Diana Chilolo aseme ukweli kuhusu elimu yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diana Chilolo aseme ukweli kuhusu elimu yake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by FortJeasus, Feb 4, 2012.

 1. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Gazeti la Mwanahalisi ktk toleo lake na.279 ukurasa wake wa Tisa, la wiki hii limechapisha mahojiano kati yake na ndugu Diana Chilolo mbunge wa viti maalumu,CCM mkoa wa Singida.Mwishoni mwa mahojiano, ameeleza kuwa amesoma ktk shule ya Sekondari Mwenge iliyopo mjini Singida.Napenda kuchukua fursa hii kuueleza umma kuwa mama huyu hakuwahi kusoma Mwenge Sekondari na yafaa hapa ifahamike wazi kuwa hana elimu ya sekondari.
  Tovuti ya bunge inaonyesha kuwa eti amepitia Mwenge kwa masomo ya Kidato cha Tano na Sita mwaka 1997.Hili katu haliwezi kuwa kweli maana,kwa makusudi kabisa, ameacha kueleza shule alikopatia elimu ya kidato cha Nne.Sote twafahamu kuwa kwa mujibu wa mfumo wa elimu wa Tanzania ,kusoma na kufaulu Kidato cha Nne ni sharti la lazima kwa mtu kuweza kufanya mtihani wa Kidato cha Sita.Kwa hiyo haiwezekani usome Tanzania ktk ngazi ya Kidato cha Sita bila kusoma kidato cha NNE.
  Jamii iwe makini na hawa matapeli wa elimu waliotapakaa kote nchini.Nimesoma Mwenge Sekondari na nimekataa kukaa kimya wakati jina la shule yetu linatumiwa na wanasiasa wababaishaji kama huyu mbunge wa viti maalumu.
   
 2. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Chakla ya mzee Six hiyo...
   
 3. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Kihiyo mwingine huyo.! Ila haina noma kwa kuwa yuko CCM siyo inshu sana...
   
 4. logbes

  logbes Member

  #4
  Feb 4, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tupe data zake wewe sasa maana unabisha tu. we ni registry wa hiyo shule?
   
 5. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Hata kama ni wa CCM inabidi tumfuatilie hadi kieleweke.
  Hatuwezi kumuacha aendelee kuupotosha umma kwa kuzingatia ukweli kuwa huyu mama kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini.Kukaa kwetu kimya kunawapa hawa wababaishaji nafasi ya kufanya watakacho.Mtu mwenye elimu ya DARASA LA SABA hawezi kuja na mapendekezo na majibu ya tatizo sugu la umeme.
   
 6. Kimbojo

  Kimbojo JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2012
  Joined: Apr 12, 2009
  Messages: 387
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huyo mama ni mwalimu wa UPE , kama kajiendeleza kafikia labda kwa kupitia MUKA (mafunzo ya ualimu kazini). Hana kidato cha sits wala nini. Kama ni mwaka anaoutaja 1997 kwa watahiniwa wa kujitegemea (walimu) wa mainspaa ya sinigida waliofanya mtihani huo Mwenge walikuwa 5 tu, naye hakuwepo, sasa kiongozi huyo andanganya umma hadharani bila aibu hafai. Nasikia baada ya kuwa mmbunge alipelekwa UK kusoma english kozi. Hana lolote zaidi ya hapo kielimu, kama ataonesha cheti atakuwa amefoji.
   
 7. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #7
  Feb 4, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Nenda ktk tovuti ya bunge, halafu ingia option ya members, baada ya hapo tafuta Diana Chilolo.Kama wewe ni mtu makini ,CV yake itakushangaza.Common sense tu inakutaka uelewe kuwa mwaka 1997, anaodai alikuwa Mwenge kwa masomo ya kidato cha Sita,alikuwa tayari na miaka 43 tangu azaliwe.Sasa hili halihitaji regester wa shule kuweza kubaini utapeli wa ndugu Diana..
  Mimi sio register wa hiyo shule, bali nimepata elimu yangu pale kihalali kwa hiyo historia yangu ya kielimu na kimaisha, imefungamana moja kwa moja na Mwenge Sekondari.
   
