Diana Chilolo aseme ukweli kuhusu elimu yake

Suala la elimu TZ lipo very seriaz aiseee!! Yaani tukifanya accessement dah, std wengi sana wataumbuka, lakini ni wachapakazi wazuri by the way
 
Ukifuatilia sana siasa za bongo unaweza kuwa chizi, namuhurumia sana Dr.Slaa. By the time hé becomes a President atakuwa ashapata brain atrophy atakayofuatiwa na senile dementia.
Hii nchi imefika hapa ilipofika baada ya baadhi ya watu kukaa pempeni na kudhani kuwa wapo watu maalumu wenye kustahili kufuatilia siasa.Ukweli ni kuwa inatupasa sote tuifuatilie siasa na matendo ya wanasiasa kwa kuwa siasa ni sehemu ya maisha yetu na hakuna tutakachopoteza zaidi ya unyonge wetu.Hata kusoma threads hapa JF ni moja ya njia za kufuatilia siasa...Kukaa kwetu pembeni hakuwezi kuwa kinga dhidi ya maamuzi ama matendo ya wanasiasa..
Wanasiasa wababaishaji , hasa wa Kiafrika,kwa asili yao ,wangependa kuona kuwa wananchi wachache,kadiri iwezekanavyo wanashiriki siasa.
 
unapoteza muda, hivi sio vya kuumiza mkuu!! hangaika kuiondoa CCM madarakani, kwani hana mimi natumia jina la Mwenge , siifahamu, sijui hata iko wapi, ila nalitumia jina vizuri tu kupatia ugali wangu wa kila siku! na mimi sio mwanasiasa.....''umenielewa??"

Nimeelewa ulichosema ingawa sikubaliani na baadhi ya mawazo yako.
Siku zako zinahesabika maana huwezi kujua kama ktk orodha ya wahitimu feki tunayoiandaa upo ama laa.Kwa hiyo usijiamini sana.
Hoja kuwa tuhakikishe tunaiondoa CCM madarakani haijibu hoja yangu ya msingi ya watu kudanganya umma kuhusu elimu zao.
Hata kama nitakubaliana na hoja yako,kitendo cha kumwanika huyu mama hapa JF ni mbinu na mkakati mojawapo wa kuiondoa CCM madarakani.
Mchakato wa kuwaanika watu wanaolitumia jina la shule yetu hauangalii itikadi wala cheo cha mtu ,ingawa kwa data tulizonazo tunatabiri kuwa wahanga wengi watatoka CCM.
 
Ukimwangalia vizuri ktk vikao vya bunge huwa anapenda sana kukaa karibu na EL. Mama anajua kujipenyeza. Sishangai akiwa waziri au naibu waziri kwa jinsi magamba walivo na akili mgando
 
Ukimwangalia vizuri ktk vikao vya bunge huwa anapenda sana kukaa karibu na EL. Mama anajua kujipenyeza. Sishangai akiwa waziri au naibu waziri kwa jinsi magamba walivo na akili mgando

Hivi kumbe Bungeni Mbunge anachagua pa kukaa?
 
Inaniuma sana.Nataka kuandaa orodha ya viongozi wanaotumia vibaya jina la shule yetu.Naomba wahitimu wa MWENGE SEKONDARI mniunge mkono.Shule yetu imetoa watu makini sana wanaolitumikia taifa letu ktk nafasi na ngazi mbalimbali nchini.Mfano JAJI KIPENKA MUSA KIPENKA wa Mahakama Kuu ya TANZANIA ,na ambaye pia amepata kuwa Katibu wa Bunge miaka ya 2000 ,amesoma pale miaka ya 1970 na wengi wetu tunajivunia sana mafanikio yake kitaaluma.

Mimi pia nilisoma hiyo shule yenu na sijivunii chochote.
 
makamu mwenyekiti kamati ya nishati na madini ataongea nini na makaburu wa barick africa,wakati unge'ng'e hamna
 
wekeni kila kitu hadharani!mbona za wengine mnazibandika hapa?bandikeni na zake tuelewe.
 
