Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,440
- 1,029
Mwanafunzi mmoja baada ya kufanya kosa shuleni,mwalimu mkuu alimtuma aende nyumbani akamlete mzazi wake.Alipofika shuleni na kuelezwa makosa ya mwanae,baba wa yule mwanafunzi alikasirika na kumpiga mwanae viboko visivyo na idadi huku akisema;"unafikiri kama mimi nisingesoma sana zile mali nyumbani zingepatikana vipi?".Baada ya kumaliza kumwadhibu mwanae,mwalimu mkuu alimpa yule baba barua ya suspension ili atie saini kama mzazi lakini yule baba alikataa kusaini akidai ana hasira mpaka anashindwa kuandika.Baada ya mwalimu mkuu kumshikia bango atie saini,yule baba alimwita mkuu wa shule pembeni na kumwambia;"kusema ukweli mimi sikwenda shule kabisa hivyo sijui hata kalamu inashikwa vipi na siwezi kuandika hata jina langu,nakuomba mkuu tia saini kwa niaba yangu".