Dilemma: Nipiganie Damu Yangu ili Ndoa Zetu Zitikisike au Ninusuru Ndoa Zetu lakini Damu Yangu Ipotee?

Hivi vizingiti tushaviruka sana. Kwa umri huu nadhani vimeshapita Sasa. Binafsi nime experience zaido ya mara 6..Tena wengine Hana hata uhusiano Yan ni serious issue.. na kigezo ni Mimi nahitaji mtoto tu kutoka kwako mengine nayamudu ila Kila nikimfukiria huyu Mama nayashinda ya dunia
 
Story yako inataka kufanana na nichakipitia
Kuna dada nilikua na mahusiano nae sikumwambia kama nna mke na mtoto kwakuwa wife siishi nae mkoa mmoja haikua ngumu kuniamini
Pole kaka. Inabidi tuwe wapole. Jamaa kashauri tujione kama Sperm donor. Ila Mtoto anauma sana wee acha tu
 
Ni wakati mgumu sana, kila ninapomkumbuka mwanangu. Ni wakati mgumu kila ninapopata hisia kwamba naweza kuharibu ndoa yangu. Ni huzuni pia moyoni nikiwaza kuwa naweza kuharibu Ndoa yake.

====================
Ndugu zangu Mwaka....niliingia katika uhusiano na mdada mmoja, ambaye ni Daktari (MD) katika hospital moja hapa Jijini.... Awali mapenzi na huyu dada, niliyachukulia kawaida, kwa sababu tayari nilikuwa nimeshaoa. Nakiri hapa kwamba sikumwambia kama nimeoa, na hakuwa amewahi kuniuliza swali hilo. Tuliendelea na mahusiano yetu vizuri tu, lkn mi nikiwa na tahadhari kubwa sana wife asijue.

Kadri siku zilivyokuwa zinaenda yule dada alizidi kunipenda, sikujua hata ni kwa nini? Sababu hakuna hata chochote cha maana nilichokuwa nakifanya kwake, ukiondoa kusex.

Siku zilivozidi kwenda nikajikuta nimeanza kumependa mno. Yaani, nikifika home naweza kumaliza hata wiki 3 bila kumgusa mke wangu. Hata akitaka namkomalia, anakuwa mpole! Shortly, Mke wangu ni mpole na mustaarabu sana.

Nakumbuka siku moja nilipata Safari ya kwenda Mkoa X kwa siku kama 4, hivi nikiwa huko mida ya usiku saa 4, huyu Dkt alinipigia simu Video call, akanambia amenikumbuka, niwahi nisije kuta nyege zimemuua! Kweli niliamka asubuhi, nikaenda kumalizia kazi iliyonipeleka huko. Hadi kufikia saa 11 nilikuwa nimekamilisha kila kitu.

Niliamua kwenda hadi kituo x na kupanda Malori ya kuja hapa Jijini usiku huo. Nilibahatisha Lori, ambapo tulifanikiwa kufika Alfajiri saa 11:45 hivi.

Kwa namna nilivyokuwa na hamu ya kukutana na Dkt wangu, nilichukua bodaboda, kwenda kutafuta Lodge, badala ya kwenda nyumbani kwa mke wangu. Nilimpigia Dkt nimefika, na kumwelekeza nilipopata room. Yeye nae aliaga kwao kama anenda job, kumbe alikuwa anakuja Lodge.

Saa 1 asubuhi, tulikuwa tumeshaanza kupapasana.Kuchomoka kwenda reception kuulizia Kinga, wakasema hamna, zimeisha. Nikarudi room, kwenda kuipiga kavukavu.Siku hiyo tulikaa hadi saa mbili usiku, huku simu yangu nikiwa nimeweka flight mode, ili wife asinitafute akaharibu, sherehe.

Nilimsindikiza Dkt, Mimi nikarudi kulala palepale, japo nyumbani na hapo nilipokuwa ni chini ya Kilomita 9 tu.

