Dhumuni la chapa "666"

Nitamfataje bila kumjua ,nita mjuaje bila kumsoma , sasa wakati namsoma katika vitabu vyake ili nimjue, yeye anakuwa na kundi lake la watu waliomfata kibubusa bila kumsoma, huyu ni Mungu wa vichekesho
 
Nitamfataje bila kumjua ,nita mjuaje bila kumsoma , sasa wakati namsoma katika vitabu vyake ili nimjue, yeye anakuwa na kundi lake la watu waliomfata kibubusa bila kumsoma, huyu ni Mungu wa vichekesho
Mkuu Biblia imegawanywa katika

Historia
Mafundisho
Unabii

kinachofichwa ni siri za ufalme wa mbinguni hasa unabii ila kuhusu kumjua Mungu si unasoma tu historia kuhusu matendo yake makubwa aliyofanya tokea agano la kale kwa kujifunza kuhusu tabia za Mungu kuanzia upendo,uumbaji,neema,rehema n.k sasa ukishajifunza hizo kupitia matendo yake makuu na ukamkubali ndio sasa unaweza pata access ya kujua hizo SIRI.

Na hii sio Biblia tu ni taasisi zote huwezi pewa codes na siri iwe TISS au jeshi au CCM kama wewe sio mwenzao..... Ukishakuwa loyal member ndio utapandishwa ranks na kujua siri zote unazotaka.

Hii ni principle mkuu kote duniani
 
Chapa ya Mnyama Ipo na itakuja, ila itakuwaje na itatekelezwa vipi Bibilia haijasema. Hivyo haya na mengine yatabaki kuwa maoni tu.
Bibilia Inamtambulisha kiunabii mnyama ni Utawala.
Utawala huu utasimama kinyume na mamlaka ya Mungu kwa Kuufanya ulimwengu umsujudie Shetani kwa kuchanganya mambo ya Mungu na Shetani ( ukahaba wa kiroho) kwa kupewa nguvu na tawala za kidunia..
Kwa Sababu hesabu ya jina lake ni ya kibinadamu. Ukokotoo wa Vicalius filii Dei unaoleta na kubeba sifa za mnyama huyu kuwa ni mfumo wa upapa na mawakala zake.



Usitafute kuogopa 666 Tafuta Kumtii Mungu na maagizo yake hayo Mengine atapigana kwa niaba yako. Yawe ni hayo machip yasiwe hayo hayazuii ukweli kwamba ipo siku moja huo unabii utatimia. Na siku sio nyingi.
 
1. Mkuu ccm ni mambo ya kibinadamu yaliyojaa udhaifu mwingi na hofu nyingi ndio maana wanatunza hizo siri zao, labda nikuulize Mungu ana hofu gani ata afanye siri mambo ya mbinguni kwa baadhi ya binadamu ?
2.Nikimsoma katika historia inanionyesha Mungu huyo alikuwa muuaji mkubwa kweli kweli ,hili unasemaje?
 
Kwanini Mungu anafahamu jambo hilo la huo utawala utakao tokea baadaye ambao utasimama kinyume cha mamlaka yake lakini anaacha utokee wakati madhara yake anayafahamu kabisaaa ?
 
Sijui njaa ya asbh,ngoja nitafute. bakuli la uji wa mchele nizimue labda nitaelewa maana kila mstari unajirudia mbele nyuma ,nyuma mbele.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Mkuu Mungu sio kama anaogopa bali anajua wanadamu kwa nature yetu tuna take things for granted kumbuka waisrael toka walipojua ni taifa teule kwa wakati ule walijiona miungu watu na hata wakamsulubu huyo Yesu afterall si walishajua Mungu ni wao tu iwe jua iwe mvua hadi pale Yesu alipokuja kuwanyang'anya huo uteule wao na kuwapa mataifa mengine.

Mathayo 3:9
9 wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto.

Same case kama Siri za ufalme wa mbinguni atapewa mtu yeyote tu awe mpagani au malaika wa shetani watu watachukua things for granted kwamba hata nikifanya dhambi kiasi gani si nshajua jinsi gani ya kufika mbinguni!!

Hivyo kuweka free pass ingekuwa ngumu kujua nani kamfuata Mungu kwa mapenzi yake au kwa sababu tu anataka uzima..... But kwa kuziba access kwa wengine ni sababu anataka wale tu waliomfuata unconditionally na kumuamini ndio awape siri zake ili waufikie ufalme wa mbinguni.

Na ndio maana hata yeye husikia maombi ya watakatifu tu na sio vinginevyo

Methali 15:29
29 BWANA yu mbali na wasio haki;Bali huisikia sala ya mwenye haki.

2. Mungu Sio muuaji , bali aliweka threshold toka mwanzoni alipomwambia hivi Adam.

Mwanzo 2:17
17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.

Mungu alitaka kuishi na sisi milele ndio maana hakukuwa na kifo ila aliweka sharti kuwa tuwe watiifu otherwise tutakufa.... Wanadamu tukasaliti maagizo yake tukamsikiliza shetani na tokea hapo kifo cha kiroho na kimwili kikaanzia hapo.

Na kwakuwa Mungu ndio aliumba Roho sioni kosa kuichukua..... Maana tulipewa choices hapa

Kumb. La Torati 30:19
19 Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;

Kwahiyo either uchague uzima kwa kufuata sheria zake au mauti kwa kuziacha sheria zake!!! Kwahiyo ukisaliti ndio alichukua Roho yake kwahiyo natumia fursa hii kukanusha kuwa Mungu sio Gaidi au ''Mass shooter'' bali alichukua kilicho chake pale kilipomsaliti.

Na ili kuprove hilo ndio maana licha ya dhambu zote na wote waliouawa amesema atawafufua na kuishi nao milele kwenye mbingu isiyo na kifo wala vilio.
Yohana 6:40
40 Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.

