Customer Care Tanzania na saa 24

Lyetu

JF-Expert Member
Feb 11, 2018
1,114
2,946
Habari za usiku wapendwa katika Bwana.

Nijikite moja kwa moja kwenye mjadala hususan ni kwa kampuni zinazotoa huduma za kifedha.

Tunashukuru tunapata huduma za kifedha masaa24, unaweza kutuma fedha, kutoa, kufanya manunuzi n.k

ILA
1. Licha ya huduma hii muhimu kupatikana masaa24 ila msaada haupatikani Masaa24 (hapa namaanisha usiku). Ukipatwa na changamoto inayohitaji msaada wa haraka utaambiwa idara husika hawapo kwa wakati huo na utaombwa usubiri ndani ya masaa24.

2. Kuna wakati unaweza kununua luku au kuhamisha fedha kupitia app labda ya bank fulani na usipate huduma, ukipiga Simu utaambiwa kuna tatizo (hawakutoa taarifa kwa wateja kuhusu hilo tatizo) na utaombwa usubiri masaa 24.

Hii inaleta usumbufu mkubwa sana, na ni aibu kwa ulimwengu wa sasa kumsubirisha mteja masaa24 kwa huduma muhimu kama hii.

Wakati mnafanya jitihada za kuboresha huduma za kifedha msisahau kutengeneza mazingira rafiki yanayoendana na uhalisia. Haiwezekani unatoa huduma za kifedha kukiwa na tatizo kwenye mifumo yako hutoi taarifa pia mteja akipatwa na changamoto huwezi kumsaidia kwa wakati.
 
Back
Top Bottom