Dilemma: Nipiganie Damu Yangu ili Ndoa Zetu Zitikisike au Ninusuru Ndoa Zetu lakini Damu Yangu Ipotee?

Nisipojua haitoniumiza,nikijua nitaumia ila yote ni juu yako kikubwa wanitunza na magonjwa huniletei....cheat utakavyo heshima yangu niachie.na nguvu za kulea watoto nibakishie nilee wanangu.Siwez pambana na dudu ya mwanaume.Utaangaika utachoka.Katika dunia hii kila kitu ni ubatili atatulia mwishoni akichoka au kaburini
Huyu sasa ndio mwanamke. Jamani mie natangaza ndoa hapa.
 
Ndugu yangu ulifanya makosa sana pasipo kumpa ukweli dokta ulipaswa kumwambia kama una familia yamkini dokta asingekubali kujiachia ivyo, yawezekana alijiachia maskini kwa kujua siku moja ungekuja kuwa mme wake wa ndoa kumbe tayali una familia ona sasa majanga unayopitia, mda mwingine tuwe wakweli pia kupitia uo ukwel waweza kukuweka huru kwenye maisha yako.

Ushauri wangu kwako wala usijisumbue kufanya lolote mwache dokta afuraie ndoa yake ambayo alikuwa akiitafuta kwa kitambo pia kumbuka ukiaribu ndoa ya watu iyo dhambi itakuumidha sana. Ila pole sana mwombe mungu atakupa mtoto wa kiume
 
Hivi kwanini mtu mzuri anakuwa paired na linyang'au. Mke akiwa mwema mwanaume mtihani and vice versa is true. Sasa ona huyu kapata mke mzuri, yeye sasa.... Mshahara wa dhambi ni mauti. Usifikiri kwenye hili unaweza toka salama mkuu unless usurrender maisha yako kwa Mungu.

Its really unfair. Mkeo hajajua lakini I can feel the pain already. Hata ufiche vipi yatakuja kujifunua wazi yooote siku moja.

Tubadilishe lifestyle zetu. Tusikumbatie uzinzi na uasherati. Mwisho wake ni aibu, majuto, fedheha, lawama na mwisho kaburi. Pole nyingi in advance kwa mwanamke huyu..lakini Mungu atamfuta machozi siku moja...wewe mkuu ulichopanda andaa makapu..utavuna tu. Its the lifestyle you chose..live it maisha mafupi pi pi....ishi sasa!!!!

#povulaninikwanimindomkeminami!!#
 
Ni wakati mgumu sana, kila ninapomkumbuka mwanangu. Ni wakati mgumu kila ninapopata hisia kwamba naweza kuharibu ndoa yangu. Ni huzuni pia moyoni nikiwaza kuwa naweza kuharibu Ndoa yake.
We mkuu Kuna mtu amekukata na wembe damu inachuuzika au. Damu si unayo meilini mwako. Mtoto siyo damu Bali Ni sperms tu ambazo zingine huwa zinamwagika ukiwa unapiga nyeto
 
Hivi kwanini mtu mzuri anakuwa paired na linyang'au. Mke akiwa mwema mwanaume mtihani and vice versa is true. Sasa ona huyu kapata mke mzuri, yeye sasa.... Mshahara wa dhambi ni mauti. Usifikiri kwenye hili unaweza toka salama mkuu unless usurrender maisha yako kwa Mungu.

Its really unfair. Mkeo hajajua lakini I can feel the pain already. Hata ufiche vipi yatakuja kujifunua wazi yooote siku moja.

Tubadilishe lifestyle zetu. Tusikumbatie uzinzi na uasherati. Mwisho wake ni aibu, majuto, fedheha, lawama na mwisho kaburi. Pole nyingi in advance kwa mwanamke huyu..lakini Mungu atamfuta machozi siku moja...wewe mkuu ulichopanda andaa makapu..utavuna tu. Its the lifestyle you chose..live it maisha mafupi pi pi....ishi sasa!!!!

#povulaninikwanimindomkeminami!!#
Sawa Mkuu Juandeglo, kwa sasa niko innocent sana tu, sema hilo kosa ndo linaleta dosari katika moyo wangu. Tuombeane tu ndugu yangu.
 
We mkuu Kuna mtu amekukata na wembe damu inachuuzika au. Damu si unayo meilini mwako. Mtoto siyo damu Bali Ni sperms tu ambazo zingine huwa zinamwagika ukiwa unapiga nyeto
Aiseee, likiwa kwa mwingine liko pembeni Kiongozi. Wee unasema tu kirahisi
 
Ndugu yangu ulifanya makosa sana pasipo kumpa ukweli dokta ulipaswa kumwambia kama una familia yamkini dokta asingekubali kujiachia ivyo, yawezekana alijiachia maskini kwa kujua siku moja ungekuja kuwa mme wake wa ndoa kumbe tayali una familia ona sasa majanga unayopitia, mda mwingine tuwe wakweli pia kupitia uo ukwel waweza kukuweka huru kwenye maisha yako. Ushaur wangu kwako wala usijisumbue kufanya lolote mwache dokta afuraie ndoa yake ambayo alikuwa akiitafuta kwa kitambo pia kumbuka ukiaribu ndoa ya watu iyo dhambi itakuumidha sana. Ila pole sana mwombe mungu atakupa mtoto wa kiume
Ahsante sana ndugu yangu!
 
Hakuna cha damu ni DNA kwa kwenda mbele. Mimi niko asilimia 90 kwamba huyu mwanamme anajua kuwa mtoto siyo wake lakini ananyamaza au atakuja kusema siku za mbele hasa wakati watakopogombana na mke wake hata kwa kitu cha kipumbavu kabisa. Na hata hao ndugu zake (hasa mashangazi wapelelezi) ndiyo wa kwanza kusema huyo si wetu tuna wasiwasi.

Jaribu kuangalia 'Paternity court' ya Lauren Lake kwenye youtube utajifunza mengi sana.
Huwa naangalia sana tena kwenye station za south Africa na online youtube. One of my favorite shows to watch. Huwa naangalia pia divorce court. .

Unachosema ndio ukweli hata wkipinga, ukiona mtu kaweka doubt ujue teyari kuna shida mahala. Mahusiano yanahitaji misingi ya uaminifu na good communication, sasa hao wanajidanganya wenyewe. Itatokea mmoja tu ataleta doubts. .
 
Lakini ni dhambi kubwa sana Dokta amefanya kumbambika mtoto huyo jamaa anaeishi naye.

Hivi dhamiri za watu wengine zinakuwa zimekufa kabisa jamani?!
Lazima atafute mlango wa kutokea kwa vile Lugumya ni kama kaikataa mimba na ni dhahiri Doctor alikuwa anagawa kotekote.
 
Ni wakati mgumu sana, kila ninapomkumbuka mwanangu. Ni wakati mgumu kila ninapopata hisia kwamba naweza kuharibu ndoa yangu. Ni huzuni pia moyoni nikiwaza kuwa naweza kuharibu Ndoa yake.

====================
Ndugu zangu Mwaka....niliingia katika uhusiano na mdada mmoja, ambaye ni Daktari (MD) katika hospital moja hapa Jijini.... Awali mapenzi na huyu dada, niliyachukulia kawaida, kwa sababu tayari nilikuwa nimeshaoa. Nakiri hapa kwamba sikumwambia kama nimeoa, na hakuwa amewahi kuniuliza swali hilo. Tuliendelea na mahusiano yetu vizuri tu, lkn mi nikiwa na tahadhari kubwa sana wife asijue.

Kadri siku zilivyokuwa zinaenda yule dada alizidi kunipenda, sikujua hata ni kwa nini? Sababu hakuna hata chochote cha maana nilichokuwa nakifanya kwake, ukiondoa kusex.

Siku zilivozidi kwenda nikajikuta nimeanza kumependa mno. Yaani, nikifika home naweza kumaliza hata wiki 3 bila kumgusa mke wangu. Hata akitaka namkomalia, anakuwa mpole! Shortly, Mke wangu ni mpole na mustaarabu sana.

Nakumbuka siku moja nilipata Safari ya kwenda Mkoa X kwa siku kama 4, hivi nikiwa huko mida ya usiku saa 4, huyu Dkt alinipigia simu Video call, akanambia amenikumbuka, niwahi nisije kuta nyege zimemuua! Kweli niliamka asubuhi, nikaenda kumalizia kazi iliyonipeleka huko. Hadi kufikia saa 11 nilikuwa nimekamilisha kila kitu.

Niliamua kwenda hadi kituo x na kupanda Malori ya kuja hapa Jijini usiku huo. Nilibahatisha Lori, ambapo tulifanikiwa kufika Alfajiri saa 11:45 hivi.

Kwa namna nilivyokuwa na hamu ya kukutana na Dkt wangu, nilichukua bodaboda, kwenda kutafuta Lodge, badala ya kwenda nyumbani kwa mke wangu. Nilimpigia Dkt nimefika, na kumwelekeza nilipopata room. Yeye nae aliaga kwao kama anenda job, kumbe alikuwa anakuja Lodge.