Na Nia hii inatimizwa hapa

Ufunuo 21:4
4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.

conclusion haiwezekani Mungu muuaji awe na nia ya kuishi na sisi milele, aifute mauti alafu atufufue siku ya mwisho..... Kwahiyo nakanusha rasmi wazo hili. Unless uje na mstari unaosema Mungu ana nia ya kutuua wanadamu wote!
 
1. Huo udhaifu wote uliozungumza kuhusu wanadamu , Mungu muweza wa yote anaweza kuwapa watu wote siri za mbinguni na binadamu akaishi kwa ustaarabu mkubwa tu, ukiona Mungu nae anajadili udhaifu kama binadamu kwa uoga huo inashangaza kweli, ni hivi Mungu anaweza kuwapa watu wote siri za mbinguni wala isiwe na athari kwake wala kwa watu kwasababu Mungu ni muweza wa kila kitu

2. Bila Mungu kumpa Ibrahim nchi ambayo alikuta wenyeji pale israel ingekuwa salama , kiufupi Muasisi wa mauaji pale israel ni Mungu , hili haliitaji maandiko unayajua
 
Wewe tayari ameshakupa hizo siri zake?
 
MAMBO YA MUNGU MAGUMU. CHA MSINGI WEWE TENDA KWA HAKI, TENDA KWA UPENDO.
 
Na wewe tengeneza 222

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Those people were called heretics.

They did whatever it takes to conceal their precious secrets by codes, cryptic texts, symbols, anagrams, ambigram, allegories, ampersand texts, transliteration writing. They were also smart to preserve their hidden secrets through society with secrets like Rosicrucian Freemasons etc. For they fully understand if they become known by unintended people the world will be at stake.

I agree with you 100%.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa mkuu ,Mungu mwenye ubaguzi mimi anifai
Mungu Hana ubaguzi
"Nawapenda wanipendao,na wote wanitafutao kwa bidii WATANIONA"

Swali je,Unampenda Mungu?!
Unamtafuta kwa bidii????

Kama hayo yote unafanya HAKUNA shida.
Binafsi nilifanikiwa ku Unlock some biblical code
inastajabisha na unaweza Enjoy.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zitto Junior upo vizuri, nilichogundua watu wanachanganya ufunuo wa Biblia na maoni ya wanafilosofia.
 
Wewe tayari ameshakupa hizo siri zake?
Mie najibu kwa msingi wa Biblia inachosema kwa sababu hoja ya mtoa mada ipo ndani ya Biblia sio maoni yangu ni vizuri na ww ujikite kwenye mada kama una maoni yako na ww weka au kama unapinga basi njoo na hoja otherwise kma hufahamu kitu basi jipe muda kasome ndio urudi kujibu mada sio unauliza maswali nje ya mada.

Embu turudishe hadhi ya JF intelligence
 
Mkuu ata hili unataka tulitolee mifano , Mungu mbaguzi ndio maana aliwapendelea Waisrael kuliko watu wengine , mbona liko wazi
 
1. Mkuu nimekuwekea hapo mistari kuwa anafanya hivyo ili tumfuate kwa free will sio kwa conditions sasa akishaweka conditions kwa free will huoni itakuwa ametulazimisha kumfuata???

Mfano leo hii makanisa ya manabii na mitume watu wanaokoka kisa miujiza wanayofanyiwa hivyo wanamuamini Mungu kwa condition kwamba lazima atafanya miujiza ila yeye anataka tumfuate unconditionally that's sio kila kitu anatufunulia mfano utakufa lini n.k maana anajua watu watamfuata unconditionally hivyo since alitoa choice ya free will kwa Adam throughout mpaka kwetu basi hiyo ndio principle anayofuata ila haimaanishi kuwa asingeweza kufanya hivi au vile.

2. Mungu alimpa hiyo ardhi ya Canaan Mr Abraham sababu alitaka kutimiza unabii huu juu ya Canaan mwana wa ham mjukuu wa Noah.

Mwanzo 9
26 Akasema,Na atukuzwe BWANA Mungu wa Shemu;Na Kanaani awe mtumwa wake.
27 Mungu akamnafisishe Yafethi.Na akae katika hema za Shemu;Na Kanaani awe mtumwa wake.


Kwahiyo ili kutimiza Hukumu yake kuwa Canaan atakuwa mtumwa wa Shemu ilibidi kwenye vizazi vya shem yaani Abraham ndio wakatimize huo unabii.

Kuhusu hio amani kukosekana ni sababu Waisrael walishindwa kufuata maagizo kuwa waue Canaan wote kuwa watakuwa mwiba kwake milele.... So kinachoendelea huko middle east ni unabii kutimia kwa mujibu wa Biblia
 
1.FREE WILL , mkuu wewe una free will gani wakati matokeo yako yanajulikana kabla ata ujayatenda ?lugha rahisi Mungu anajua wewe Zitto utakwenda jahanamu au mbinguni kabla ujakufa wala ujazaliwa, sasa free will gani unazungumza wakati matokeo yanajulikana kabla ata ya mechi kuanza ?

2.Huko kutimiza unabii angekufanya kwa hao wawili sio vizazi vyao, wewe huoni kama huko ni kutafuta migogoro kwa lazima , ata ungekuwa wewe umekuta eneo ni mapori hakuna mtu , umejitahidi umelima mapori umejenga mji , halafu mtu anakuja anasema ONDOKA hapa nimepewa na Mungu , wewe ungekubali? huku ni kuasisi migogoro kwa wazi wazi , ndio maana badae akataka wapigane na wenye mji wao wawamalize kabisa ili wabaki wao huu ni unabii au uuaji ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…