Top Bottom