PreGE2025 Mgamba ajitosa Ubunge Jimbo la Bariadi Vijijini

PreGE2025 Mgamba ajitosa Ubunge Jimbo la Bariadi Vijijini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,152
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Bariadi Vijijini, Mesela Giligisi Mgamba, leo tarehe 26 Juni 2026 ametangaza rasmi nia yake mbele ya wanahabari na wafuasi wake.

Akizungumza mara baada ya kutangaza nia hiyo, Mgamba amesema kuwa moja ya sababu kubwa iliyomsukuma kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho ni kuona vijana wengi wakikosa ujasiri wa kujitokeza kuomba nafasi za uongozi, jambo ambalo amesema si sahihi.

"Vijana wengi wamekuwa waoga wa kuonyesha nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, kitu ambacho si sawa hata kidogo. Ni vyema wakatambua kuwa waliyoikomboa nchi ya Tanzania walikuwa vijana kama sisi," alisema Mgamba kwa msisitizo.

Aidha, Mesela amesema endapo atapata ridhaa ya wananchi wa Bariadi Vijijini, atahakikisha anasimamia maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kuhakikisha vijana wanashirikishwa kikamilifu katika maamuzi na shughuli za maendeleo.

Mgamba amewahimiza vijana wenzake kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kisiasa kwa kujitokeza kugombea na pia kushiriki uchaguzi kwa kupiga kura ili kuleta mabadiliko chanya katika maeneo yao.

Mwisho, ametoa wito kwa wananchi wa Bariadi Vijijini kumpa ushirikiano katika safari yake ya kuomba ridhaa ya kuwatumikia kupitia nafasi ya ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.
 
Back
Top Bottom