Dharula moja inaweza kufuta akiba zako zote kama hukujipanga

Dharula moja inaweza kufuta akiba zako zote kama hukujipanga

RMK Freelancers Agency

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2025
Posts
298
Reaction score
292
Dharula/emergency au Ugonjwa mmoja unaweza kufuta savings zako zote kama hujajiandaa

Watu wengi wanapanga bajeti vizuri lakini wanapuuza kitu kimoja muhimu sana: emergencies. Dharula haipigi hodi, hujui ni lini utapata malaria, hujui lini mama nyumbani ataugua, mwanao ataharibu mali za watu, hujui lini utapata short ya umeme kwenye nyumba yako au kitasa cha geti kitaharibika. Hujui lini simu yako itaibiwa au kuzima ghafla.
YES, Ugonjwa, ajali, au matatizo ya familia yanaweza kuja ghafla na kuharibu mfumo mzima wa fedha.

Huwezi kuzuia emergency, lakini you can simply get prepared, get ready once they come.

HOW?

Kwanza: Health Insurance/bima ya afya.
Hospitali si mahali pa kufanya maamuzi ya kifedha. Ukifika hospitali bila bima, unalazimika kulipa chochote kinachohitajika wakati huo huo. Kila kipimo utaambiwa ulipie, utalipia dawa zaidi ya moja, hapo ukiwa hujaandikiwa drip au kulazwa.
Kwa mtu anayepata kipato cha kawaida, cha kati au hata kikubwa, bima ya afya ni risk management tool, ni protection ya pesa zako dhidi ya ugonjwa. Bima haizuii ugonjwa kuja lakini ukija bima itahakikisha ugonjwa hauigusi wallet yako, M-pesa yako wala akaunti yako ya benki. Hata kama ni basic cover ya mwaka, inaweza kukulinda dhidi ya gharama kubwa za matibabu ambazo zingeharibu bajeti yako.
Pili: Emergency Fund
Hii ni pesa ambayo haitumiki kula bata, biashara, wala investment. Ni pesa ya dharura tu.
Sheria ya msingi ni;
Emergency fund inapaswa kuwa sawa na gharama za miezi 3 hadi 6 za maisha.
Mfano:
Kama gharama zako kwa mwezi 400k kwa mwezi kuishi, emergency fund inapaswa kuwa kati ya 1.2M – 2.4M.
Faida yake ni nini?
  • Ukipoteza kazi, hautaanza kukopa
  • Ukipata dharura ya afya, hutauza vitu.
  • Unapata peace of mind
  • Ukitaka kutake risk, unakuwa na ujasiri since you have something that "Got your back"

Ni vizuri ukajenga financial protection kabla hujatake risk, au kujenga lifestyle.
Watu wanakimbilia kununua simu mpya, lakini hawana hata akiba ya miezi miwili ya maisha au hata bima.
Jinsi ya Kujenga Emergency Fund
Emergency fund ni pesa ya dharura tu. Haitumiki kwa biashara, starehe, au safari.
Ni pesa ya matibabu kama huna bima, ni pesa ya kutengeneza simu ikiharibika au kuibiwa ghafla(sio kubadilisha simu), pesa ya kufix shot za umeme, matengenezo ya nyumba na furniture au kitu chochote cha ghafla lakini cha muhimu.
Step 1: Tambua gharama zako za msingi
Hizi ni gharama za kuishi tu:
Kodi
Chakula
Usafiri
Umeme na maji
Mahitaji ya msingi
Mfano:
Kodi: 120,000
Chakula: 150,000
Usafiri: 60,000
Bills: 40,000
Total = 370,000 kwa mwezi
Step 2: Weka target ya miezi 3–6
Rule ya personal finance:
Emergency fund = 3–6 months of expenses
Kwa mfano hapo juu:
Minimum target = 370,000 × 3 = 1,110,000
Strong protection = 370,000 × 6 = 2,220,000
Step 3: Anza kidogo lakini consistently
Usisubiri uwe na pesa nyingi.
Mfano:
30,000 kila mwezi
50,000 kila mwezi
Baada ya mwaka mmoja unaweza kuwa na 600,000 – 1,000,000.
Step 4: Weka pesa mahali salama
Emergency fund haitakiwi kuwa investment yenye risk.
Mahali pazuri:
Bank savings account
Mobile money wallet
Money market fund yenye liquidity
Lengo ni kupata pesa haraka wakati wa dharura.
Step 5: Usitumie bila sababu ya dharura
AGAIN, Dharura ni kama:
Ugonjwa
Kupoteza kazi
Ajali
Matatizo ya familia
Sio:
Simu mpya
Safari
Starehe
2. Bima ya Afya Tanzania
Mimi sio mtaalam wa bima. Kwa Ushauri zaidi wasiliana na watoa huduma za bima.
Moja ya dharura zinazo kula fedha na akiba ni gharama za hospitali.
Ndiyo maana health insurance ni sehemu muhimu ya financial planning au mipango ya kifedha.

