Digital broadcasting: naomba nieleweshwe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Digital broadcasting: naomba nieleweshwe!

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by JAYJAY, Feb 24, 2012.

 1. JAYJAY

  JAYJAY JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 31, 2008
  Messages: 2,495
  Likes Received: 824
  Trophy Points: 280
  katika huu utaratibu mpya, nilisikia kuna makampuni matatu yaliyopewa haki ya kuendesha mfumo huo, mawili ni star times, agape, la mwisho sikumbuki jina lake lakini nakumbuka linahusiana na itv/star tv. naomba kueleweshwa

  1. je kampuni hizi zitakuwa zinahusika na matangazo ya tv pekee au na redio pia?

  2. je hawa watu wa dstv na zuku tv wao wanahudumiwa na nani hivi sasa? kwani wapo ndani ya hizo kampuni tatu? na kama hawapo mfumo ukianza rasmi wao watakuwa wanaangukia wapi kwa sababu waliopewa haki hizo ni kampuni hizo tatu tu?

  3. watumiaji wa tv watalazimika kutafuta decoder, vipi kuhusu watumiaji wa redio, kutakuwa na mahitaji yeyote kwao pia?
  4. ni kweli kuwa mmiliki wa redio au tv binafsi hatalazimika kuwa na mitambo ya kurusha matangazo kila mkoa bali kazi hiyo itafanywa na kampuni hizo tatu kwa malipo?
  5. hakuna uwezekano wa kampuni zote hizo kutumia decoder moja, na kuondoa ulazima wa kuwa na mlundikano wa decoder pia kupunguza gharama? (kama vile mtumiaji wa simu anakuwa na simu moja lakini ana uwezo wa kuweka laini za mitandao tofauti hivyo halazimiki kuwa na simu nyingi). au teknolojia hairuhusu?
  naomba niishie hapa kwa leo!
   
 2. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  hizo ni sera tu kaka kwa tecnlogia ya tanzania bado tuko nyuma
  kwa wenzetu kama hapa nilipo natumia canal digital ambayo ni service provider wanahost cable zingine ndani yake
  kama DTV,smarttv nk ndani yake kuna channel zaidi ya 100 pamoja na radio channels,hawa wanatumia fibres kumfikia mteja na sio satelite. ndani yake unapata pia internet na simu.zipo pia analogue channels lkn radio hata kama huna cable hiyo bado zinapatika on air kama ilivo bongo.hawa waliingia digital 10 years ago.kwa hivo tv stations zinabaki kuwa content providers lkn miundombinu ni ya service provider.
  kwa Tanzania nchi maskini makampuni 3 ya nn? mwananchi atawezaje kununua decorder 3 ili kupata local channels?
  ni mzigo kwa wananchi,bado haijakaa sawa hii. TCRA wanatakiwa wakasomee ICT kabla ya kukurupuka.hakuna kitakachozimwa tarehe hiyo waliotangaza.miundo mbinu bado duni na ni garama sana kurusha matangazo kwa satelite wkt wenzao nchi tajiri wanatumia fibres,labda watuambie ule mkonga wa mawasiliano upo tayari na unapatika nchi nzima
   
 3. M

  Majala Kimolo JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 344
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mhishimiwa vuta subira kidogo tupate uffanuzi kutoka kwa watu wa TCRA huwa wanafika huku. Ni kitambo kiasi upo nje ya nchi hii, yawezekana huna picha ya kuwa Mkongo wa taifa umefika mbali sana. Ili utoe maoni ya kutosha unatakiwa uwe na taarifa za kutosha pia. Karibu Bongo
   
Loading...