Mimi pia nilisoma hiyo shule yenu na sijivunii chochote.

Sikumaanisha kujivunia kusoma Mwenge..Ukisoma kwa umakini hiyo sentensi hapo juu,nililkuwa naamanisha mafanikio ya kitaaluma na kikazi ya JAJI KIPENKA MUSSA KIPENKA akiwa mhitimu wa MWENGE na ambaye anaipenda sana shule yake hiyo ya zamani.
Hata hivyo, kwa sababu mbalimbali,wapo wasiojivunia mahali wanakotoka, wanaodharau makabila yao na hata wanaojidharau wao wenyewe. Kwa hiyo wewe kutojivunia kusoma Mwenge iliyofunguliwa na JK Nyerere mwaka 1967,haishangazi sana...
 
unapoteza muda, hivi sio vya kuumiza mkuu!! hangaika kuiondoa CCM madarakani, kwani hana mimi natumia jina la Mwenge , siifahamu, sijui hata iko wapi, ila nalitumia jina vizuri tu kupatia ugali wangu wa kila siku! na mimi sio mwanasiasa.....''umenielewa??"

waberoya you are boring!
 
Sikumaanisha kujivunia kusoma Mwenge..Ukisoma kwa umakini hiyo sentensi hapo juu,nililkuwa naamanisha mafanikio ya kitaaluma na kikazi ya JAJI KIPENKA MUSSA KIPENKA akiwa mhitimu wa MWENGE na ambaye anaipenda sana shule yake hiyo ya zamani.
Hata hivyo, kwa sababu mbalimbali,wapo wasiojivunia mahali wanakotoka, wanaodharau makabila yao na hata wanaojidharau wao wenyewe. Kwa hiyo wewe kutojivunia kusoma Mwenge iliyofunguliwa na JK Nyerere mwaka 1967,haishangazi sana...

Ha ha ha haaa...!!!! Haya bana!
Umemaliza lini Shule pale Mwenge? Uliishi wapi? Mimi niliishi Kujitegemea a.k.a "MAGEREZA" kwa miaka minne.

Mwenge haitonisahau!
 
Gazeti la Mwanahalisi ktk toleo lake na.279 ukurasa wake wa Tisa, la wiki hii limechapisha mahojiano kati yake na ndugu Diana Chilolo mbunge wa viti maalumu,CCM mkoa wa Singida.Mwishoni mwa mahojiano, ameeleza kuwa amesoma ktk shule ya Sekondari Mwenge iliyopo mjini Singida.Napenda kuchukua fursa hii kuueleza umma kuwa mama huyu hakuwahi kusoma Mwenge Sekondari na yafaa hapa ifahamike wazi kuwa hana elimu ya sekondari.
Tovuti ya bunge inaonyesha kuwa eti amepitia Mwenge kwa masomo ya Kidato cha Tano na Sita mwaka 1997.Hili katu haliwezi kuwa kweli maana,kwa makusudi kabisa, ameacha kueleza shule alikopatia elimu ya kidato cha Nne.Sote twafahamu kuwa kwa mujibu wa mfumo wa elimu wa Tanzania ,kusoma na kufaulu Kidato cha Nne ni sharti la lazima kwa mtu kuweza kufanya mtihani wa Kidato cha Sita.Kwa hiyo haiwezekani usome Tanzania ktk ngazi ya Kidato cha Sita bila kusoma kidato cha NNE.
Jamii iwe makini na hawa matapeli wa elimu waliotapakaa kote nchini.Nimesoma Mwenge Sekondari na nimekataa kukaa kimya wakati jina la shule yetu linatumiwa na wanasiasa wababaishaji kama huyu mbunge wa viti maalumu.
Kweli mkuu! nimepitia web site ya Bunge,haionyeshi O level kasoma wapi!
 