Mfano wa bima Tanzania ni :
1. National Health Insurance Fund (NHIF)
Hii ndiyo bima kubwa zaidi nchini.
Ina packages tofauti kama:
Ngorongoro Afya
Serengeti Afya
Baadhi ya packages zinaanzia karibu na 150,000 TZS kwa mwaka kulingana na umri na kiwango cha huduma.
Coverage inaweza kufika hadi:
22M TZS inpatient
3M TZS outpatient kulingana na package.
Faida zake:
Network kubwa ya hospitali
Inatumika sana kwa wafanyakazi wa serikali
Gharama yake ni nafuu ukilinganisha na private insurance
2. Community Health Fund (CHF / iCHF)
Hii ni bima ya gharama ndogo inayotolewa kwa ngazi ya wilaya.
Baadhi ya maeneo gharama yake ni kwa kaya kwa mwaka kwa huduma za msingi.
Faida yake:
Bei nafuu
Inasaidia huduma za msingi hospitali za serikali
Hasara:
Coverage yake ni ndogo kuliko NHIF.
3. Private Health Insurance
Makampuni ya bima binafsi pia yanatoa medical insurance.
Hizi mara nyingi:
zina coverage kubwa zaidi
zinatumika sana hospitali binafsi
Lakini gharama yake huwa kubwa zaidi kuliko NHIF.


Personal finance si kuwekeza tu.
Hatua sahihi ya mpangilio wa fedha ni:
1️ Health insurance
2️ Emergency fund
3️ Savings
4️Investment
Watu wengi wanaruka hatua mbili za kwanza, halafu wanashangaa kwanini dharura moja inavunja mfumo mzima wa fedha.

Je, una emergency fund inayoweza kukusaidia kuishi angalau miezi 3 bila kipato?
Na kama huna, ni nini kinakuzuia kuanza kuijenga?
RMK,
WATSAPP:+255 737 450 640

Kwenye channel yetu tunajadili budgeting, saving na investment kwa watu wenye kipato cha kawaida, cha kati na cha juu. Pia unaweza kupata msaada wa kifedha na uwekezaji kwa kupata mawasiliano ya mentors wetu.
Follow the Tanzania Wall Street channel on WhatsApp: Tanzania Wall Street
 
Asante kwa kukumbusha lakin maisha ya binadamu yamejaa mitihani mingi mingine hata inapotokea huwez jua...
Kama kurogwa,starehe,emergence za wakwe,mashemeji na watoto wetu zama hizi wanazingua sana...
Hata insuarance za afya hazikupi mileage ya kutibiwa kila ugonjwa lazma hela itatoka tu...
 
Asante kwa kukumbusha lakin maisha ya binadamu yamejaa mitihani mingi mingine hata inapotokea huwez jua...
Kama kurogwa,starehe,emergence za wakwe,mashemeji na watoto wetu zama hizi wanazingua sana...
Hata insuarance za afya hazikupi mileage ya kutibiwa kila ugonjwa lazma hela itatoka tu...
Yes sir. Ni vizuri kuzingatia emergency zinazokuhusu moja kwa moja. Kumbuka "wewe" kabla ya wengine.
Au niwe straight, be selfish kidogo.
 
Ondoa hofu ya kesho itakuaje, badala yakuwaza utaumwa kesho waza kuwa hutaumwa, badala yakuwaza kupata hasara waza kupata mapene zaidi, hofu ni ugonjwa unaopandikizwa kwa agenda za kisirisiri sana.
 
Ondoa hofu ya kesho itakuaje, badala yakuwaza utaumwa kesho waza kuwa hutaumwa, badala yakuwaza kupata hasara waza kupata mapene zaidi, hofu ni ugonjwa unaopandikizwa kwa agenda za kisirisiri sana.
Wazo zuri, Lakini ni vizuri kufanya strategic thinking kuliko kutumia hisia hasa kwenye maswala ya kifedha.
 
Maisha ya watu wa hali ya chini hadi kusogea wenye uchumi "wa kati mwisho" huwa hawana bajeti.Maisha yanaenda kimungumungu tu.Hewala yapite.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom