Kuwa diaspora hasa hapa US ilikuwa kitu kigumu sana hasa kwa vijana wengi ambao tuliondoka tukiwa na miaka 1997-2001 baada ya kumaliza high school. Sio tu kulikuwa hakuna Watanzania wengi miaka hiyo 1997-2001 bali wengi walikuwa wadogo hivyo tulikuwa hatuna mifano mingi ya kuiga. Lakini kibaya zaidi wazee wa Kitanzania ambao walikuwa wasomi wakati huo wengi waliwakimbia Watanzania vijana na kuona ni kama mizigo.
Baada ya miaka 25 jumuia zimekuwa na mafanikio sana. Kuna wasomi wengi, wafanyabiashara wengi na hata watoto wa kizazi kipya wengi wamefanikiwa kwenye vyuo vya juu sana. Hizi hatua nyingi wengi hawazifahamu lakini Watanzania wamepiga hatua sana diaspora hasa US
Tushukuru Mungu kwa hili na tuanze mikakati ya kusaidia nchi yetu. Sasa tuna wataalamu kila mahali