Nilikaa hadi kesho yake, saa 4 asubuhi nikaanza safari ya kurudi nyumbani kwa wife. Nimefika akanipokea kwa furaha zote, na watoto wangu, baaaabaaa, baaaabaaa, baaaabaaa. Nikawabeba pale, tukaingia ndani.

Pole mume wangu, za huko! Nimekutafuta sana jana mume wangu, hukuwa unapatikana! Ulipatwa na tatizo gani!!! Nikajibu ninavyojua, basi yakaisha.

====================
Usiku umeingia wife anataka, mi nikakaza maana nilikuwa nimechoka balaa. Akawa ananiuliza Kuna tatizo gani? Kama Kuna dosari namuona nayo nimsamehe na nimwambie ili airekebishe. Yeye ananipenda, na ana hamu na mimi.

Nilimwambia, Kuna dawa naitumia, hivo mpaka nimalize Miezi mitatu ndo nifanye hilo jambo. Hivo anivumilie tu. Alinipa pole, tukakumbatiana tukalala.

Kuna wakati nilikuwa nikiamka usiku, namkuta anasali au analia. Hata roho ya kumpa pole tu sikuwa nayo. Na ukweli huyu mke wangu ni moja ya watu ambao nina wapenda sana katika maisha. Maana mapito aliyoyapitia kwa ajili yangu ni mengi sana. Si hayo tu lkn nafikiri bond yetu si ya kubahatisha. Japo mwenzangu upendo wake kwangu umezidi. Pamoja na haya yote sijui nini kilitokea. Hisia kwake zilipungua kabisa.

====================
Dkt. aliendelea kushika kasi, hadi siku aliyokuja kunambia hajaona siku zake. Na amepima amebaini kuwa ana ujauzito. Jambo hilo lilinishtua sana. Japo nampenda, na amebahatika kuchukua moyo wangu, lkn katika jicho la kibinadamu nilimuona mke wangu akiwa bora kama mke kuliko Dkt. Na matunda ya mimba yake, yanaweza kuniharibia ndoa yangu, na hasa future ya watoto wangu.

Pamoja na ujinga wote, lakini akili ya kuhudumia familia yangu ilikuwa ipo, isipokuwa sakramenti ya Ndoa tu ndo nilisitisha kushiriki.

Basi ndugu zangu, baada ya kupata taarifa hizo, niliamua kuzipokea kwa furaha, japo kumridhisha tu, lakini moyoni nilipata mtanziko wa mawazo. Nifanye nini? Mtoto? Tena mdogo kuliko wanangu wa kwenye ndoa. Mke wangu atapokeaj? Itakuaje? Nilijiuliza maswali mengi.

Kati ya vitu ambavyo naviogopa ni kuachana na huyu mke wangu. Ni muungwana mno. Hana shida, na anapenda amani. Akija kusikia nina Mtoto nitamuumiza sana. Akibadilika itakuaje? Akiamua kuondoka, hao watoto itakuaje?

Basi nilikata kauli, kwamba nimwambie Dkt ukweli, kwamba nina mke na ni baba wa watoto kadhaa. Niliamua kuandika ujumbe wa sms , usiku saa 4 na kumtumia. Kumwambia kuhusu Mimi kuwa mume wa mtu. So kuhusu hiyo mimba tujadiliane, kujua mustakabali. Aliiopkea na alinijibu tu "sawa"

Tangia hapo sikupata simu yake. Aliniblock kila sehemu. Nami siku zilivoenda, nikaanza kusahau na kurejesha amani katika ndoa yangu. Maisha yakarudi kama kawaida.

Ikumbukwe kuwa katika mahusiano yetu hayo, sikuwa namfahamu hata rafiki yake mmoja na yeye hakuwa akifahamiana na rfk yng au mtu yeyote wa karibu na Mimi. Ilikuwa Mimi na yeye, yeye na Mimi. Labda watu wa ile Lodge tuliyokuwa tumezoea kwenda.

Akinambia kwenda kwangu, namwambia naishi na wazazi wangu, na yeye nilijua anaishi na wazazi wake. Ila sikuwahi kufika, najua tu anaishi sehemu fulani kwa jina. Nyumba na mtaa sijui.

Siku zilipita na Mawasiliano yakiwa hakuna. Nikichukua simu nyingine nikipiga, akijua ni mimi anakata. Baadae akabdili namba kabisa. Nikajua imeisha ngoja nikomae na familia yangu.

Mwezi jana sasa, nimeenda kijiwe fulani kupunga upepo. Nikiwa hapo, ilikuja gari ikapaki, wakatoka watu wazima wawili na Mtoto wa kiume. Walionekana wenye furaha sana. Kuinua uso vizuri namuona Dkt, akiwa na kaka mmoja, wakiwa wamevalia Pete. Yule kaka, akamshika yule Mtoto, wakatembea kuelekea niliko. Wakanipita. Yule kaka alinisalimia, ila Dkt alinibinyia jicho tu, na kumshika mume wake begani wakatafuta sehemu ya kukaa. Wakaketi na kuendelea kupata vinywaji.

Katika yote, ni yule Mtoto. Mtoto ni Mimi kabisa. Tunafanana nae balaa. Jambo ambalo lilinifanya nisogee kwa pembeni kidogo, ili yule kaka asinione, maana naamini angeweza kabisa kunifananisha na huyo Mtoto.

Katika ile movement yangu, kumbe Dkt alikuwa ananichora. Nikashangaa, sms inaingia kwangu.. tafadhali...., akili inanambia kuna kitu unataka kujiridhisha nacho. Tafadhali naomba usiniharibie ndoa yangu ndugu yangu. Nakuomba sana. Nitakupigia nafasi ikiruhusu!

Ukweli, niliamua kuondoka lile eneo. Kesho yake saa 3 asubuhi, Dkt alinipigia tukaongea sana. Na kwamba mme wake anajua huyo mtoto ni wake! Lakini ni wangu, na amempa jina langu. Ila sasa, mme wake anampenda sana Mtoto na atamhudumia kadri ya uwezo. Na kwa kuwa Mimi nina familia yangu, nisjiaribu kufanya chochote kumuaribia ndoa yake. Anadai Wana amani na Mtoto amekuwa kiunganishi kikubwa katika amani yao hiyo. Na kwa kuwa namba yangu anayo, atakuwa ananiambia maendeleo ya Mtoto.

=================================
Hayo yote kwangu ni sawa. Lakini najikuta naumia kuona Mtoto wangu anahudumiwa na mtu mwingine wakat Mimi nipo! Kuna wakati najikuta namkumbuka sana. Cha kuumiza zaidi Mimi nina watoto watatu na mke wangu lkn wote wa kike. Huyo pekee ndo wakiume tu. Nawaza wakati mwingine hadi nakosa Raha.

Pamoja na kukosa Raha, najikuta nikiamini kwamba furaha ya mke wangu inatakiwa ndo iwe kipaumbele, maana anasimamia watoto vizuri, ananipenda na kuniheshimu sana. Nikipigania damu yangu, akajua nitamuumiza sana. Ana imani kubwa sana na Mimi, lakini Mimi sina tabia njema kama yeye. Nimemsaliti, tena bila Kinga.

Zaidi Dkt, tuliishi kwa amani, hakuwahi kunambia neno baya. Hata nilipomwambia kuwa na familia, alisema tu sawa. Hakusema neno baya lolote hadi leo.

Amani ya familia ni kipaumbele, lkn huyo mwanangu ananiuma sana. Hekima na busara ziendelee kutawala, maana sijui kwa kweli.

=Codes zimezingatiwa sana, ili kuendelea kulinda ndoa yake=.

