Diamond platinumz ashusha thamani ya shillingi ya TZ

Diamond platinumz ashusha thamani ya shillingi ya TZ

"Huyu kijana kila akienda nje anarudisha nyumbani dola nyingi kama laki mbili.....".
Daah! Dollar laki mbili kweli inaweza kuleta athari katika uchumi wetu? Hauko serious mkuu...katikati ya jiji sasa hivi nyumba hupati kwa hiyo amount,..labda kijiapartment tu ghorofa ya sita kuendelea.
 
Naona huyu mchumi namba moja topic ya macro-economy alichengana na mwalimu...
 
yaani inawezekana mwalimu kwa mwaka akawa analipa kodi kubwa kuliko anayolipa DIAMOND PLATINUM... kwani diamond anakale kamachine ka electronic???,,, vipi maodita naye wanamkagua kama walivyoenda kwa gwajima,, maana hizi hela wanazotutangazia kwenye magazeti wanapata halafu kodi hawalipa hamuoni kama wanatunyonya hawa??? kuna haja ya kuhakikisha hawa jamaa nao wanalipa kodi na wale bongo movie walipe kodi na ili tumpunguzie mwalimu huu mzigo... Kila siku wanasanii watanzania wanalilia hati miliki hati miliki lakini hatuwasikii wakiandamana kuishinikiza serikali wanataka kulipa Kodi kama watanzania wengine walivyoelemewa na huu mzigo hasa wafanyakazi>>>>....

TIME FOR FACT NA SIO UJANJAUJANJA...

Mkuu serikali iki ikusanye kodi ni lazima itengeneze miundombini ya sehemu inayataka kukusanya kodi

Serikali haija wekeza nguvu zake kutengeneza mazingira mazuri kukusanya kodi kwenye sanaa

Hela unazoona Diamond anaidhumu serikali hazifikii hela mbayo serikali inawadhulumu wasanii kwa kuto watengenezea miundo mbinu kufaidi kazi zao

Wasanii wanakufa masikini sababu serikali haiwajali kwa maana ya kuwatengenezea mazingira mazuri wafaidi na serikali ifaidi......watu wakodi wanalijua hili huwezi kumkamua maziwa ng'ombe usiyemtunza

Sio Diamond tu, matamasha makubwa yapo kila siku, madalali hawalipi kodi, wenye nyumba za kupangisha hawalipi kodi, tunauziana magari na mashamba na majumba hatulipi kodi

Kodi inaandaliwa mazingira mkuu sio unadai tu
 
Back
Top Bottom