Saa 1 asubuhi, tulikuwa tumeshaanza kupapasana.Kuchomoka kwenda reception kuulizia Kinga, wakasema hamna, zimeisha. Nikarudi room, kwenda kuipiga kavukavu.Siku hiyo tulikaa hadi saa mbili usiku, huku simu yangu nikiwa nimeweka flight mode, ili wife asinitafute akaharibu, sherehe.

Nilimsindikiza Dkt, Mimi nikarudi kulala palepale, japo nyumbani na hapo nilipokuwa ni chini ya Kilomita 9 tu.

Nilikaa hadi kesho yake, saa 4 asubuhi nikaanza safari ya kurudi nyumbani kwa wife. Nimefika akanipokea kwa furaha zote, na watoto wangu, baaaabaaa, baaaabaaa, baaaabaaa. Nikawabeba pale, tukaingia ndani.

Pole mume wangu, za huko! Nimekutafuta sana jana mume wangu, hukuwa unapatikana! Ulipatwa na tatizo gani!!! Nikajibu ninavyojua, basi yakaisha.

====================
Usiku umeingia wife anataka, mi nikakaza maana nilikuwa nimechoka balaa. Akawa ananiuliza Kuna tatizo gani? Kama Kuna dosari namuona nayo nimsamehe na nimwambie ili airekebishe. Yeye ananipenda, na ana hamu na mimi.

Nilimwambia, Kuna dawa naitumia, hivo mpaka nimalize Miezi mitatu ndo nifanye hilo jambo. Hivo anivumilie tu. Alinipa pole, tukakumbatiana tukalala.

Kuna wakati nilikuwa nikiamka usiku, namkuta anasali au analia. Hata roho ya kumpa pole tu sikuwa nayo. Na ukweli huyu mke wangu ni moja ya watu ambao nina wapenda sana katika maisha. Maana mapito aliyoyapitia kwa ajili yangu ni mengi sana. Si hayo tu lkn nafikiri bond yetu si ya kubahatisha. Japo mwenzangu upendo wake kwangu umezidi. Pamoja na haya yote sijui nini kilitokea. Hisia kwake zilipungua kabisa.

====================
Dkt. aliendelea kushika kasi, hadi siku aliyokuja kunambia hajaona siku zake. Na amepima amebaini kuwa ana ujauzito. Jambo hilo lilinishtua sana. Japo nampenda, na amebahatika kuchukua moyo wangu, lkn katika jicho la kibinadamu nilimuona mke wangu akiwa bora kama mke kuliko Dkt. Na matunda ya mimba yake, yanaweza kuniharibia ndoa yangu, na hasa future ya watoto wangu.

Pamoja na ujinga wote, lakini akili ya kuhudumia familia yangu ilikuwa ipo, isipokuwa sakramenti ya Ndoa tu ndo nilisitisha kushiriki.

Basi ndugu zangu, baada ya kupata taarifa hizo, niliamua kuzipokea kwa furaha, japo kumridhisha tu, lakini moyoni nilipata mtanziko wa mawazo. Nifanye nini? Mtoto? Tena mdogo kuliko wanangu wa kwenye ndoa. Mke wangu atapokeaj? Itakuaje? Nilijiuliza maswali mengi.

Kati ya vitu ambavyo naviogopa ni kuachana na huyu mke wangu. Ni muungwana mno. Hana shida, na anapenda amani. Akija kusikia nina Mtoto nitamuumiza sana. Akibadilika itakuaje? Akiamua kuondoka, hao watoto itakuaje?

Basi nilikata kauli, kwamba nimwambie Dkt ukweli, kwamba nina mke na ni baba wa watoto kadhaa. Niliamua kuandika ujumbe wa sms , usiku saa 4 na kumtumia. Kumwambia kuhusu Mimi kuwa mume wa mtu. So kuhusu hiyo mimba tujadiliane, kujua mustakabali. Aliiopkea na alinijibu tu "sawa"

Tangia hapo sikupata simu yake. Aliniblock kila sehemu. Nami siku zilivoenda, nikaanza kusahau na kurejesha amani katika ndoa yangu. Maisha yakarudi kama kawaida.

Ikumbukwe kuwa katika mahusiano yetu hayo, sikuwa namfahamu hata rafiki yake mmoja na yeye hakuwa akifahamiana na rfk yng au mtu yeyote wa karibu na Mimi. Ilikuwa Mimi na yeye, yeye na Mimi. Labda watu wa ile Lodge tuliyokuwa tumezoea kwenda.