NB:
Ndugu zangu tutulie katika ndoa zetu, hasa tunapokuwa tumebarikiwa wanawake wanaojielewa na wenye upendo kwetu. Tazama haya maumivu ninayopitia ni kutokana na upuuzi wangu tu usiokuwa na kichwa wala miguu. Niko njia panda Wada

Nawasilisha kwa maoni na ushauri!
Mkuu hiyo Ni dhambi usikubali kufa nayo mkuu, tubu kwa MUNGU juu ya hayo ila iendane sambamba na kumwambia mkeo , na kwenda kumchukua mtoto , nafikili mtoto huyo atakuwa Ni mkubwa Sana kwa Sasa, ila usiache huyo mtoto kutokufahamu ,hutapata amani mkuu, mpaka yatimie mkuu.
 
Pole kaka. Inabidi tuwe wapole. Jamaa kashauri tujione kama Sperm donor. Ila Mtoto anauma sana wee acha tu
Kama utakubali kufa na dhambi hio , Basi usijalibu kumchukua mtoto ambapo kashakuwa mkubwa na kashalelewa na huyo mwanaume mwingine, coz SI unajua ghalama za malezi mkuu, usijekuja umiza baadae, Kama kumchukua fanya Sasa hivi au, kufa na hio dhambi.
 
Lugumya; kuna jamaa hapo juu mwenye ID Mapena, amesema " labda nature iamue" nakushauri ukubaliane na hili.

Kwanza mimi nakulaumu sana kwa kutomtendea vyema shemeji yetu. Nawashangaa sana wanaume wenzangu mnabahatika kupata wanawake walio bora lakini hamuwatendei haki na hasa katika karne hii iliyojaa wanawake jinsia, wanawake waliojaa ushetani vichwani mwao, na ndio maana Muumba kakupa za uso.

Nikushauri tu kwamba, endelea tu kuumia rohoni, lakini ukijaribu kujifanya kudai mtoto unaweza kuripua bomu kubwa la Atomic kama lililoangushwa kule Hiroshima na Nagasaki, athari yake najua unaifahamu.

Kumbuka ulipomwambia Dr. unafamilia, alikujibu simple tu 'sawa' then alikuonya usimuharibie ndoa yake. Do you think atakuacha salama? Na anaelea mtoto akizani wake kumbe sio, je atalichukuliaje? Mkeo nae akijua? Ataendelea kukuheshimu? Atakusamehe? Au na yeye attaanza kuchepuka?

Kuna njia mbili tu za kumpata mtoto. Either ndoa yao ivunjike au baba mlezi afariki. Na hilo.muumba ndio anajua .
Mkuu na kukaa nayo moyoni iyo ishu itamsuta Sana, maana uwezi kwenda kanisani na kufanya maombi na sal nyumbani huku Kuna dhambi inakuumiza moyoni , lazima iyo itoke moyoni mwako Kisha ndo ukae vizuri mkuu, na uwe na amani.
 
Wakuu siku zote shetani akikushawishi kufanya dhambi flani lazima I na Matokeo flani katika maaisha yako lazima Hilo KITU kitokee ni wachache sana wananusurioa Tena Ni kwa msaada ya MUNGU tu,. Na ikileta Matokeo flani lazima aache na maumivu flani ndani yako. Na hayo maumivu yanaweza kukutesa mpaka mwisho wa maaisha yako , lakini lengo la shetani Ni kukuangamiza kabisa upotee,
So mkuu kabla halijafuka mbali usisahau kuweka SAWA hio ishu sawa mkuu , Ili UTENGENEZE mahusiano yako na MUNGU yawe mazuri mkuu, nakushauri usije kusahau kabisa hi Lugumya
 
Ndugu yangu ulifanya makosa sana pasipo kumpa ukweli dokta ulipaswa kumwambia kama una familia yamkini dokta asingekubali kujiachia ivyo, yawezekana alijiachia maskini kwa kujua siku moja ungekuja kuwa mme wake wa ndoa kumbe tayali una familia ona sasa majanga unayopitia, mda mwingine tuwe wakweli pia kupitia uo ukwel waweza kukuweka huru kwenye maisha yako.

