Huyu kwangu ndie alikuwa mchezaji bora wa karne, sio Pele.
Kwanza aliwafunga waingereza goli la mkono wakapiga sana kelele kwa refa akakataa, jamaa ni kama akawaambia nyie hamnijui, goli lililofuata aliwapiga chenga karibia timu nzima ya Uingereza mpaka kipa wao akaenda kuweka kambani, hapo akawafunga midomo kabisa.
Hiyo ilikuwa ni World Cup final ya 1986, mpaka leo nakiri kusema hapajatokea wa aina yake.
R.I.P Diego Armando Maradonna.