Diamond ampima DNA ‘Tiffah’

geometry

JF-Expert Member
Oct 30, 2014
466
356
Mitandao ya Udaku Afrika inaripoti kuwa muimbaji kutoka Tanzania Diamond Platnumz amempima DNA mtoto wake ‘Tiffah’ na mpenzi wake ‘Zari’ ilikujua kama yeye ni baba wa mtoto huyo.

Chanzo cha taarifa hizi kinasema kipimo hicho kimafanyika Afrika Kusini siku chache kabla staa huyu hajaenda Las Vegas.

Gazeti la Amani kutoka Tanzania pia limeripoti kufanya mahojiano na Diamond Platnumz.

Diamond alisema “Kutokana na manenomaneno ya watu, ilifika mahali alichoka, akawa njia panda. Hivyo ili kuondoa figisufigisu, akamwambia Zari waende wakampime DNA mtoto na yeye. Ni kabla hajaenda Marekani.”

Vipimo vya DNA vimethibitisha kuwa Tiffah Dangote ni mtoto wa Diamond na sio mtoto wa billionaire Ivan Ssemwanga ambaye ni Ex wa Zari aliyekaa naye kwa miaka 10.

Ivan ana watoto watatu na Zari ambao ni Pinto, Quincy na Didy.

===============
===============

Updates...

Diamond akanusha kuhusu kumpima Tiffah DNA

Mkali wa muziki wa Bongo fleva hapa nchini, Nasib Abdul aka Diamond Platnumz, amekanusha tetesi zakwenda kumpima mtoto wake Latiffah 'Tiffah' vinasaba 'DNA' ili kupata uthibitisho wa kuwa ni mwanawe au sio mwanae.

Diamond amezungumza hayo baada ya kufanyiwa mahojiano na eNewz ya EATV kuhusiana na tetesi hizo ambapo alikanusha suala hilo,

Diamond Anasema kumpima mtoto wako DNA ni kutojiamini na yeye hawezi kufanya hivyo, Diamond anasema alianza kumjua Tiffah akiwa tumboni.

Pia Diamond ameweka wazi kuwa picha inayomuonyesha akilia ni ya show yake ya Dar Live.
 
Udaku tu watu kujipatia pesa, wangeweka na picha basi... eti Baba Tiffah alitokea SA kwenda USA mmmmh
 
Kumtamzama mtoto tu inatosha. Kwa nini mpaka ma DNA, sijui ma Diamond?
TIFA NA MAMA YAKE.jpg
 
hivi huyu kijana na umri wake kweli kaamua kabisa kuapeleka maisha kwa bibi huyo?
sijui atahadithia nini maisha yake ya ujana na mapenzi
 
Mitandao ya Udaku Afrika inaripoti kuwa muimbaji kutoka Tanzania Diamond Platnumz amempima DNA mtoto wake ‘Tiffah’ na mpenzi wake ‘Zari’ ilikujua kama yeye ni baba wa mtoto huyo.

Chanzo cha taarifa hizi kinasema kipimo hicho kimafanyika Afrika Kusini siku chache kabla staa huyu hajaenda Las Vegas.

Gazeti la Amani kutoka Tanzania pia limeripoti kufanya mahojiano na Diamond Platnumz.

Diamond alisema “Kutokana na manenomaneno ya watu, ilifika mahali alichoka, akawa njia panda. Hivyo ili kuondoa figisufigisu, akamwambia Zari waende wakampime DNA mtoto na yeye. Ni kabla hajaenda Marekani.”

Vipimo vya DNA vimethibitisha kuwa Tiffah Dangote ni mtoto wa Diamond na sio mtoto wa billionaire Ivan Ssemwanga ambaye ni Ex wa Zari aliyekaa naye kwa miaka 10.

Ivan ana watoto watatu na Zari ambao ni Pinto, Quincy na Didy.
HAITUHUSU!!!!
 
Back
Top Bottom