Diamond Karanga. Mafanikio Ya Diamond na karanga zake

Diamond Karanga. Mafanikio Ya Diamond na karanga zake

Makau Js

Member
Joined
May 25, 2017
Posts
93
Reaction score
233
b1bdace96df7d0146c923cab05cd9d96.jpg
Wanasema kwenye kila mafanikio ya mwanaume nyuma yake kuna mwanamke ambaye huwa ni mama mzazi kisha anakuja mke wako ,hawa ni watu wenye Baraka katika mafanikio ya kila mwanaume.

Pia umaarufu huleta jina zuri na pesa na hasa muhusika ukijitambua na kutumia vyema jina lake na umaarufu wake basi pesa huwa inakufuata wewe na wewe unaichukua pesa kisha unaikata miguu inatulia kwenye wallet yako na kwenye accounts zako za Bank.

Pesa inatulia kwenye accunt zako zote mbili , kwenye account ya In God We trust[USD] ,na kwnye account ya pesa yetu ya Hapa kazi tu [Tsh] pesa inatulia na kukusikiliza wewe utakavyo kisha yeye inakutii wewe.

Naseeb Abdul Juma, wazazi walimpa jina hili ila yeye akaamua kujipa jina la biashara ambalo litampa mvuto na pesa akaamua kujiita , Diamond Platnumz, basi kwa kuwa jinaa huumba tabia ya mtu , Naseeb Abdul Juma amekuwa Diamond Platnumz wa kweli na wa uhakika mwenye jina,pesa na umaarufu kama ilivyo Diamond halisia.

Mabinti wa Tanzania ,walikosa ubongo wenye macho,hawakuwa na mioyo yenye macho kuweza kujua hitaji la Diamond ,alikuwa anahitaji nini nyuma ya umaarufu wake ?

Jina huumba tabia na tabia hutengeneza mwenendo wa mtu .
Zari akapata Zari lake kama jina lake jinsi lilivyo sababu alikuwa ana macho yenye ubongo na moyo wenye jicho:akajua hitaji la Diamond Platnumz ,akaingia kwenye moyo wa Diamond akawa Auditor wa penzi akamkagua akajua huyu ni kijana mdogo anahitaji mtoto kisha akampatia mtoto.

Mwanamke mtundu anayejitambua huwa mjinga na mwerevu na mtulivu anayemsoma mwanaume mapungufu yake na ubora wake.Zari kama kawaida anammiliki kijana ambaye anapendwa na warembo wengi Tanzania na Africa ,ila yeye alitumia akili yake na umri wake kumteka Diamond Platinumz.

Kwenye biashara ,nimependa sana Product design ya [DIAMOND KARANGA] huu ndio unaitwa ubunifu wenye tija katika kizazi hiki cha vijana wajuaji wasio na ubunifu katika uwekezaji makini kwa kutumia pesa katika biashara nzuri.

Ukimchukia Diamond Platnumz kwa kutomtizama kwenye YouTube ,basi mwanao atakulazimisha umletee Diamond Karanga ili ale, Zari the Boss Lady anacheza vyema karata zake na Diamond anatumia vyema jina lake .Kila jambo na wakati wake na huu ni wakati wa Diamond.

Tumia vyema umaarufu wako na tumia vyema pesa yako sababu pesa huja na kuondoka ,na umaarufu haudumu milele na kuwa makini kwenye kuchagua mwanamke/mwnaume uwapo na jina zuri wengi hufuata umaarufu na umaarufu ukiondoka na wao huondoka.

Biashara ya chakula haina msimu ila biashara ya nguo ina msimu ,niliona nguo za TMK Wanaume Halisi,Niliona nguo za East Coast na sasa naona Diamond Karanga.

Mwenyezi Mungu akimbariki mwanadamu na wewe unatakiwa umpe Baraka zake huyo mwanadamu sababu ,ukimlaani mtu aliyebarikiwa na wewe unapata laana na ukimbariki mtu aliyebarikiwa na wewe unabarikiwa . Whoever is trying to bring you down is already below you.[emoji146][emoji183][HASHTAG]#BongoCelebrity[/HASHTAG]


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeandika porojo nyingi ambazo hazieleweki.. Haya fupisha.. Hoja yako hasa ni nini?
 
Ktk kuepukana na umasikini Jina lako ,biashara na uwekezaji ndivo vitakutoa !!.


Asante somo .
 
Shhittt..... Unahadithia hadithi.. Acha hzo!??
 
Mkuu kama kitu hujui ni heri ukauliza kwa watu ,

Hizo Diamond Karanga sio mali ya diamond ,diamond ameingia nao ubia tu na kampuni inayotengeneza hizo karanga na hizo karanga zipo mtaani tangu 2015.
 
Mkuu kama kitu hujui ni heri ukauliza kwa watu ,

Hizo Diamond Karanga sio mali ya diamond ,diamond ameingia nao ubia tu na kampuni inayotengeneza hizo karanga na hizo karanga zipo mtaani tangu 2015.
Najiuliza mbona Diamond hatangazi hizo karanga kwenye video zake.
 
Hizo karanga naona kama ni za smart industry wanauza similar products na ndio wanaofanya kila kitu kuanzia production mpaka distribution. Diamond naona kama vile anatumika kama brand tu ila all in all ni jambo zuri.
 
Diamond ana promote tuu sio za kwake. Zipo siku nyingi sokoni naona sasa hao smart industries wameamua kuzi primote na ku market kwa nguvu mpya watu wengi walikuwa hawazijui ila zilikuwa zinapatikana madukani siku nyingi.
 
Back
Top Bottom