Diamond agombee ubunge jimbo la Ubungo

Diamond agombee ubunge jimbo la Ubungo

East African Eagle

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
3,759
Reaction score
2,209
Napendekeza Mwanamuziki Diamond agombee ubunge jimbo la ubungo uchaguzi ujao.

Ubungo kuna vijana wengi wa mitaani ambao Diamond ana uwezo mkubwa si tu wa kuwashawishi wampe kura lakini ana uwezo pia wa kuwasaidia vijana wengi kwa kuwa yeye mwenyewe katokea maisha ya mtaani hadi kufikia hapo alipo kung`ara kimataifa.

Na pia ni kijana aliyekomaa kimikakati ya kimaisha ni rahisi kufunza vijana wenzie.
 
Ubungo kuna vijana wengi wa mitaani ambao Diamond ana uwezo mkubwa si tu wa kuwashawishi wampe kura lakini ana uwezo pia wa kuwasaidia vijana wengi kwa kuwa yeye mwenyewe katokea maisha ya mtaani hadi kufikia hapo alipo kung`ara kimataifa.Na pia ni kijana aliyekomaa kimikakati ya kimaisha ni rahisi kufunza vijana wenzie.

Mwambie akagombee Ilala ndo kuna vijana wengi wanaozurura kila kukicha haswa maeneo ya magogoni, KKoo na Buguruni
 
Diamond yeye amefika hapo kwa kufunzwa na nani? Unafikiri ukifanikiwa katika jambo moja, ni lazima ufanikiwe katika jambo la pili au la tatu? Majimbo uliyoyaona na upungufu wa kile ambacho unafikiri Diamond atakifanya Ubungo, ni jimbo la Ubungo tu?
 
Nakubaliana na wewe. Waliochagua watu kwa kigezo cha muziki kama Sugu kule Mbeya mjini wanajuuuuta kuchagua mvuta bangi
 
Napendekeza Mwanamuziki Diamond agombee ubunge jimbo la ubungo uchaguzi ujao.

Ubungo kuna vijana wengi wa mitaani ambao Diamond ana uwezo mkubwa si tu wa kuwashawishi wampe kura lakini ana uwezo pia wa kuwasaidia vijana wengi kwa kuwa yeye mwenyewe katokea maisha ya mtaani hadi kufikia hapo alipo kung`ara kimataifa.Na pia ni kijana aliyekomaa kimikakati ya kimaisha ni rahisi kufunza vijana wenzie.
Labda Mapunga wenzake awe Mbunge wao.

Hivi Sadifa yupo wapi?
 
Napendekeza Mwanamuziki Diamond agombee ubunge jimbo la ubungo uchaguzi ujao.

Ubungo kuna vijana wengi wa mitaani ambao Diamond ana uwezo mkubwa si tu wa kuwashawishi wampe kura lakini ana uwezo pia wa kuwasaidia vijana wengi kwa kuwa yeye mwenyewe katokea maisha ya mtaani hadi kufikia hapo alipo kung`ara kimataifa.

Na pia ni kijana aliyekomaa kimikakati ya kimaisha ni rahisi kufunza vijana wenzie.

Itabidi wapiga kura wanye gongo na viroba siku hiyo maana akili ya kawaida hapo haihitajiki
 
Ni mawazo ya Kijinga kama kila mtu anayefanya wezapata pesa kwa kuchochea ngono etu leo aje awe mbunge. Kipaji chake yawezekana ni Mipasho ya Mziki na wala awezi kuingia kwenye Siasa akaperform.

Asubirie wabunge wa Kuteuliwa CCM ili awawakilishe vijana kunengua Viuno bungeni. Na tena akijidanganya Kugombea hatafail miserably.
 
East African Eagle

Nilikuwa nadhani wewe ni mtu mwenye fikra pana nà pevu kumbe siku zote nilikuwa najidanganya.In fact your IQ is very low and you such a narrow minded person. If anything, the new constitution should have a section banning uninformed people with poor thinking capacity like you from voting so that we can save our country from possible destruction.
 
Last edited by a moderator:

Umemaliza kutukana? Haya kakojoe ulale
 
Kha,,,,,,!!! Vilaza tu ndio wanaweza kumchagua huyo.
 
Mnaota kuua kipaji cha Diamond... Tayari JK ameasisi ... Hope akina FELA watamshauri vema Zaidi ... Diamond hastahili kujiingiza kwenye siasa, CCM itaua kipaji chake soon akiwaendekeza ... anatakiwa ajikite sana kwenye Muziki huku akiendelea kumshukuru sana Muumba wake kwa Kheri nyingi alizomjaalia ..
 
Nakubaliana na wewe. Waliochagua watu kwa kigezo cha muziki kama Sugu kule Mbeya mjini wanajuuuuta kuchagua mvuta bangi
Kweli Kabisa Mkuu,

Juzi nilikuwa pale MAFIAT, vijana wa pale wanajuta sana kumchagua SUGU, vyote alivyowaahidi hajatekeleza hata kimoja!
 
Vijana kina nani uliokaa nao wakalalamika???

Mmekaa kikao cha chama ambacho kipo against Sugu, ww unadai vijana wa Mbeya wanalalamika, that's absolutely not:sly:
 
Ubungo ni jimbo lisilo na vijana wenye fikra mfu kama zako,Ubungo ni moja ya jimbo lenye wingi wa vijana wasomi nchini!mtafutie jimbo lingine akagombee
 
Achen pumba vijana, diamond aimbe ngololo tu, unataka kulinganisha ubongo wa mnyika na huyo muwaza mapenz tena mtunzwa na Wema, me nadhan aende akalelewe na wanawake maana fani yake mapenzi tu,. Kwa kujua ni kweli weka cv ya mnyika na huyo ngololo ndo ufanye comparisons
 
Back
Top Bottom