Dili kusoma Bongo au Mbele?!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dili kusoma Bongo au Mbele?!?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Scolari, Aug 10, 2008.

 1. Scolari

  Scolari JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2008
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jamani nimekaa sana na kutafakari mno baada ya kusoma thread kadha wa kadha...!

  Pia nimeangalia mno kuangalia status ya vyuo vyetu na kucompare na vya mbele...mmmh!!

  Pia tuangalie jinsi vijana wengi wakichoropoka kwenda nje kusoma je kweli wanafata elimu bora ama?!?
   
 2. mpogolo

  mpogolo New Member

  #2
  Aug 10, 2008
  Joined: Aug 10, 2008
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika Sekta ya Elimu Tanzania Bado iko nyuma hivyo basi ni Vizuri zaidi kusoma nje kuliko hapa ili mradi tukirudi tuje kupanua wigo wa Elimu.Ama kuhusu Vijana wengi waliopo nje ni kweli wanfata kusoma au La hasha! Nadhani ni vigumu kulizungumzia jambo hilo!!
   
 3. BantuGirl

  BantuGirl Senior Member

  #3
  Aug 10, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 157
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nafikiri Mtu akisoma nje ya hapa huwa ni nzuri sana maana kuna kitu anajifunza haswa wengi wao upeo wa kufikiri huongezeka....... kuhusu vijana waliopo nje ka wanasoma au la ..... mh hilo linategemeana
   
 4. Mr Kiroboto

  Mr Kiroboto JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  suala la maana ni kuelimika,nikiwa na maana ya kuitumia elimu uliyoipata katika kuwezesha maendeleo ya jamii yako,sasa hapa hatuangalii kusoma marekani,uk,wala china,wala tz.kwani mafisadi wangapi wamesoma nje na wangapi walisoma tz?jibu ni kwamba wapo wengi tu.kuhusu kama wanaoenda nje wanasoma kweli au ala,hiyo pia mtu binafsi,mfano hapa nilipo mie wapo wanafunzi wameacha kusoma wanafanya shughuli zingine wakati lengo lao la kuja hapa ilikuwa kusoma,mie naona hilo nao ni akili ya mtu tu.
   
 5. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  kuelimika ni popote pale vitabu ni vilevile ,sema tofauti inayojitokeza ni jinsi wanafunzi wanavyopagawishwa na wahadhili wao.

  Mtu anaweza soma nyumbani kwake bila kwenda kokote kule akaelimika zaidi kuliko aliyepaa mwezini.Maana huyu anakua na uwanja mpana wa kuhoji na kudadisi mambo tofauti na aliye pale UDSM ama havard anayelazimishwa kukalili ili apasi mtihani yani ya kwamba hapewi uhuru wa kuhoji ama ku logic
   
 6. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa ndugu yangu
  hiyo filosofia yako ya akili karirifu nimeifurahia,achana ni hiyo akili karirifu kuna watu nimesoma nao hawa wazungu wanameza vidonge yani akili yake inakumbuka mambo yote yani akiyameza kila atakachosoma atakumbuka kila kitu hadi koma,nukta.Ila balaa lake ni baada ya mtihani itabidi asinzie siku nzima.

  Kuelimika ni filosofia iliyofichika na saizi kama tungekua kweli tunataka maendeleo tungeanza kufuatilia walio elimika ki kweli kweli.
   
 7. Dar_Millionaire

  Dar_Millionaire JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2008
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Miguu, tafuta kwa bidii fursa ya kwenda kusoma nje hata kama ni semina ya siku mbili. Faida kubwa ni exposure. Kukutana na watu toka mataifa mbalimbali, mkabadilishana mawazo, mkashindana na mkashirikiana ni experience moja nzuri sana. Pili Tanzania tunachofanya ni "catching up" kwa hiyo ni vema ukaenda kuona wale tunaowaiga wamefikia wapi na wanaendesha vipi jamii zao.
   
 8. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #8
  Aug 11, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Inategemea malengo yako kielimu.

  Tangu nimeondoka Tanzania kuna vyuo vingi vimeanzishwa na sijapata bahati kutathmini mitaala yao. Mimi nitakupa mawazo yangu kwa kutumia chuo kikuu cha dar es salaam ambako nilisoma na nikapata bahati ya kufundisha.

  (a) Kama unataka kupata digrii moja tu na kuingia mzigoni ukiwa mahiri sana wa taaluma yako kiutendaji kulingana na taratibu zilizopo basi ni afadhali ukasome nchi za nje. Kwa mitaala ya chuo kikuu cha Dar es Salaama, wanafunzi pale wanafunduisha kufikiri zaidi ya kutenda kwa mikono yao. Huo ndio ukweli wenyewe, na sitaki kuuficha.