Ushauri wangu kwako wala usijisumbue kufanya lolote mwache dokta afuraie ndoa yake ambayo alikuwa akiitafuta kwa kitambo pia kumbuka ukiaribu ndoa ya watu iyo dhambi itakuumidha sana. Ila pole sana mwombe mungu atakupa mtoto wa kiume
Mkuu still Ni dhambi ya kuvunja ndoa pia, Kuna dhambi ya kumficha mkewe kuto kuomba msamaha, pia mtoto Ana Hali ya kujua baba yake Ni Nani, na hata huyo dkt bado anadhambi kumdanganya mumewe, so lazima watengeneze mahusiano yao na MUNGU yawe mazuri kwa kueleza ukweli pande zote mbili.
 
wakati mwingine lazima ukubaliane na matokeo ya uzinzi ,sio kuukosa ufalme wa Mbinguni tu,hata hasara nyingine utazipata hapa hapa dunia. tulia hivyo hivyo,hesabu ni matokeo ya dhambi na ndio hasara yake
 
Kama yeye yupo tayari kukaa na maumivu mpo mwisho wake Ni uwamuzi wake binafsi coz ufalme wa MUNGU unatafutwa na mtu mmoja mmoja kea uwamuzi wake binafsi haulaximishwi, Kama ataamua hivyo hivyo sawa.
 
katika ufalme wa Mungu ni lazima atubu na ni lazima aiweke wazi mbele ya mkewe na amwombe msamaha,hapo ndio atapata toba ya kweli Mbele za Mungu,na atapata amani ya kweli
 
Hayo mambo ambayo mwamba kayasema nahisi yananiijia mimi kabisa...
nina shemeji yangu ana mtoto alizaa na dada mmoja, yule dada alimbambiki mimba jamaa mwingine akamuo, lakini mtoto amefafana copy shemeji yangu, shem hana namna emetulia tu
 
Ni wakati mgumu sana, kila ninapomkumbuka mwanangu. Ni wakati mgumu kila ninapopata hisia kwamba naweza kuharibu ndoa yangu. Ni huzuni pia moyoni nikiwaza kuwa naweza kuharibu Ndoa yake.

====================
Ndugu zangu Mwaka....niliingia katika uhusiano na mdada mmoja, ambaye ni Daktari (MD) katika hospital moja hapa Jijini.... Awali mapenzi na huyu dada, niliyachukulia kawaida, kwa sababu tayari nilikuwa nimeshaoa. Nakiri hapa kwamba sikumwambia kama nimeoa, na hakuwa amewahi kuniuliza swali hilo. Tuliendelea na mahusiano yetu vizuri tu, lkn mi nikiwa na tahadhari kubwa sana wife asijue.

Kadri siku zilivyokuwa zinaenda yule dada alizidi kunipenda, sikujua hata ni kwa nini? Sababu hakuna hata chochote cha maana nilichokuwa nakifanya kwake, ukiondoa kusex.

Siku zilivozidi kwenda nikajikuta nimeanza kumependa mno. Yaani, nikifika home naweza kumaliza hata wiki 3 bila kumgusa mke wangu. Hata akitaka namkomalia, anakuwa mpole! Shortly, Mke wangu ni mpole na mustaarabu sana.

Nakumbuka siku moja nilipata Safari ya kwenda Mkoa X kwa siku kama 4, hivi nikiwa huko mida ya usiku saa 4, huyu Dkt alinipigia simu Video call, akanambia amenikumbuka, niwahi nisije kuta nyege zimemuua! Kweli niliamka asubuhi, nikaenda kumalizia kazi iliyonipeleka huko. Hadi kufikia saa 11 nilikuwa nimekamilisha kila kitu.

Niliamua kwenda hadi kituo x na kupanda Malori ya kuja hapa Jijini usiku huo. Nilibahatisha Lori, ambapo tulifanikiwa kufika Alfajiri saa 11:45 hivi.

