Diamond hakuna unachodaiwa Kwenye music, lakini muombe saana Harmonize aendeleee kuwa juu la sivyo endelea kusimamia Biashara zako

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
2,161
1,493
Nafikiri ni nature tu vitu viwili vinavyovyutana huvuma saana

Kanumba na Ray Kigosi walivuma saana kwenye bongo movie, sio kwa sababu walikuwa bora saana ila ushindani uliokwepo, Mwenyezi Mungu alipo mchukua Kanumba mbele za haki, Ray Kigosi I think ametafuta shughuli nyingine ya kufanya.

Nasma Hamis Kidogo Vs Hadija Kopa, kwa wale wahenga kidogo wanajua jinsi wababe hawa wa taarabu walivyokuwa kuwa juu lakini Najma alivyoenda mbele za haki Kopa tunamuona tu kwenye matamasha ya Zuchu tumesahau hata kama naye ni Mwanamuziki.

Ray C Vs Komando Jide , Ray C alipopata changamoto na kupotea kwenye music hata Lady Jay dee kwa sasa anazidiwa mpaka na mabinti wa juzi licha ya kuwa Jay dee nyimbo zake zina ujumbe, zinaishi, zinaelimisha kuliko hawa mabinti wanaoimba za kwikwi jogoo anawika.

Ally Choki na Banza Stone, hii miamba ina historia kubwa kwenye music wa dansi wa kisasa, lakini baada ya Banza stone kutangulia mbele za haki, kwa mara ya mwisho nilisikia Ally Choki amekuwa MC ametafuta.

Uwepo wa Simba Imara ndio kunafanya Yanga ifanye vizuri zaidi.

Vitu viwili vinavyovyutana sio kwa ubaya ila kwa kuendeleza kitu fulani ni jambo jema, ushindani huleta ubunifu na jitihada za kufanya vizuri.

Diamond endelea kuombea saaana Harmonize aendeleee kuwepo wepo kwenye game, Tanzania yote inajua hakuna unachodaiwa kwenye bongo flavour lakini ukweli mchungu pia kuwa nyimbo zako sio za kuishi, nyimbo za chutama mkongojo upite ni nyimbo zinazoishi siku chache, upinzani wako na Harmonize kwa sasa unakufanya uwe juu kimuziki na Harmonize bila wewe kuwa juu naye jioni tu atakuwa amesahaulika maana nyimbo za koh koh sio za kuishi.

Akina Marijani Rajabu etc ndio waliotengeneza nyimbo za kuishi.

Sio kwa ubaya kwa soko la sasa linahitaji nyimbo hizo mazoimba, Music umekuwa Biashara kubwa hivyo ni lazima uzalishe product inayotakiwa na wateja..

Ni muhimu saana wakati unaombea familia yako USISAHAU KUMUOMBEA ADUI YAKO MAANA KUNA NAMNA ANAFANYA AU ANAMCHANGO WA WEWE KUWEPO HAPO ULIPO YAWEZEKANA HATA BILA YEYE KUJUA.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
 
Mleta mada ni kichaa sana....ulishawai sikia wasanii wote hao uliowataja hapo miaka ya nyuma mmoja waoa anasema hasingekuwa huyu mm nisingekuwepo,walikuwa wanaimba ila wanaimba kwa ushindani,Harmoze alishawai kusema Diamond ni Baba yake kwenye maisha ya mjini kila anachokujua kajifunzia kwa Diamond.
Sema diamond labda kama alimwosha huyo KIAZI wako machimbo yote ya kusavive mjini,Zaid ya hapo aeendelee tu kumwimbia kajala nyimbo za kuachana.
 
Siuoni huo ushindani wa Diamond na Harmonize naona mnaufosi uwe hivyo, ushindani wa Diamond na Kiba ndio ulikuwa ushindani wa kweli kwa maana walikuwa wanakaribiana kwenye fan base, wanashindana kwa maneno na hata upande wa ngoma lakini pia hata kwenye upande international walikuwa washindani Sana na hii ilipelekea kuwe na urushwaji wa vijembe kwa pande zote mbili.

