Diamond apata mshtuko deni la mil.800 (TRA WAIKANA BARUA)

Diamond apata mshtuko deni la mil.800 (TRA WAIKANA BARUA)

Ila wabongo kwa saundi noma kuna kipindi nikasikia daimond amenunua mtaa mzima anataka kujenga magholofa tu mara nikasikia amenunua gari ya m.200 kumbe gari yenyewe alizima kwa chief kiumbe yani anafanya kila linalowezekana kuhakisha daimond hashuki kwenye chati kijumla watu wanajua kucheza na media.
 
Diamond kudaiwa kodi ya mapato, Lowassa ahusishwa.

Hali ya taharuki iliyozuka hivi karibuni baada ya meneja wa msanii wa muziki wa kizazi kipya kuandikiwa barua na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ikimtaka kuwasilisha kopi ya mkataba ya kazi ya Nasseeb Abdul pamoja na maelezo yanayoonyesha malipo ya diamond platnumz katika kazi yake ya muziki ndani ya siku saba (7).

Watu wamekuwa wakijiuliza maswali mengi hasa mashabiki wake kwamba kwa nini diamond na sio wengine, ukweli nyuma ya pazia wadhihirika.

Habati za ndani zinasema katika harakati za kutangaza nia za urais za aliekuwa waziri mkuu na Mbunge wa Monduli ndugu Edward Lowassa, ilimbidi amtafute Bw Ruge mutahaba ili kuweza kumpatia wasanii wa kutosha katika tukio hilo ambalo limepangwa kufanyika Arusha mwanzoni mwa mwezi April baada ya pasaka.

Bw Ruge Mutahaba amepatiwa kazi hiyo maalum kwa kile kinachosemekana anawamudu wasanii wengi wa Bongo flava hivyo angewapata kwa bei nafuu zaidi tofauti na vile ambavyo wangepitia kwa Lowassa moja kwa moja.

Katika zoezi hilo la kuwapata wasanii hao limeenda vizuri kwa baadhi ya wasanii isipokuwa kwa msanii Diamond platnumz.

Kama kawaida ya Bw Ruge Mutahaba kupenda kuwabana saana wasanii kwenye malipo ya show zilizo mikononi mwake, alipotaka kufanya hivyo kwa Diamond safari hii management yake ilikuja juu na kukataa kuifanya kazi hiyo yenye maslahi madogo kupitiliza.

Kwa habari za ndani zinasema Diamond platnumz amekuwa akilipwa hela ndogo saana Katika show za Bw Ruge kwa kuwa amekuwa akipata promotion kwa kupigiwa kazi zake bure katika clouds medias.
Mfano, ni show ya 'Diamonds are forever' alilipwa million 3 tuu wakati show iliingiza zaidi ya mil 450.

Katika show nyingine zilizopo nje ya mikono ya Ruge amekuwa akipata 40% ya kile kinachopatikana, 30% anachukua Ruge kwa vile anavyopromote nyimbo zake na 30% anachukua Babu Tale na Mkubwa Fella kama mameneja wake.Hivyo kama kwenye show atalipwa mi5 ,mil2 tu ndo ya kwake awalipe madancers, dj wake, avae nk.

Baada ya Diamond na meneja wake kugomea hela hiyo ndogo, Ruge akamtumia TRA kumkomesha na pia kuanza kumpromote msanii Ally Kiba zaidi hivi karibuni, kama ni msikilizaji wa Radio utakubaliana na mimi.

Ifike mwisho sasa huu ufedhuli na unyonyaji uliopituliza wa Ruge ufikie kikomo, wasanii wamekuwa wakilalamika kila kukicha bila msaada wa aina yeyote na wengine kufikia kujihusisha na madawa ya kulevya kutokana na stress za mapato madogo wanayopata totlfauti na kazi wanazozifanya. Wasanii wanaolalamika ni hata wale waliopo THT wamesikika mara nyingi wakimlaumu Boss wao na kushindwa kupata ufumbuzi wa tatizo hilo.

ANGALIZO: Wasanii muungane umoja ni nguvu bila hivyo mtaendelea kuwa na majina makubwa bila kitu mfukoni.

Nimependa mstari mmoja tu hapa,nanukuu ,
Baada ya diamond na meneja wake kugomea hela hiyo,bwana Ruge "akamtumia"TRA
 
Jiulize ni Kweli anafanya shows idad hiyo kila mwezi na je itabakia Idadi hiyo mwaka mzima.

Kama anahela iyo mbona matibabu ya mama yake tu yamemshinda mpaka wanasiasa wamechangia gharama.

Habari za udaku haziendani hata na mfano wa uhalisia yan hazipo .
 
Habari ya cku nyingi hyoo

Kwa hiyo kama ina ukweli itakuwa imekomaa tayari kwa mavuno. Hivi mbona wale wote waliokuwa wanapiga piga picha na mkulu mstaafu unakuta nyuma ya pazia kuna viskando?
 
na masamaki je waacheni vijana wanaotafuta kwa jasho lao kuliko wezi wanao kula jasho la wananchi kiulaini tu
 
Back
Top Bottom