Kwa namna nilivyokuwa na hamu ya kukutana na Dkt wangu, nilichukua bodaboda, kwenda kutafuta Lodge, badala ya kwenda nyumbani kwa mke wangu. Nilimpigia Dkt nimefika, na kumwelekeza nilipopata room. Yeye nae aliaga kwao kama anenda job, kumbe alikuwa anakuja Lodge.

Saa 1 asubuhi, tulikuwa tumeshaanza kupapasana.Kuchomoka kwenda reception kuulizia Kinga, wakasema hamna, zimeisha. Nikarudi room, kwenda kuipiga kavukavu.Siku hiyo tulikaa hadi saa mbili usiku, huku simu yangu nikiwa nimeweka flight mode, ili wife asinitafute akaharibu, sherehe.

Nilimsindikiza Dkt, Mimi nikarudi kulala palepale, japo nyumbani na hapo nilipokuwa ni chini ya Kilomita 9 tu.

Nilikaa hadi kesho yake, saa 4 asubuhi nikaanza safari ya kurudi nyumbani kwa wife. Nimefika akanipokea kwa furaha zote, na watoto wangu, baaaabaaa, baaaabaaa, baaaabaaa. Nikawabeba pale, tukaingia ndani.

Pole mume wangu, za huko! Nimekutafuta sana jana mume wangu, hukuwa unapatikana! Ulipatwa na tatizo gani!!! Nikajibu ninavyojua, basi yakaisha.

====================
Usiku umeingia wife anataka, mi nikakaza maana nilikuwa nimechoka balaa. Akawa ananiuliza Kuna tatizo gani? Kama Kuna dosari namuona nayo nimsamehe na nimwambie ili airekebishe. Yeye ananipenda, na ana hamu na mimi.

Nilimwambia, Kuna dawa naitumia, hivo mpaka nimalize Miezi mitatu ndo nifanye hilo jambo. Hivo anivumilie tu. Alinipa pole, tukakumbatiana tukalala.

Kuna wakati nilikuwa nikiamka usiku, namkuta anasali au analia. Hata roho ya kumpa pole tu sikuwa nayo. Na ukweli huyu mke wangu ni moja ya watu ambao nina wapenda sana katika maisha. Maana mapito aliyoyapitia kwa ajili yangu ni mengi sana. Si hayo tu lkn nafikiri bond yetu si ya kubahatisha. Japo mwenzangu upendo wake kwangu umezidi. Pamoja na haya yote sijui nini kilitokea. Hisia kwake zilipungua kabisa.

====================
Dkt. aliendelea kushika kasi, hadi siku aliyokuja kunambia hajaona siku zake. Na amepima amebaini kuwa ana ujauzito. Jambo hilo lilinishtua sana. Japo nampenda, na amebahatika kuchukua moyo wangu, lkn katika jicho la kibinadamu nilimuona mke wangu akiwa bora kama mke kuliko Dkt. Na matunda ya mimba yake, yanaweza kuniharibia ndoa yangu, na hasa future ya watoto wangu.

Pamoja na ujinga wote, lakini akili ya kuhudumia familia yangu ilikuwa ipo, isipokuwa sakramenti ya Ndoa tu ndo nilisitisha kushiriki.

Basi ndugu zangu, baada ya kupata taarifa hizo, niliamua kuzipokea kwa furaha, japo kumridhisha tu, lakini moyoni nilipata mtanziko wa mawazo. Nifanye nini? Mtoto? Tena mdogo kuliko wanangu wa kwenye ndoa. Mke wangu atapokeaj? Itakuaje? Nilijiuliza maswali mengi.

Kati ya vitu ambavyo naviogopa ni kuachana na huyu mke wangu. Ni muungwana mno. Hana shida, na anapenda amani. Akija kusikia nina Mtoto nitamuumiza sana. Akibadilika itakuaje? Akiamua kuondoka, hao watoto itakuaje?

