Diaspora Na Uraia Pacha Tanzania

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,810
Suala La Uraia Pacha Tanzania

Suala la uraia pacha limejitokeza tena kuwa hoja nzito katika mkutano wa tatu wa uratibu wa wadau Watanzania wanaoishi ughaibuni (diaspora), huku baadhi wakiitaka Serikali kuharakisha mchakato wa kuanzisha utaratibu huo.

Walisema Watanzania wanaoishi nje ya nchi wanapata adha kubwa na wengine wanashindwa kuwekeza, kurudi au hata kusaidia familia zao kile walichochuma kwa sababu tofauti zikiwemo za usumbufu na kupanda kwa gharama.

Mbunge wa Viti Maalum, Leticia Nyerere, (CHADEMA), alisema suala la uraia pacha ni muhimu na kwa sasa halikwepeki. Aliitaka serikali kuharakisha utaratibu wa huo ili kuwapunguzia adha Watanzania wanaoishi nje ya nchi na ambao hawataki kuukanauraia wao, “Kuwa na uraia pacha ni muhimu, wapo Watanzania waliokwenda Marekani kwa sababu tu ya ukimbizi wa kiuchumi na wakapata watoto huko, lakini watoto wao wanakuwa ni Wamarekani, kama kungekuwa na uraia pacha, hao wangeweza kuwa raia wa Tanzania na Marekani kwa wakati mmoja,” alisema.

Pia alisema Mtanzania aliyezaliwa Marekani akiwa na uraia pacha hataweza kuhatarisha vitegauchumi vyake iwapo atapenda kuwekeza nchini au hata huko Marekani, “Watu wetu wa diaspora wanafanya mambo mengi na makubwa katika kuchangia uchumi wa taifa letu, lakini kwa kuwa misaada yao haijaorodheshwa na hakuna takwimu, michango yao haijulikani,” alisema na kuongeza: “Naiomba serikali kulitafutia ufumbuzi suala lauraia pacha mapema

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, John Haule, alisema suala la uraia pacha ni la Muungano na la kikatiba na kuwa lipo kwenye mchakato na litapatiwa ufumbuzi kwa kuwashirikisha Watanzania wote (Bara na Visiwani). Alisema kutokana na vuguvugu la mchakato wa kuwa na Katiba Mpya suala hilo linaweza kujadiliwa na kupatiwa ufumbuzi. Aidha, Haule alisema wizara yake imezielekeza balozi zake zote kuorodhesha Watanzania wanaoishi nje, shughuli wanazozifanya na utaalamu walionao ili kuwapa nafasi nzuri ya kuwekeza nchini kama wanataka.


- Nipashe
 
Back
Top Bottom