Nilifanya kazi na watu wa bondeni katika mambo ya migodi, na niligundua kwamba wengi wao wanapoongelea nchi nyingine za Afrika wanatumia neno Afrika, kama vile South Africa haiko Afrika. Yaani utakuta mtu aliyeko Johannesburg akiwa na safari ya Tanzania anasema "Kesho ninaenda Afrika".
Sasa nimeona kwenye habari za bondeni kwamba Zuma amenukuliwa akihutubia na kutamka maneno yafuatayo, "We cant think like Africans in Africa, generally. We are in Johannesburg, this is Johannesburg (Tafsiri: Tuache kufikiri kama Waafrika katika Afrika. Tuko Johannesburg, na hapa ni Johannesburg".
Je, Zuma alimaanisha watu wa nchi za Afrika hawana akili nzuri kama watu wa bondeni?
Bila shaka maneno haya yataudhi watu wengi ndani ya Afrika, na hasa Malawi ambayo aliitamka katika hotuba yake. Hadi sasa amekuwa akielekezewa lawama tele.