Sasa ukiangalia kwa Diamond na harmonize Diamond kamzidi Sana harmonize fan base kwa kiasi kikubwa gap ni kubwa Sana, ukija kwenye international level ndio kabisa hakuna kitu alichofanya harmonize umlinganishe na Diamond

Diamond anaweza asitoe wimbo kwa muda mrefu na still akapata shows nyingi na jina lake likaendea kama vile ana nyimbo na hii nguvu alikuwa nayo pia Kiba je harmonize ana hiyo nguvu?

Ukija kwenye mauzo ya mziki kuna kipindi Kiba alikuwa juu zaidi ya Diamond ukija kulinganisha diamond na harmonize achilia tu Diamond kuwa top ya kazi zake kuuzika Sana wanaofuatia ni Zuchu, Rayvanny, mbosso na Marioo Harmonize anakuja kushika nafasi ya 5 sasa huo ndio ushindani gani unazungumzia mtoa mada?
 
Mleta mada ni kichaa sana....ulishawai sikia wasanii wote hao uliowataja hapo miaka ya nyuma mmoja waoa anasema hasingekuwa huyu mm nisingekuwepo,walikuwa wanaimba ila wanaimba kwa ushindani,Harmoze alishawai kusema Diamond ni Baba yake kwenye maisha ya mjini kila anachokujua kajifunzia kwa Diamond.
Sema diamond labda kama alimwosha huyo KIAZI wako machimbo yote ya kusavive mjini,Zaid ya hapo aeendelee tu kumwimbia kajala nyimbo za kuachana.
Umecomment kihisia....rudia kusoma utamwelewa mleta mada
 
Sina team, sipo kwa Mondi, Kiba wala Harmonize, ila kiuhalisia Diamond hamtegemei Harmonize ili aendelee kung'aa kimuziki. Hawafanani, Diamond na Kondeboy ni mbingu na ardhi. Kiufupi kwasasa Tz Diamond sio wa kufananishwa na ng'ombe yeyote
Huna ufahamu wowote juu ya soko la muziki,
Hujui nguvu za wafuasi kwa msanii,
Tatizo mnajibu kwa hisia kuliko uhalisia.
 
Huna ufahamu wowote juu ya soko la muziki,
Hujui nguvu za wafuasi kwa msanii,
Tatizo mnajibu kwa hisia kuliko uhalisia.
Harmonize sio mshindani wa Diamond kabisa wanatofautiana kwa kiasi kikubwa Sana.Harmonise ndio anaweza kumuhitaji Diamond ili ashine kimziki ndio maana diamond hajawahi kunichukulia Harmonize ni mshindani wake ndio maana hata vijembe anavyorusha harmonize kwa Diamond au ile interview aliyofanya airport hakumjibu lets say angekuwa ni Alikiba ndio kafanya vile Diamond angemjibu fasta kiufupi Ushindani ulikuwa ni wa Alikiba na diamond tu kwa maana walishabiana kwenye vitu vingi ndio ukafanya ushindani wao uwe mkubwa Wana tofauti Sana kwenye fan base, ila ukija kuangalia kea Diamond na Harmo, Diamond kamzidi Sana harmo
 
mleta mada elewa mshindani mkuu wa jadi wa Mondi ni King Kiba na sio Harmo.
Harmo akishuka au Kiba akishuka kimuziki Mondi hawezi kutetereka kwasababu Mondi anajua ku-maintain starndards kwenye soko la muziki.
hivyo Harmo atapita kama alivyopita Hasley ila Mondi atabakia kileleni.
 
Kumlinganisha mtu aliepata sifuri na alie pata mia kwenye mtihani ..hakuna tofauti na ukisefu wa akili
 
Back
Top Bottom