  (b) Kama unataka kusoma na kupanda hadi darini (Ph.D) basi ni afadhali uichukulie digrii yako ya kwanza hapo UDSM kusudi utakapoingia kwenye masters huko nje utakuwa na upeo mkubwa kuliko competitors wako wengi na hivyo kuweza kukwea hadi mwisho. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kiko kama Sharif University cha Iran; kinawajenga vijana kwa nguvu sana katika nyanja ya kuchanganya nadharia ili kufikiria mambo mbali mbali, lakini wengi wa wahitimu wanakuwa ni wafikiriaji katika mazingira ambayo yanahitaji vitendo, na hivyo uwezo wao unakuwa haonekani kwa jamii.
   
 9. M

  Mtuwamungu Senior Member

  #9
  Aug 11, 2008
  Joined: Jun 21, 2007
  Messages: 110
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwani mtu akisoma nyumbani anazuiwa kusafiri nchi nyingine? Exposure sio lazima iwe ni kwenda kusoma tu, inaweza kuwa ni kutembea kwa kutalii tu. Kwa maana hiyo hata aliyesoma nyumbani na akapata nafasi ya kusafiri na kubadilishana mawazo na watu wengine atapata exposure.

  Jambo lingine kusom nje inategemea pia ni level gani ya elimu (msingi, sekondari, shahada ya kwanza, shahada ya uzamili, au shahada ya uzamifu). Kwa maoni yangu ni vizuri zaidi mtu kabla hajaenda nje awe kwanza amesoma shahada ya kwanza nyumbani. Hapo atakuwa na msingi mzuri wa uelewa wa mambo na hali halisi ya nchi yake kuliko ambaye atasomea shahada ya kwanza nje. Kwa kawaida katika fani kama sheria wanafundishwa mambo yanayolenga zaidi sheria za nchi husika, sasa kama mtu atasoma shahada ya kwanza ya sheria Marekani itakuwa ni vigumu sana ku-apply elimu hiyo Tanzania. Kwa hiyo kama ni kusoma nje, basi mtu aende huko kusoma kuanzia shahada ya uzamili.
   
 10. N

  Njimba Nsalilwe JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2008
  Joined: Mar 23, 2008
  Messages: 251
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni Bahati Mbaya Sana bila Kukariri Huendi Popote.

  Ni Nani Aliyesoma bila Kuweka Ka-element Ka Kukariri? Kama yupo ninaomba anipe Alifanyaje!

  Njimba
   
 11. s

  susu Member

  #11
  Aug 11, 2008
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 37
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Ukweli ni kwamba Elimu ya Bongo na nyumbani ni tafauti.Nchi za wenzetu wanafunzi wanawezeshwa zaidi kujiongoza wenyewe kuliko kumtegemea mwalimu kitu ambacho kinasaidia kuwa na ufahamu mkubwa wa ufanyacho zaidi ya kukariri.Pia jinsi ya kuutumia muda wako na kuwa mbunifu na kujiamini.Nikiwa kama Mtanzania ninayeishi na kusoma hapa Uk pia nilyesoma nchini Kenya na Nyumbani Tanzania ni kweli kwamba hata hiyo Elimu ya Kenya tu na Tanzania ,sisi tuko Nyuma.Kuhusu watu wankuja kusoma kweli au lah! hiyo inategemea na mtu mwenyewe .Wenzetu wengine wanakiingia mitini kutokana na ugumu wa maisha ada inawashinda.Ufisadi ni roho ya mtu wala haijalishi umesoma wapi kwani hamna chuo kikuu chochote kinachofundisha wanafunzi kuwa mafisadi ,Vyuo vyote lengo lao ni kuuandaa wanachuo wakawe raia wema.Ufisadi ni tabia ya mtu.
   
 12. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #12
  Aug 12, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  mkamap@yahoo.com
   
 13. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #13
  Aug 13, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Ila jamani elimu ya bongo ina bore sana....hasa ya vyuo vikuu.lol
   
 14. Dar_Millionaire

  Dar_Millionaire JF-Expert Member

  #14
  Aug 14, 2008
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mtuwamungu ukienda mahali kama mtalii you'll always be an outsider. Utaona majengo n.k. lakini utakuwa na insights kidogo sana kuhusu fikra zinazoendelea. Ila ukienda kama mwanafunzi, au mfanyakazi una fursa kubwa ya kupata ufahamu mkubwa kuhusu kwa nini watu hao wanafanya vitu unavyoviona.
   
Loading...