Basi nilikata kauli, kwamba nimwambie Dkt ukweli, kwamba nina mke na ni baba wa watoto kadhaa. Niliamua kuandika ujumbe wa sms , usiku saa 4 na kumtumia. Kumwambia kuhusu Mimi kuwa mume wa mtu. So kuhusu hiyo mimba tujadiliane, kujua mustakabali. Aliiopkea na alinijibu tu "sawa"

Tangia hapo sikupata simu yake. Aliniblock kila sehemu. Nami siku zilivoenda, nikaanza kusahau na kurejesha amani katika ndoa yangu. Maisha yakarudi kama kawaida.

Ikumbukwe kuwa katika mahusiano yetu hayo, sikuwa namfahamu hata rafiki yake mmoja na yeye hakuwa akifahamiana na rfk yng au mtu yeyote wa karibu na Mimi. Ilikuwa Mimi na yeye, yeye na Mimi. Labda watu wa ile Lodge tuliyokuwa tumezoea kwenda.

Akinambia kwenda kwangu, namwambia naishi na wazazi wangu, na yeye nilijua anaishi na wazazi wake. Ila sikuwahi kufika, najua tu anaishi sehemu fulani kwa jina. Nyumba na mtaa sijui.

Siku zilipita na Mawasiliano yakiwa hakuna. Nikichukua simu nyingine nikipiga, akijua ni mimi anakata. Baadae akabdili namba kabisa. Nikajua imeisha ngoja nikomae na familia yangu.

Mwezi jana sasa, nimeenda kijiwe fulani kupunga upepo. Nikiwa hapo, ilikuja gari ikapaki, wakatoka watu wazima wawili na Mtoto wa kiume. Walionekana wenye furaha sana. Kuinua uso vizuri namuona Dkt, akiwa na kaka mmoja, wakiwa wamevalia Pete. Yule kaka, akamshika yule Mtoto, wakatembea kuelekea niliko. Wakanipita. Yule kaka alinisalimia, ila Dkt alinibinyia jicho tu, na kumshika mume wake begani wakatafuta sehemu ya kukaa. Wakaketi na kuendelea kupata vinywaji.

Katika yote, ni yule Mtoto. Mtoto ni Mimi kabisa. Tunafanana nae balaa. Jambo ambalo lilinifanya nisogee kwa pembeni kidogo, ili yule kaka asinione, maana naamini angeweza kabisa kunifananisha na huyo Mtoto.

Katika ile movement yangu, kumbe Dkt alikuwa ananichora. Nikashangaa, sms inaingia kwangu.. tafadhali...., akili inanambia kuna kitu unataka kujiridhisha nacho. Tafadhali naomba usiniharibie ndoa yangu ndugu yangu. Nakuomba sana. Nitakupigia nafasi ikiruhusu!

Ukweli, niliamua kuondoka lile eneo. Kesho yake saa 3 asubuhi, Dkt alinipigia tukaongea sana. Na kwamba mme wake anajua huyo mtoto ni wake! Lakini ni wangu, na amempa jina langu. Ila sasa, mme wake anampenda sana Mtoto na atamhudumia kadri ya uwezo. Na kwa kuwa Mimi nina familia yangu, nisjiaribu kufanya chochote kumuaribia ndoa yake. Anadai Wana amani na Mtoto amekuwa kiunganishi kikubwa katika amani yao hiyo. Na kwa kuwa namba yangu anayo, atakuwa ananiambia maendeleo ya Mtoto.

=================================
Hayo yote kwangu ni sawa. Lakini najikuta naumia kuona Mtoto wangu anahudumiwa na mtu mwingine wakat Mimi nipo! Kuna wakati najikuta namkumbuka sana. Cha kuumiza zaidi Mimi nina watoto watatu na mke wangu lkn wote wa kike. Huyo pekee ndo wakiume tu. Nawaza wakati mwingine hadi nakosa Raha.