Akinambia kwenda kwangu, namwambia naishi na wazazi wangu, na yeye nilijua anaishi na wazazi wake. Ila sikuwahi kufika, najua tu anaishi sehemu fulani kwa jina. Nyumba na mtaa sijui.

Siku zilipita na Mawasiliano yakiwa hakuna. Nikichukua simu nyingine nikipiga, akijua ni mimi anakata. Baadae akabdili namba kabisa. Nikajua imeisha ngoja nikomae na familia yangu.

Mwezi jana sasa, nimeenda kijiwe fulani kupunga upepo. Nikiwa hapo, ilikuja gari ikapaki, wakatoka watu wazima wawili na Mtoto wa kiume. Walionekana wenye furaha sana. Kuinua uso vizuri namuona Dkt, akiwa na kaka mmoja, wakiwa wamevalia Pete. Yule kaka, akamshika yule Mtoto, wakatembea kuelekea niliko. Wakanipita. Yule kaka alinisalimia, ila Dkt alinibinyia jicho tu, na kumshika mume wake begani wakatafuta sehemu ya kukaa. Wakaketi na kuendelea kupata vinywaji.

Katika yote, ni yule Mtoto. Mtoto ni Mimi kabisa. Tunafanana nae balaa. Jambo ambalo lilinifanya nisogee kwa pembeni kidogo, ili yule kaka asinione, maana naamini angeweza kabisa kunifananisha na huyo Mtoto.

Katika ile movement yangu, kumbe Dkt alikuwa ananichora. Nikashangaa, sms inaingia kwangu.. tafadhali...., akili inanambia kuna kitu unataka kujiridhisha nacho. Tafadhali naomba usiniharibie ndoa yangu ndugu yangu. Nakuomba sana. Nitakupigia nafasi ikiruhusu!

Ukweli, niliamua kuondoka lile eneo. Kesho yake saa 3 asubuhi, Dkt alinipigia tukaongea sana. Na kwamba mme wake anajua huyo mtoto ni wake! Lakini ni wangu, na amempa jina langu. Ila sasa, mme wake anampenda sana Mtoto na atamhudumia kadri ya uwezo. Na kwa kuwa Mimi nina familia yangu, nisjiaribu kufanya chochote kumuaribia ndoa yake. Anadai Wana amani na Mtoto amekuwa kiunganishi kikubwa katika amani yao hiyo. Na kwa kuwa namba yangu anayo, atakuwa ananiambia maendeleo ya Mtoto.

=================================
Hayo yote kwangu ni sawa. Lakini najikuta naumia kuona Mtoto wangu anahudumiwa na mtu mwingine wakat Mimi nipo! Kuna wakati najikuta namkumbuka sana. Cha kuumiza zaidi Mimi nina watoto watatu na mke wangu lkn wote wa kike. Huyo pekee ndo wakiume tu. Nawaza wakati mwingine hadi nakosa Raha.

Pamoja na kukosa Raha, najikuta nikiamini kwamba furaha ya mke wangu inatakiwa ndo iwe kipaumbele, maana anasimamia watoto vizuri, ananipenda na kuniheshimu sana. Nikipigania damu yangu, akajua nitamuumiza sana. Ana imani kubwa sana na Mimi, lakini Mimi sina tabia njema kama yeye. Nimemsaliti, tena bila Kinga.

Zaidi Dkt, tuliishi kwa amani, hakuwahi kunambia neno baya. Hata nilipomwambia kuwa na familia, alisema tu sawa. Hakusema neno baya lolote hadi leo.

Amani ya familia ni kipaumbele, lkn huyo mwanangu ananiuma sana. Hekima na busara ziendelee kutawala, maana sijui kwa kweli.

=Codes zimezingatiwa sana, ili kuendelea kulinda ndoa yake=.

NB:
Ndugu zangu tutulie katika ndoa zetu, hasa tunapokuwa tumebarikiwa wanawake wanaojielewa na wenye upendo kwetu. Tazama haya maumivu ninayopitia ni kutokana na upuuzi wangu tu usiokuwa na kichwa wala miguu. Niko njia panda Wada

Nawasilisha kwa maoni na ushauri!
Kwa hapo naona kaa kimya tu.... Mtoto angekua anaish maisha ya shida ndio ungeingilia Kati Ila kwa sasa kaa kimya na usimfuatilie kabisa.... Usije kosa vyote
 
Back
Top Bottom