 8. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #8
  Feb 4, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Inaniuma sana.Nataka kuandaa orodha ya viongozi wanaotumia vibaya jina la shule yetu.Naomba wahitimu wa MWENGE SEKONDARI mniunge mkono.Shule yetu imetoa watu makini sana wanaolitumikia taifa letu ktk nafasi na ngazi mbalimbali nchini.Mfano JAJI KIPENKA MUSA KIPENKA wa Mahakama Kuu ya TANZANIA ,na ambaye pia amepata kuwa Katibu wa Bunge miaka ya 2000 ,amesoma pale miaka ya 1970 na wengi wetu tunajivunia sana mafanikio yake kitaaluma.
   
 9. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #9
  Feb 4, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  unapoteza muda, hivi sio vya kuumiza mkuu!! hangaika kuiondoa CCM madarakani, kwani hana mimi natumia jina la Mwenge , siifahamu, sijui hata iko wapi, ila nalitumia jina vizuri tu kupatia ugali wangu wa kila siku! na mimi sio mwanasiasa.....''umenielewa??"
   
 10. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #10
  Feb 4, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu kwanini usimvue nguo sokono kwa kuweka data zake za ukweli hapa jamvini?
   
 11. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #11
  Feb 4, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Yupo wapi Kainerugaba msemakweli aka FISADI WA ELIMU Atueleze!
   
 12. M

  Makunga JF-Expert Member

  #12
  Feb 4, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 772
  Likes Received: 497
  Trophy Points: 80
  Mmh,huyu mama niliwai kumsikia bungeni anasema yeye ni ticha wa primary,i wonder khs hiyo form 6 yake.
   
 13. G

  GALIMA JF-Expert Member

  #13
  Feb 4, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  daah!!uongo mwingine bwana???nackitika mbunge wangu kuudanganya umma.wadanganye wanyaturu tu,kwingine utaumbuka mama
   
 14. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #14
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,739
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  Yaani kuna wabunge hawana hata elimu ya sekondari?!
   
 15. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #15
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Jamani Kainerugaba yupo wapi? ALikuwa ameshikilia orodha ya watu aliodhani wamefoji? Yuko wapi huyo jamaa?
   
 16. Amakando

  Amakando Senior Member

  #16
  Feb 4, 2012
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nakumbuka wakati anagombea nafasi hiyo kwa mara ya kwanza watu walihoji elimu yake akachimba mkwara kuwa atakayemfuatilia itakula kwake watu Kimya, kwao shelui na inasemekana ni mtaalamu wa mambo ya utamaduni wa kiafrika.
   
 17. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #17
  Feb 4, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Kinachoniuma ni kitendo cha kumchezea rafu za kisiasa na hatimaye kumshinda Mhadhiri Mwandamizi wa UDSM Dkt.Rebecca Sima ktk uchaguzi wa ubunge wa viti maalumu CCM mwaka 2005 na baade 2010... mimi si mwana CCM japo naihusudu sana ile moja ya Ahadi za MWANA TANU inayohimiza kusema kweli daima.
  Ninaandaa orodha ya viongozi wa umma na wale wa kisiasa wanaotumia vibaya jina la Mwenge Sekondari, na ninatarajia kuiweka wazi orodha hiyo hapa JF hivi karibuni. Ninawahakikishia orodha hiyo itatikisa sana wahusika na washirika wao, maana hadi sasa nina majina ya wanasiasa maarufu hapa nchini wanaoji identify na shule hii na bila shaka watalazimika kujiuzulu nafasi zao.Sihongeki na wala simwonei mtu huruma maana sikumtuma yeyote kuudanganya umma.
  Wahitimu wenzangu wa Mwenge niungeni mkono tafadhali.
   
 18. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #18
  Feb 4, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135

  Ufafanuzi kidogo unahitajika hapo kwenye red
   
 19. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #19
  Feb 4, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Ni wazi Kinachomaanishwa hapo kwenye red ni uchawi.Kwa elimu na upeo wa huyu mbunge mbabaishaji wala siwezi kushangaa.
  Sasa kwa kuwa nimeamua kumuanika aniloge.Namuhakikishia kuwa hawezi kuniloga maana kama kulogwa siogopi hata kidogo na Mungu wa Yakobo amekuwa ananilinda na kuniepusha mara nyingi na hila za wachawi na wao wenyewe wamesalimu amri kwangu.
   
 20. m

  msabato masalia Senior Member

  #20
  Feb 4, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ukifuatilia sana siasa za bongo unaweza kuwa chizi, namuhurumia sana Dr.Slaa. By the time hé becomes a President atakuwa ashapata brain atrophy atakayofuatiwa na senile dementia.
   
Loading...