Pamoja na kukosa Raha, najikuta nikiamini kwamba furaha ya mke wangu inatakiwa ndo iwe kipaumbele, maana anasimamia watoto vizuri, ananipenda na kuniheshimu sana. Nikipigania damu yangu, akajua nitamuumiza sana. Ana imani kubwa sana na Mimi, lakini Mimi sina tabia njema kama yeye. Nimemsaliti, tena bila Kinga.

Zaidi Dkt, tuliishi kwa amani, hakuwahi kunambia neno baya. Hata nilipomwambia kuwa na familia, alisema tu sawa. Hakusema neno baya lolote hadi leo.

Amani ya familia ni kipaumbele, lkn huyo mwanangu ananiuma sana. Hekima na busara ziendelee kutawala, maana sijui kwa kweli.

=Codes zimezingatiwa sana, ili kuendelea kulinda ndoa yake=.

NB:
Ndugu zangu tutulie katika ndoa zetu, hasa tunapokuwa tumebarikiwa wanawake wanaojielewa na wenye upendo kwetu. Tazama haya maumivu ninayopitia ni kutokana na upuuzi wangu tu usiokuwa na kichwa wala miguu. Niko njia panda Wada

Nawasilisha kwa maoni na ushauri!
Pole sana kaka najua inapitia wakati mgumu sana,Cha msingi kuwa au huru ili uwe na amani.Hili swala ukiliacha hivi litakutesa Hadi siku ya mwisho wako apa duniani.Naona dk alikushauri vizuri data ushauri wake na fatilia atua kwa atua Kama kweli alikueleza hivyo navyojua wanawake huyo mtoto utampata Cha msingi nenda hatua kwa hatua.Kwangu Kama ni damu yangu sikubali ipotee kabisa sinaga uvumilivu kuhusu mwanangu.
 
Alikua kaolewa katafuta mtoto kwako kapata,alikua anajua km una mke
Off course we ndo uliingizwa kingi hapo
 
Mkuu still Ni dhambi ya kuvunja ndoa pia, Kuna dhambi ya kumficha mkewe kuto kuomba msamaha, pia mtoto Ana Hali ya kujua baba yake Ni Nani, na hata huyo dkt bado anadhambi kumdanganya mumewe, so lazima watengeneze mahusiano yao na MUNGU yawe mazuri kwa kueleza ukweli pande zote mbili.

Kuna vitu ni rahisi sana kushauri au kuongea kama havijakufika. Unafikiri dhambi ni Moja tu? Kwamba hawana dhambi nyingine isipokua hiyo Moja tu?

Na wewe Kwa vile hauna mtoto nje unaemficha mkeo ndio kigezo Cha kutokua na dhambi?

Hilo jambo linahitaji busara na HEKIMA zaidi ya hisia. Linaweza kusababisha madhara makubwa zaidi ya Hali ilivyo Sasa.
 
Kutokana na maigizo ya Mungu kwenye amri zake, mm naona aliyetendewa ubaya hapa ni mke wa Lugumya ambapo mume wake amemsaliti kwa kuzini na dokta.

Ila kwa upande wa mume wa dokta na yeye hana haja ya kuhurumiwa kabisa ana stahili kabisa aliyotendewa kwa kuivunja amri ya sita kuzini na mwanamke kabla ya ndoa, hayo ndo matunda yake, laiti angefata utaratibu wa Mungu kutokozini kabla ya ndoa basi Mungu angemnusuru kuingia kwenye matatizo ya kulea mtoto asiye muhusu na angemgundua mapema huyu binti dr sio mtu sahihi kwake.

Kwa upande wa dr na mchepuko wake hii dhambi itaendelea kuwatafuna polepole, wamrudia Mungu kwa kuomba neema ya utakaso kufanya kitubio.

Mungu hapoozwi wakuu na wala hadanganywi kwa excuses zetu za hapa duniani, na kwa jinsi anavotupenda ametuwekea na sakramenti ya kitubio kwa kuwa hakuna mkamilifu, sasa ni ww kuchagua kutubu au kupalilia kiburi upate mavuno mengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom