Scolari Ndenga
JF-Expert Member
- Aug 4, 2008
- 271
- 43
Nimehamasishwa Sana Na Maoni Yako, Kusoma Na Kuwa Msomi Kunatofauti Kubwa Sana. Pia Kuelimika. Kuelimika Hakuhitaji Shule Ya Darasani Ni Kuwa Na Busara Inayokuwezeza Kupambana Na Maisha Ya Kila Siku Kwa Haki. Kuhusu Hili Suala Kukariri Mimi Huwa Naliita Akili Karirifu Ambayo Ndio Inategemewa Kwenye Academics Karibu Zote Duniani. Hii Inadumaza Sana Akili Inaziba ,mianya Ya Ubunifu Kwa Vizazi. Inakandamiza Akili Asilia Natural Intelgence. Ukija Kwenye Upande Wa Logic Huu Ni Muhimu Sana Kwani Mlolongo Wake Huwa Na Hitimisho La Haki Na Kweli Kutokana Na Mtizamo Wa Mtiu Binafsi
Jamani nimekaa sana na kutafakari mno baada ya kusoma thread kadha wa kadha...!
Pia nimeangalia mno kuangalia status ya vyuo vyetu na kucompare na vya mbele...mmmh!!
Pia tuangalie jinsi vijana wengi wakichoropoka kwenda nje kusoma je kweli wanafata elimu bora ama?!?
Miguu, tafuta kwa bidii fursa ya kwenda kusoma nje hata kama ni semina ya siku mbili. Faida kubwa ni exposure. Kukutana na watu toka mataifa mbalimbali, mkabadilishana mawazo, mkashindana na mkashirikiana ni experience moja nzuri sana. Pili Tanzania tunachofanya ni "catching up" kwa hiyo ni vema ukaenda kuona wale tunaowaiga wamefikia wapi na wanaendesha vipi jamii zao.
Nimehamasishwa Sana Na Maoni Yako, Kusoma Na Kuwa Msomi Kunatofauti Kubwa Sana. Pia Kuelimika. Kuelimika Hakuhitaji Shule Ya Darasani Ni Kuwa Na Busara Inayokuwezeza Kupambana Na Maisha Ya Kila Siku Kwa Haki. Kuhusu Hili Suala Kukariri Mimi Huwa Naliita Akili Karirifu Ambayo Ndio Inategemewa Kwenye Academics Karibu Zote Duniani. Hii Inadumaza Sana Akili Inaziba ,mianya Ya Ubunifu Kwa Vizazi. Inakandamiza Akili Asilia Natural Intelgence. Ukija Kwenye Upande Wa Logic Huu Ni Muhimu Sana Kwani Mlolongo Wake Huwa Na Hitimisho La Haki Na Kweli Kutokana Na Mtizamo Wa Mtiu Binafsi
nitumie email yako tuandike mchakato tukagombee nobel prize. maana kule japani walimfanyia uchunguzi nyani wakadai hana akili kama binadamu wakimshinikiza nyani awe na akili karirifu. wakati akili yake ni kwa ajili yake na maisha ya kila siku huko mwituni. Hata panya anakumbukumbu ya kujua pango lake liko wapi akalale, pia atapatawapi kitoweo chake cha kila siku. kumbukumbu ni sehemu ndogo sana ya akili ya viumbe. email yangu ni tgeofrey@gmail.com
Kwani mtu akisoma nyumbani anazuiwa kusafiri nchi nyingine? Exposure sio lazima iwe ni kwenda kusoma tu, inaweza kuwa ni kutembea kwa kutalii tu. Kwa maana hiyo hata aliyesoma nyumbani na akapata nafasi ya kusafiri na kubadilishana mawazo na watu wengine atapata exposure.
Jambo lingine kusom nje inategemea pia ni level gani ya elimu (msingi, sekondari, shahada ya kwanza, shahada ya uzamili, au shahada ya uzamifu). Kwa maoni yangu ni vizuri zaidi mtu kabla hajaenda nje awe kwanza amesoma shahada ya kwanza nyumbani. Hapo atakuwa na msingi mzuri wa uelewa wa mambo na hali halisi ya nchi yake kuliko ambaye atasomea shahada ya kwanza nje. Kwa kawaida katika fani kama sheria wanafundishwa mambo yanayolenga zaidi sheria za nchi husika, sasa kama mtu atasoma shahada ya kwanza ya sheria Marekani itakuwa ni vigumu sana ku-apply elimu hiyo Tanzania. Kwa hiyo kama ni kusoma nje, basi mtu aende huko kusoma kuanzia shahada ya uzamili.