Nenda ktk tovuti ya bunge, halafu ingia option ya members, baada ya hapo tafuta Diana Chilolo.Kama wewe ni mtu makini ,CV yake itakushangaza.Common sense tu inakutaka uelewe kuwa mwaka 1997, anaodai alikuwa Mwenge kwa masomo ya kidato cha Sita,alikuwa tayari na miaka 43 tangu azaliwe.Sasa hili halihitaji regester wa shule kuweza kubaini utapeli wa ndugu Diana..
Mimi sio register wa hiyo shule, bali nimepata elimu yangu pale kihalali kwa hiyo historia yangu ya kielimu na kimaisha, imefungamana moja kwa moja na Mwenge Sekondari.

Haina tofauti na Nchimbi aliyejiita dr miaka mingi iliyopita halafu aka graduate mwaka jana PHD yake

Chakla ya mzee Six hiyo...

Kha!!! Hivi kumbe mzee six anatabia mbaya namna hii..mama Magreth six anajua hii habari? Lakini mkuu kuna taarifa kuwa huyu mama ni kambi ya white hair.Sasa inakujaje hapa tena wawe na ushikaji na six wakati six na white hair ni kama paka na mbwa? Au huyu mama anatumika na white hair kumchakachua mzee six,na hapa atapigwa poison asipokaa mkao mzuri....
 
Ha ha ha haaa...!!!! Haya bana!
Umemaliza lini Shule pale Mwenge? Uliishi wapi? Mimi niliishi Kujitegemea a.k.a "MAGEREZA" kwa miaka minne.

Mwenge haitonisahau!

Kwa sababu ya unyeti wa suala ninalolifuatilia kwa sasa na kwa sababu za kiintelijensia naomba nisitaje mwaka niliosoma pale..Ila elewa tu kuwa nimeishi bweni la Jamuhuri na Azimio.
 
Kwa sababu ya unyeti wa suala ninalolifuatilia kwa sasa na kwa sababu za kiintelijensia naomba nisitaje mwaka niliosoma pale..Ila elewa tu kuwa nimeishi bweni la Jamuhuri na Azimio.

Kila la heri, endelea kufuatilia. Ukihitaji msaada zaidi tuwasiliane!
 
Hivi hatuwezi kufanya initiative tukamfikisha mahakama kwa udanganyafu wa ELIMU akavuliwa huo ubunge kama alivyowahi kufanya Dr. Masumbuko Lamwai dhidi ya Kihiyo? Hawa waongo tutaendelea kuwalea hadi lini?

Hili suala la kuchakachua ELIMU limekuwa so notoroius kwa wabunge wetu! tulikomeshe vipi? Hapa mimi huwa ndiyo CCM wananiacha hoi, STD VII unampatia kuwa Kaimu mwenyekiti tena wa kamati ya Nishati? Hivi jamani CCM mko je? Ujinga kama huu ndiyo unatufanya tuwachukie. Kwanini basi hata msingempatia yule Mbunge Kijana na Muleba somebody Mwijage ambaye amefanya kwenye sector hiyo kwa miaka mingi. Au basi wasomi wengine waliojaa huko CCM au kwakuwa wao sio watu wa NDIYO MZEE?!

Kusema kweli CCM mnatu let sana down, tukiwa nje hii ni AIBU yetu wote sio ya nyinyi CCM tu! Please give us break, we are tired na USANII wenu.
 
Wazo zuri sana mkuu... kwa kuwa mamlaka zinazohusika na elimu nchini zimekaa kimya kuhusu hili tatizo sugu,na kwa kuwa baadhi ya wabunge wawapo bungeni, badala ya kuuliza maswali ama kutoa michango ya mawazo inayogusa mustakabali wetu, wao wanaijadili Jamiiforums ,sasa tunapaswa tujikomboe sisi wenyewe kwa kuliendesha hili zoezi sisi wenyewe ,kwanza kwa kuwaanika wahusika hadharani ikifuatiwa na hatua za kisheria dhidi ya wahusika
 
Back
Top Bottom