Ifururu
JF-Expert Member
- Dec 28, 2017
- 549
- 626
Kwa mara ya kwanza naingia hapa katika benki ya Equity,nashangazwa na mwenendo wa huduma ninazozikuta hapa katika ofisi yao mkoani Morogoro.Kama hapa manispaa huduma zimedorora namna hii,je vipi kuhusu huko vijijini ambapo wana matawi?
Nimekutana na daftari la maoni hapa,inaonesha huwa hawapitii maoni ya wateja wao.
Wateja wengi wanalalamikia suala zima la mikopo,kwamba kuna ucheleweshwaji mkubwa wa mikopo,yaani inachukua mpaka wiki sita mpaka nane kupata mkopo,na hapo ni baada ya kuwa mteja ameshakamilisha taratibu zote za kupewa mkopo.Benki nyingine wanatoa huduma ndani ya saa 24,yaani kama mteja amekamilisha kila kitu basi ndani ya saa 24 ameshachukua chake na kutatua mambo yake.
Kama EQUITY Bank mmeishiwa,mnashindwa kukopesha kwanini msifunge mikopo?
Mnakera wateja wenu.