A
Anonymous
Guest
Imefika wakati sasa wa kuizungumzia tamaduni inayozidi kushamiri katika baadhi ofisi zetu za umma: Kitendo cha kufanya likizo ya mwaka ionekane kama "kosa la jinai."
Kwa watumishi wengi, kitendo cha kuwasilisha fomu ya kuomba likizo kimekuwa kama chanzo cha unyonge mahali pa kazi. Badala ya likizo kutambulika kama haki ya kisheria na hitaji la kibailojia la mwili kupumzika, kuomba likizo sasa kunachukuliwa kama "usaliti" au uzembe wa kukimbia majukumu ya ofisi.
Mtego wa "Kulipwa Pesa Badala ya Kupumzika"
Tumeshuhudia mwelekeo wa hatari ambapo viongozi wa ofisi wamekuwa wakikataa maombi ya watumishi kwenda likizo kwa kisingizio cha "mrundikano wa kazi," na badala yake kutoa agizo kuwa mtumishi alipwe fedha za likizo (Leave Pay) lakini abaki ofisini kuendelea na kazi.
Ingawa malipo haya ni haki ya mtumishi, si mbadala wa mapumziko. Huwezi kutumia pesa "kununua" akili iliyochoka. Kwa kuweka kipaumbele "uwepo wa mtumishi sebuleni" badala ya "afya ya mtumishi," ofisi zetu zinatengeneza nguvu kazi ambayo; Ipo ofisini kimwili lakini kiakili imechoka vibaya sana, ina msongo wa mawazo unaopelekea makosa mengi katika kutoa huduma kwa wananchi, haina uwiano wa maisha ya kazi na familia, jambo linalopunguza ufanisi wa muda mrefu.
Ni Kushindwa kwa Uongozi, si Wingi wa Kazi
Ikiwa ofisi ya umma au idara fulani ni dhaifu kiasi kwamba mtumishi mmoja akiondoka kwa siku 28 ofisi "inasimama," basi hapo tatizo siyo "wingi wa kazi." Hiyo ni ishara ya kushindwa kwa uongozi. Taasisi imara hujengwa kwa mfumo wa kurithishana majukumu (succession planning) na sio kumtesa mtumishi mmoja bila mapumziko.
Sisi siyo mashine. Sisi ni wazazi, wenzi wa ndoa, na raia ambao tunahitaji muda wa kujichaji upya ili turudi kuijenga nchi yetu kwa nguvu na uadilifu ambao wananchi wanastahili.
Hivyo;
Tunatoa wito kwa viongozi ndani ya taasisi zetu za umma:
1. Heshimuni Ratiba za Likizo: Acheni kuifanya likizo kama "fadhila" ya kuombwa; itambuliwe kama hitaji la lazima la afya na usalama kazini.
2. Komesheni Unyanyasaji wa Kihisia: Mtumishi hapaswi "kuomba radhi" kwa kuchukua mapumziko aliyoyafanyia kazi kwa mwaka mzima.
3. Wekeni Kipaumbele Afya ya Akili: Tambueni kuwa mtumishi aliyepumzika na kuchangamka ana faida kubwa kwa serikali kuliko yule "aliyenunuliwa" kubaki mezani kwa miezi 24 mfululizo bila mapumziko.
Likizo ya mwaka ni haki, siyo kosa. Turudishe heshima ya utumishi wa umma kwa kuthamini utu wa wanaoufanya utumishi huo uwezekane.