Dhima ya mkakati wa kuwa na Plan B

Dhima ya mkakati wa kuwa na Plan B

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,446
Reaction score
829,809
Tumetoka kwenye zama za siasa za fitina, siasa za majitaka, siasa za uongo na kusingiziana... Siasa za propaganda na mashindano ya hoja mitandaoni na kwenye majukwaa....
Tuko kwenye zama za ukatili mkuu mateso na unyama... Hakuna KUBISHANA kwa hoja tena... Hakuna kuvumiliana tena hakuna maridhiano.... Kinachoendelea ni ushetani... Hakuna kupinga wala kukosoa... Ukisalimika sana ni kifungo....
Tuko kwenye nyakati za hatari mno kukichwa kukicha hatujui hatima yetu ni ipi au nani atafuatia... Sasa kwa hali ilivyo ni vema kubadili mbinu na mikakati..
Kwa njia hii tutaokoa vifo vingi
Kwa njia hii tutaokoa majeraha mengi
Kwa njia hii tutaokoa mateso na ukatili mwingi
Kwa njia hii tutaokoa ongekezo la yatima na wajane
Kwa njia hii tutaokoa tutaokoa nguvukazi na think tank kubwa ya taifa
Kuanzia sasa tusijaribu kumzuia yeyote anayeachia nafasi yake kuunga mkono juhudi... Tena ikibidi liwekwe tangazo la wazi kuwa viongozi na wanachama wanaotaka kuhama RUKSAA au tuwaombe list ya wanaowataka kisha tuwaandae na kuwasindikiza kwa maturumbeta...
Hivi tunavyojifanya tunaumia wao ndio furaha yao... Tusiumie tena tuwape tena wakitaka buree ili pesa ya kuwanunua ielekezwe kwenye huduma za kijamii
Wengi hawahami kwa ridhaa yako.. Wanaambiwa wazi kubali uishi... Kataa ufe... Tuchukue maamuzi ya kihistoria tuwaombe LIST ya wote wanaowataka nasi tutawapa
ab21127e9e0e3b5ed430d096484bca2c.jpg
 
Kuliko kuendelea kupoteza watu wetu na tukawe kenge kwenye msafara wa mamba
7bc3842467d9747e4801a0d825110c33.jpg
 
Aisee!
Tunahitaji kupima akili na tabia za watawala kabla..kwa namna hii tutaepuka kuwapata viongozi aina ya Sizonje.
Nakataa hii,Lissu itakuwa mwisho wa career yake,hata Kubenea sidhani kama atabaki salama
 
Kitu watu wasichokijua things comes and goes include vyeo, uongozi, madaraka etc, kuna maisha baada ya utawala 26th/4/ ----
 
Kwa utawala huu uliolaaniwa nakubaliana na wewe mkuu
Mzee umekuwa masihi umeteremshiwa dodoso kutoka mbinguni au unatumia vipimo gani kujua kama huu utawala umelaaniwa na huu umebarikiwa ..?
 
Kaka unakielewa unachosema hapa?

Wengi wetu sio mang’ombe, babu zetu walijitosa baharini baada ya kuamua hawawezi kuishi chini ya minyororo ya utumwa.

Swali ni kwamba upo tayari kutoa uhai wako kwaajiri ya watoto wako, ambao wataimba jina lako vizazi kwa vizazi?
 
Kaka unakielewa unachosema hapa?

Wengi wetu sio mang’ombe, babu zetu walijitosa baharini baada ya kuamua hawawezi kuishi chini ya minyororo ya utumwa.

Swali ni kwamba upo tayari kutoa uhai wako kwaajiri ya watoto wako, ambao wataimba jina lako vizazi kwa vizazi?
Ninachoongea ni mkakati wa muda mrefu... Ulichoniuliza sitaweza kukujibu hapa kwenye open forum
 
Back
Top Bottom