Diamond Platnumz aweka rekodi YouTube barani Afrika

Diamond Platnumz aweka rekodi YouTube barani Afrika

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,341
Diamond Platnumz kila kukicha anaendelea kuweka rekodi kwenye muziki wake na awamu hii sio views wa kwenye mtandao wa YouTube bali ni Subscribers.

Diamond kwenye akaunti yake ya YouTube tayari amefikisha Subscribers milioni 1+ na kuwa msanii wa muziki wa 8 barani Afrika kuwa na Subscribers zaidi ya milioni 1.

Kwa sasa Diamond Platnumz ameungana na wasanii kama Amr Diab kutoka Misri mwenye Subscribers milioni 1.6, Kundi la muziki la Die Antiwoord kutoka Afrika Kusini subscribers milioni 1.8, Dzjoker Chemsou milioni 1.6, Lartiste milioni 2.2, Ilias Tiiw milioni 1.8, Sofia Carlsberg milioni 1.8 .

Wengine ni Tamar Hosny milioni 2.8, shady Srour milioni 2.8 wote kutoka Misri na Saad Lamjarred kutoka Morocco ambaye ndiye msanii wa muziki anayeongoza kwa bara la Afrika kuwa na Subscribers wengi milioni 4.4 .

Kwa upande wa wasanii wengine kutoka Afrika kama Davido, Wizkid, Yemi Alade, Tiwa Savage, Sarkodie, Alikiba na Cassper Nyovest wote bado hawajafikisha Subscribers milioni 1 ingawaje hao wanatumia mtandao wa VEVO, na akaunti inayoongoza kuwa na Subscribers wengi ni ile ya kundi la PSquare ina subscribers laki 7.

Wiki iliyopita Diamond Platnumz aliachia album yake ya ‘A BOY FROM TANDALE’ na tayari imepokelewa vizuri na mashabiki wa muziki barani Afrika ambapo imeanza kutrend kwenye mitandao ya kununulia nyimbo kwenye baadhi ya nchi kama Burkina Faso, Oman, Namibia, Kenya, na Malaysia na kwenye mitandao mikubwa ya kimuziki kama SPOTIFY.

Screenshot_2018-03-19-14-01-25-1.jpg
 
Ukiwekeza kwenye juhudi na kujituma, matokeo mazuri yanakuja yenyewe. Sasa wale wazee wa kuponda, eti ananunua view,watapinga. Yaani YouTube wa verify acc yako na wakupe tuzo hiyo ya gold, maana yake wana uhakika na acc yako na wamesha monitor na kufanya ukaguzi wa views na subscribers wako kuwa wapo sahihi.
 
wengine watasema ananunua subscribers..dah
 
mimi sijawahi kuona msanii aliye serious akifurahia ama kushangilia viewers kweny eyoutube.Huku ni danganya toto kabisa kwanini anakataa kujisubscribe kwenye zile channel za mbele? Huku youtube si ata DAB ana viewers 10M
 
Eti kama amekuwa mwanamuziki wa 8 ndo anakuwa kavunja rekodi? Au mimi sijui maana ya kuvunja rekodi?
mwanamuziki gani tanzania au afrika.mashariki ambaye ana subscribers milioni moja..??! je kati ya wizkid/davido/tiwa savage,,japo wako vevo nani ana subscribers milioni 1??
kwani kuvunja rekodi ni.lazima uwe namba moja?! au kiswahili.hujakielewa hapo

fally ipupa kaanza muziki 2009, ana subscribers laki 5 na 90 kwa sasa, alikiba kaanza muziki 2006 na ana subcribers laki 1 na 57 hadi sasa katika you tube yake ya kawaida ila vevo ana elfu 97,

diamond kaanza music 2009 sawa na fally ipupa lakin ana subscribers milioni 1 sasa kwa you tube account yake, na vevo ana 98k

wizkid kaanza music 2001, you tube yake ya kawaida ana subscribers laki 1, na ya vevo ana laki 3...

davido ameanza music 2011, you tube account yake ya kawaida ana subscribers elfu 7, ila.ya VEVO ina laki 5...

sasa see the difference!!!
 
mimi sijawahi kuona msanii aliye serious akifurahia ama kushangilia viewers kweny eyoutube.Huku ni danganya toto kabisa kwanini anakataa kujisubscribe kwenye zile channel za mbele? Huku youtube si ata DAB ana viewers 10M
aisee..dig deep...kawaulize akina drake wenye 9 million kwamba inawasaidia nini katika muziki business yao...kuna kijana mdogo.tu mswedish anaitwa alex.. dogo tu ana subscribers milioni 60, you tube wanamlipa zaidi ya bilioni 25 za kitanzania kwa mwaka ...
sasa tofaut ya alex na diamond ni nini...alex ni mtu wa video games, diamond ni muziki...sasa hapa nimekufafanulia kidogo tu..je bado unaona hamna umuhimu wa "kushangilia" SUBSCRIBERS?!
 
kumuelimisha mjinga Ni matumizi mabaya ya data
 
Back
Top Bottom