Nilipokua darasa la 5 Nilianza kusikia kitu kama mwiba kinachoma ndani ya moyo nikawa nawaambia walezi wangu kua moyo unaniuma ila walichukulia poa. nami sikua nasema tena jambo hilo. Nikiwa form two hali ilikua mbaya zaid maana nikicheza mpira naumia nashindwa kupumua kifua kinauma natoka jasho nyingi.
Nikapelekwa hospital piga x-ray kifuani kuangalia kama moyo una tundu ila halikuwepo walinikuta tu nina pressure ya kushuka ambayo walisema inasababishwa na ulcers na mawazo. nilikataliwa kucheza mpira na kuombwa nisiwe na mawazo.
2017 hali ilizidi kua mbaya maana moyo ulikua unalipuka tu Anytime,Nikikimbia kidogo naanguka jasho zinatoka ila sikuwahi eleza tena ndugu/wazazi jambo hilo.
Mwaka jana nilikua naenda sehemu na baiskeli nilipofika nikawa nasubiria huduma nimeinama chini moyo ulienza kwenda kasi jasho zikawa zanitoka nikaanguka chini nikapoteza fahamu kifua kilikua kinauma sana macho hayaoni kitu na kichwa kinauma. wasamalia wakanipeleka Zahanati.
Huko nilitulia nikawa sawa wakanipima wakakuta pressure imeshuka sana.Nilikaa sawa nikarudi nyumbani bila kutumia dawa yoyote ila niliambiwa nikapime ECG na Echo ili nijue nini kinafanya moyo kuuma na pressure kushuka.
Baada ya kupima hivyo vipimo nikakutwa na ugonjwa huo wa Rheumatic fever.
Rheumatic fever
Ugonjwa ambao hua Ukiumwa mafua, Kikohozi au Tonsils wale bacteria wa magonjwa hayo hua wana tabia ya kushuka kifuani na kuushambulia moyo. Wakiingia ndani ya moyo hua wanashambulia Valve zinazotoa damu kwenye moyo.
Hivyo nilikutwa Valve mbili za moyo moja imeshakufa kabisa haifanyi kazi na nyingine ndio inafanya kazi kwa shida so inaeelekea kufa nayo maana inaelemewa kazi.
Kumbe ndio maana nikikimbia moyo unauma kifua kinabana nashindwa kupumua naanguka naanza kutoka jasho sababu valve ile inazidiwa nguvu. maana damu inakua inatakiwa isambae nyingi mwilini na valve haikizi mahitaji.
hospital waliniambia kwamba tiba pekee ya kuziwia tatizo Hili ni kuwekewa Moyo bandia. hizo ghalama za kuuweka ilibidi niachane na mawazo hayo kabisa.
ila daktari aliniandikia dawa fulani ambazo zitasaidia kuua bacteria ili ile valve iliyobaki isife mapema. So nimeandikiwa Penadure injection kwa muda wa miaka 6. kila mwez nachoma sindano moja.
Nishachoma kama mara sita ila naona haisaidii Siku zinavyozidi kwenda maumivu yanazidi kuongezeka hapa naandika kifua kinauma kama nimepigwa tofali na hii ipo hivi kila siku. Nikiinama kidogo tu Nashikwa na kizunguzungu nakua napoteza fahamu
Nimepoteza natumaini ya kuishi aisee, kwa hali hii najua muda wowote tu Moyo unasimama. Nilishauriwa nisifanye kazi nziyo,nisiwaze wala Kukimbia maaana nikikimbia tu naweza fanya hiyo valve ife. ikifa nami ndio mwisho wangu. Sijui kama nina miaka 5 mbele nikiwa Hali hii. Inatesa sana plan zangu zote sioni hata maana ya kuzifanya.
Nilikua nakaa naImagine nikiwa na watoto zangu na familia ila ndoto hizo zimeyeykua sitaki niache watoto wasio na baba. Mama yangu nikiongea nae ananiambia nioe au nimtafutie hata mjukuu ili ikitokea nimeondoka abaki na damu yangu atamlea ila naogopa. nilipenda wanangu niwe nao mimi.
Ni Maisha tu. Wote tunapita!!
Samahanini kuwachosha.
NB: Mzazi/mlezi usidharau lolote mwanao analokuambia kuhusu mwili wake, laiti mimi wasingedharau ugonjwa wangu ulikua unatibika mapema tu. Sasa leo hii niko hivi sometimes nalala nahisi kesho sitaamka maana maumivu yanakua makali mno!
Alamsiki [emoji17]